Rais Magufuli una bifu gani na Hussein Bashe?

Rais Magufuli una bifu gani na Hussein Bashe?

Bashe amefanyia kazi zile semi za 'mtumikie kafir upate mradi wako' na 'ukienda Roma ishi kama wa Roma'....sasa yupo mezani ametulia tuli anachapa zake pork chop kwa kwenda mbere.
Bashe alisimamia upande wake anaouamini. Hakuwa hivyo unavyomsemea
 
Hakuna yeyote anayemjua yeyote, tunandika kwa uzoefu.
Watu wanaishi na wake zao miaka na miaka na hawajui kwamba wake wana watoto wa "nje", itakuwa Magufuli mtu wa kumsoma magazetini?

Pia, kumjua mtu inahitajika huyo mtu awe na consistency.Nyerere alikuwa na consistency, kwa sababu alielewa anataka kufanya nini. Kama alichotaka kufanya ni kizuri, alifanikiwa au hakufanikiwa, hayo ni mambo mengine.

Magufuli kumjua ni ndoto, kwa sababu hana consistency na sijui hata kama yeye mwenyewe anajua anataka kufanya nini.Mara anatukana wastafu waliomtangulia, mara anaongelea umuhimu wa kuwa na fadhila kwa watu waliokusaidia kufika ulipo.

Mara anasema anapiga vita rushwa, mara anasema ukimpa traffic police kitu kidogo ni hela ya brush ya viatu tu!

Amejaa contradictions, sasa mtu anayesema anamjua, atamjua wapi wakati mtu mwenyewe kajaa contradiction?

Na kama sharti la kuandika hapa ni kumjua mtu vizuri, hakuna atakayeandika lolote kuhusu yeyote.

Hizi ndizo calculations zilizoendelea.

Laowassa karudi kundini. Bashe ni team Lowassa, anarudishwa kundini.

Zaidi, Bashe akiwa kundini atanyamazishwa vizuri zaidi kwa "collective responsibility".

Zaidi kabisa, Magufuli si kwamba haoni watu wanaoshusha nondo kama Bashe, anawaona, tatizo linakja anapojiweka yeye kujua kila kitu.Tatizo linakuja kwenye mfumo huko kutumia ushauri in a comprehensive way.

Kumteua Bashe kuwa junior minister ni kazi ndogo, kufanyia kazi mawazo yake ambayo yanaonesha udhaifu serikalini ni kazi kubwa.
Kiranga kwa hili nakuunga mkono, mchezo wa siasa za Magufuli hazitabiriki, huwa anatafuta watu wa kuwatoa kafara.
 
Bashe amefanyia kazi zile semi za 'mtumikie kafir upate mradi wako' na 'ukienda Roma ishi kama wa Roma'....sasa yupo mezani ametulia tuli anachapa zake pork chop kwa kwenda mbere.
Aisee! Wewe kweli duuh! Noma sana. Aisee una mawazo ya kikamba kweli.

No, ulimwengu wa leo hauko hivyo. Unajua, nilitegemea vijana wa leo kama nyie sio kuwa watu tena wa kuwaza upuuzi kama huo. Enzi zetu za Mwalim Nyerere ningeweza sema uko right, lakini katika karne hii 21 na maendeleo yote haya ya teknolojia katika kitengo cha mawasiliano, nisinge tegemea kusikia kijana kama wewe ukiwa na mawazo haya.

Nyie vijana wa leo mna bahati kubwa sana ya kuishi katika bahari ya Information Technology kifupi IT. Kwa hali hiyo nilitegemea nyie kuwa watu wenye mawazo mapana sana ya maisha, kwani mnashuhudia mengi yanayo tokea ulimwenguni kupitia hiyo Technology development. Kwa hali hiyo nina uhakika kuwa katika Generation yenu nyie sio watu tena wa kuburuzwa buruzwa kama enzi zetu sisi.

Nyie ni vizazi vya watu wa kujiamini sana na watu wenye msimamo mkubwa, kwani mara nyingi mna tetea mawazo yenu kwa hali na mali kwa kutumia mifumo ya kisasa ya mawasiliano ya habari

Nasema haya kwa sababu naona hivi sasa Europe pia, jinsi gani teen agers wanavyo kuwa mashupavu katika kushikilia ideology yao ya mazingira.

Yalianza na msichana wa kiswidish mwenye umri wa miaka 16 Greta Thunberg huko Stockholm, Sweden na kusambaa Europe nzima, hasa huko Ujerumani ndiyo mambo moto moto. Wanafunzi wa shule za msingi, Secondary na hata high schools baadhi ya siku hawaendi shule wakidai upatikanaji wa ufumbuzi wa matatizo yanayo ikabali dunia kutokana na climate changes.

Naibu Waziri mpya wa Kilimo Mh. Bashe nahisi sasa yuko katika nafasi ambayo nyota yake ilikuwa ina mwongoza. Nategemea atajitahidi kuyatekeleza yale ambayo mwenyeezi Mungu amempangia kuyatekeleza kwa manufaa yetu wote.

Sisi tunacho taka ni maendeleo yetu watanzania kama ambavyo Rais wetu mpendwa ameyaanzisha na sisi wote kushuhudia.

Kuwa positive na mpe naib waziri nafasi.

Nilitegemea Rais Magufuli angeyafanya haya yote kwa mda mfumo hivi? Sidhani! Lakini kwa ujasiri wake kama binafam na mwanamme mwenye msimamo amefanikisha.

Hizi ndiyo tabia za majasiri ya wenzetu wazungu walio waletea wenzao maendeleo. Tukiendelea hivi nafikiri Tanzania tunaweza tukiwa trend setter wa mabadiliko ya maisha ya watu warusi Afrika. Ngoja tuone!! Mimi generally niko very very optimistic na haya ambayo Rais wetu Buldozer ameyaanzisha.

Namwombea uzima na afya njema ili aendelee kutuleta maendeleo chanya na hivyo ukombozi wa maisha bora na uhuru wa kiuchumi.
 
Back
Top Bottom