Rais Magufuli umetuvuruga wala sio siri tena. Hotuba yako ya leo Chato imezidi kuleta taharuki

Kingjr2

JF-Expert Member
Sep 8, 2018
644
1,271
Hii ya leo ni funga kazi! Wananchi tunajiuliza. Dunia mzima inatoa takwimu za uongo au ni Vipimo vyetu tu ndo vinadanganya au Wataalamu wetu tu ndo hawana ujuzi stahiki wa kuvitumia?

Maswali mengine tunayojiuliza na yametuvuraga sana sana ni :-

Je, kuanzia leo watu hawapimwi tena Korona? Watapimwaje na Vipimo vimepima mbuzi zikawa positive?

Kuanzia leo Waziri Mkuu na Waziri wa Afya hawatatoa tena update za walioambikizwa wala waliopona! Watazitoa wapi wakati vipimo haviko sawa?

Ni nani atakubali kuambiwa yuko positive wakati hata mapapai yako positive?

Walioko chini ya uangalizi wa wataalamu wataendelea kubaki huko wakati kipimo kilichowapima kimepima mafenesi na yamekutwa na Corona? Wana uhakika gani kama kweli wanaumwa wakati vipimo haviko sawia?

Ugonjwa upo na unaua na Rais amekiri hivyo, mbona hasemi mikakati iliyowazi kuudhibiti?

Kila siku tunaambiwa ni Vita vya kiuchumi, hilo liko wazi na hasa kwa mataifa makubwa.

Lakini hapa tunajiuliza pia, kwani hii Vita ya kiuchumi imeelekezwa Tanzania pekee? Yaani sisi ndo walengwa wakuu wa hii Vita ya kiuchumi kupitia Korona!? Mbona kama sielewi

Tukiacha kufuata ushauri wa kitaalamu wa WHO na wengine mataifa mengine wakafuata, huo uchumi wetu wenyewe hautegemei hizo nchi?

Tukijifungia ndani ya mikoa yetu au hata wilaya zetu (simaanishi watu wote kuwa ndani) halafu tukaruhusu safari za mizigo tu kwa utaratibu maalum kwa wiki kadhaa huo uchumi unaokufa kwa wiki tatu hadi sita tutashindwa kweli kuufufua kwa miaka kadhaa ijayo baada ya Korona?

Kwa kweli Mimi nimevurugwa kabisa! Yaani Mkuu wetu anasema Ugonjwa upo na unaua kweli kweli!! Halafu anasisitiza tena tuendelee kuchapa kazi it is not to that extent!!!

Hiyo to that extent anayotaka ifikiwe ni hadi tufe Milioni moja ndo waamini kwamba it is that extent!?!? Kwamba waanze kuzikwa watu 1000+ kwa siku ndo watakubali it is that extent!?

KWA MAONI YANGU HOTUBA KAMA HII YA LEO NDO INAWEZA KULETA TAHARUKI KWA JAMII KULIKO HATA HIZO IDADI ZA VIFO NA MAAMBUKIZI ZINAZOPINGWA NA KINA MWIGULU

Mstaafu Kikwete aliwahi kusema "za kuambiwa changanya na zako"

Stay home be safe! Vingine vyote tutakufa na wanaotuzika watakosekana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkurungenzi mkuu wa maabara ya taifa mara baada ya hutuba ya Rais hivi leo!
africansafaris_B_iSBULpOZZ.jpg
 
Hii ya leo ni funga kazi! Wananchi tunajiuliza. Dunia mzima inatoa takwimu za uongo au ni Vipimo vyetu tu ndo vinadanganya au Wataalamu wetu tu ndo hawana ujuzi stahiki wa kuvitumia?

Maswali mengine tunayojiuliza na yametuvuraga sana sana ni :-

Je, kuanzia leo watu hawapimwi tena Korona? Watapimwaje na Vipimo vimepima mbuzi zikawa positive?

Kuanzia leo Waziri Mkuu na Waziri wa Afya hawatatoa tena update za walioambikizwa wala waliopona! Watazitoa wapi wakati vipimo haviko sawa?

Ni nani atakubali kuambiwa yuko positive wakati hata mapapai yako positive?

Walioko chini ya uangalizi wa wataalamu wataendelea kubaki huko wakati kipimo kilichowapima kimepima mafenesi na yamekutwa na Corona? Wana uhakika gani kama kweli wanaumwa wakati vipimo haviko sawia?

Ugonjwa upo na unaua na Rais amekiri hivyo, mbona hasemi mikakati iliyowazi kuudhibiti?

Kila siku tunaambiwa ni Vita vya kiuchumi, hilo liko wazi na hasa kwa mataifa makubwa.

