Rais Magufuli: Upone haraka,tunakuhitaji

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,280
25,859
Rais John P. J. Magufuli,alipomtembelea Maalim Seif Sharrif Hamad leo amemtakia Maalim heri na kupona haraka. Pia,Rais Magufuli ametamka kuwa Maalim Seif anahitajika,ingawa hakusema ni wapi.

Kimsingi,kauli ya Rais Magufuli imeonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kukiri kuwa hata wapinzani wanahitajika. Binafsi,naitafsiri kauli ya Mhe. Rais kama ni kauli ya kutambua umuhimu wa Maalim Seif katika kutatua mgogoro wa kisiasa na kikatiba wa Zanzibar.

Hongera Rais Magufuli kwa kauli komavu ya kisiasa na moyo wako wa kutembelea wagonjwa.
 
Taratibu unapona dogo.
 
Talking and acting are two different things. Moja ya upungufu wa Magufuli ni kutothamini upinzani. Katika hotuba zake nyingi lazima auponde upinzani. Kinachoendelea Zanzibar kinaonyesha kauli yake ni ya unafiki. Na ndio maana huwa nasema kama kweli Mungu yupo basi ni wengi tutaadhibiwa... Unakumbuka msemo wake anaoupenda sana wa 'msema kweli ni mpenzi wa Mungu''?
 
Sasa ni unafiki.
wamemnyima ushindi,amemwambia hawezi kuingilia tume ya uchaguzi na amepeleka majeshi ili kulinda wizi wao,halafu anakuja kukuona kiunafiki.
 
Wangekuwa wanamhitaji wangemkabidhi ushindi wake. Hapa wanapiga porojo tu.Huyu Magufuli mwenyewe ndiye aliyekuwa kinara wa kubeza wagonjwa kipindi cha kampeni mwaka 2010.
 
Sasa ni unafiki.
wamemnyima ushindi,amemwambia hawezi kuingilia tume ya uchaguzi na amepeleka majeshi ili kulinda wizi wao,halafu anakuja kukuona kiunafiki.
Kwani angesema UGUA POLE kuna shida? Ya nini kusema unafiki? Tangu Lini CCM wakamuhitaji mpinzani wakati wamekuwa wakitishia upinzani mpaka kufikia kuua baadhi yao?
 
Kuna mtu jaba alilamika amezulumiwa millioni mbili yake na mshikaji .mimi nikamwambia hapa tanzania yupo mtu amezulumiwa URAISI mara 5na bado yupo na anaishi
 
Rais or Raisi?
Ni Rais na si Raisi kama unavyotaka wewe,usiharibu lugha yetu. Pengine si mtanzania wewe maana nadhani kuuliza kwako ama unataka kujifunza au umekosa cha kukosoa kwa kuwa ni mkosoaji wa kila kitu. Umeona post hiyo haina cha kukosoa ndo ukaamua uibuke na rais au raisi napo umemkosa pa kumkosoa mleta mada.
 
Talking and acting are two different things. Moja ya upungufu wa Magufuli ni kutothamini upinzani. Katika hotuba zake nyingi lazima auponde upinzani. Kinachoendelea Zanzibar kinaonyesha kauli yake ni ya unafiki. Na ndio maana huwa nasema kama kweli Mungu yupo basi ni wengi tutaadhibiwa... Unakumbuka msemo wake anaoupenda sana wa 'msema kweli ni mpenzi wa Mungu''?
Talking and acting are two different things. Moja ya upungufu wa Magufuli ni kutothamini upinzani. Katika hotuba zake nyingi lazima auponde upinzani. Kinachoendelea Zanzibar kinaonyesha kauli yake ni ya unafiki. Na ndio maana huwa nasema kama kweli Mungu yupo basi ni wengi tutaadhibiwa... Unakumbuka msemo wake anaoupenda sana wa 'msema kweli ni mpenzi wa Mungu''?
Huo msemo aliutumia katika kuomba kura.
Mungu yupo kwa haki na ukweli
Wakati siasa ni ulaghai,ujanja ujanja, usanii ,ahadi hewa alimradi avute hisia za wapiga kura wamuamini kwa kuwa amemuingiza mungu ndani ya kampeni yake.

Kuna wakati Mungu hutumika kama blanketi kwa madhumuni fulani fulani wakati wa baridi blanketi linahitajika na wakati wa joto blanketi halina thamani. hivyo ndivyo wanasiasa humtumia Mungu kama blanketi kwa lugha tamu tamu wanapoyapata mahitaji yao humsahau kabisa na hutawasikia tena wakimtaja mpaka mahitaji ya kumtumia yatakapojitokeza tena
 
Back
Top Bottom