Lakini hapa tunajiuliza pia, kwani hii Vita ya kiuchumi imeelekezwa Tanzania pekee? Yaani sisi ndo walengwa wakuu wa hii Vita ya kiuchumi kupitia Korona!? Mbona kama sielewi

Tukiacha kufuata ushauri wa kitaalamu wa WHO na wengine mataifa mengine wakafuata, huo uchumi wetu wenyewe hautegemei hizo nchi?

Tukijifungia ndani ya mikoa yetu au hata wilaya zetu (simaanishi watu wote kuwa ndani) halafu tukaruhusu safari za mizigo tu kwa utaratibu maalum kwa wiki kadhaa huo uchumi unaokufa kwa wiki tatu hadi sita tutashindwa kweli kuufufua kwa miaka kadhaa ijayo baada ya Korona?

Kwa kweli Mimi nimevurugwa kabisa! Yaani Mkuu wetu anasema Ugonjwa upo na unaua kweli kweli!! Halafu anasisitiza tena tuendelee kuchapa kazi it is not to that extent!!!

Hiyo to that extent anayotaka ifikiwe ni hadi tufe Milioni moja ndo waamini kwamba it is that extent!?!? Kwamba waanze kuzikwa watu 1000+ kwa siku ndo watakubali it is that extent!?

Mstaafu Kikwete aliwahi kusema "za kuambiwa changanya na zako"

Stay home be safe! Vingine vyote tutakufa na wanaotuzika watakosekana!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimemaliza siongei tena
 
Attachments

  • IMG-20200503-WA0045.jpg
    IMG-20200503-WA0045.jpg
    10.7 KB · Views: 1
  • IMG-20200503-WA0046.jpg
    IMG-20200503-WA0046.jpg
    20.3 KB · Views: 1
  • IMG-20200503-WA0043.jpg
    IMG-20200503-WA0043.jpg
    52.2 KB · Views: 1
  • IMG-20200503-WA0044.jpg
    IMG-20200503-WA0044.jpg
    48.3 KB · Views: 1
  • IMG-20200503-WA0049.jpg
    IMG-20200503-WA0049.jpg
    49.2 KB · Views: 1
  • IMG-20200503-WA0047.jpg
    IMG-20200503-WA0047.jpg
    77.5 KB · Views: 1
  • IMG-20200503-WA0048.jpg
    IMG-20200503-WA0048.jpg
    37.1 KB · Views: 1
Akihutubia Taifa kutokea Ikulu ya Chato, Rais Magufuli ameonesha kutokuwa na imani na majibu ya vipimo vya Covid-19 vinavyotolewa na Maabara kuu ya Taifa, Dar es Salaam. Bila kupepesa macho ameonesha kutokuwa na imani na Mkuu wa maabara ya Taifa kwa kile alichosema aliwaamuru watu wake wapeleke sampuli zinazotokana na mapapai, mafenesi, nyanya, Mbuzi, Kondoo na Sungura na matokeo yake Mafenesi na Mbuzi waliopewa majina ya binadamu walifundulika kuwa na maambukizi. Kutokana na majibu hayo ametoa wito kwa watanzania kutotishika na ugonjwa huu. Kwa maana halisi ni kwamba tatizo siyo kubwa tunatishwa tu kumbe majibu mengine ni ya sampuli za Mbuzi na Mafenesi.
Je, hii hotuba inapunguza au kuondoa hofu au ndo inaongeza?
Kwa nini yeye kama Rais hatoki hadharani akasema nini kifanyike badala ya kuendelea kutumia mafumbo na kuwasimanga wasaidizi wake kama alivyomnanga Leo Mkuu wa mkoa wa Mtwara?
1.Je, sasa Watanzania watashusha pumzi kwamba walikuwa wanadanganywa kumbe tatizo siyo kuubwa kiasi hicho Bali vipimo na wapimaji ndio walikuwa wanaongeza takwimu?
2.Au hofu itaongezeka baada ya hotuba, kwa Watanzania kujua ukweli kwamba maabara yao kuu inatoa majibu feki na kwamba waliombiwa hawana maambukizi labda wanayo na ndo maana watu wanakufa ghafla?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunapo elekea ndio pa baya sana. Makonda pamoja na madhaifu yake lakini alijitahidi kwa kupulizia lakini aliitwa mpumbavu.

Rc wa mtwara na yeye kapata yake leo. Viongozi wa dini walio funga makanisa na misikiti wameambiwa hawana imani,tena kuwaambia viongozi wa dini hawana imani ni tusi kubwa sana ni sawa na kumwambia mwanaume husimamishi.

Nahisi viongozi wa dini na waserekali wataogopa kufanya mapambano dhidi ya corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kule MADAGASCAR huku TANZANIA ! Mapambano dhidi ya gonjwa COVID-19
Hii itasomeka Duniani ndani ya masaa machache yajao!
Viongozi nchi jirani lazima watapigiana simu,maana walikuwa wanasema tuko nyuma katika mapambano!!!!
 
Back
Top Bottom