Rais Magufuli umemsikia Rais wa Ufilipino?

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
12,485
50,898
Rais wa Ufilipino amewaonya wananchi wa nchi hiyo na wakiwemo maseneta na wafanyabiashara wa kawaida kuwa atawapiga risasi na kuwauwa kama wapo kwenye list ya wauza madawa aliyo nayo..

List yote Niko nayo na nitawapiga risasi wote wanaouza madawa ya kulevya bila kujari ni watu wakubwa Serikalini au ni mfanyabishara mkubwa.....

Naomba rais Magufuli aige misimamo ya huyu jamaa njia za kupambana na wahujumu uchumi kupitia kuuzwa kwa madawa ya kulevya na kuua vijana wetu imefikia pabaya sana.

Hizi ndio issue za Ku deal nazo nafikiri umemsikia.

Hao ndio strong leader tunaowataka wanao deal na issue sio ku deal na wapinzani..
 
Huku kwetu anajinasibu kupambana na rushwa anahonga wabunge wa CCM milioni 10 kila mbunge wa chama chake wapitishe muswada wa habari bungeni.
Watuhumiwa wa kuhujumu uchumi wanafutiwa mashtaka na kuachiwa huru lakini Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema ambaye ameonyeshwa maono yupo mahabusu leo zaidi ya siku 40 dhamana yake imezuiwa.
 
Hasa wale waliokuwa wavuta ndumu kule Katoke sec na pale Lake wapigwe risasi haraka sana
 
nadhani ngada ina madhara kwa watoto wa dar si salama mikoa mingine sio sana (japo inabidi atilie maanani) sisi adui yetu mkubwa kwenye nchi hii NJAA, akitangaza vita na njaa nitamuona kweli yeye ni m'babe, kauli ya kusema bongo hamna njaa ili kuwakomoa wanaotoa taarifa ni udhaifu mkubwa sana. AKISHINDWA KUPAMBANA NA NJAA ASAHAU KUSHINDA VITA DHIDI YA NGADA!
 
Acha kumshauri mkuu wa nchi ujinga nchi hii inaongozwa kwa sheria uwezi kupiga watu risasi kisa una list ambayo imeandikwa tu bila watuhumiwa kufikishwa mahakaman na kujibu tuhuma pia sheria zetu hazisemi muuza madawa adhabu yake ni kupigwa risasi sio kwamba nawatetea no wapelekwe mahakaman mahakama itahamua.
 
Rais wa Ufilipino amewaonya wananchi wa nchi hiyo na wakiwemo maseneta na wafanyabiashara wa kawaida kuwa atawapiga risasi na kuwauwa kama wapo kwenye list ya wauza madawa aliyo nayo..

List yote Niko nayo na nitawapiga risasi wote wanaouza madawa ya kulevya bila kujari ni watu wakubwa Serikalini au ni mfanyabishara mkubwa.....

Naomba rais Magufuli aige misimamo ya huyu jamaa njia za kupambana na wahujumu uchumi kupitia kuuzwa kwa madawa ya kulevya na kuua vijana wetu imefikia pabaya sana.

Hizi ndio issue za Ku deal nazo nafiki umemsikia.

Hao ndio strong leader tunaowataka wanao deal na issue sio ku deal na wapinzani..
Nawe hueleweki, unatetea nini sasa! Tanzania kuna watu!
 
Thubutu yako, unawajua wauza unga wa Tz wewe? atampiga risasi mtoto wa naniliu halafu iweje? it will never happen on our land.
 
Rais wa Ufilipino amewaonya wananchi wa nchi hiyo na wakiwemo maseneta na wafanyabiashara wa kawaida kuwa atawapiga risasi na kuwauwa kama wapo kwenye list ya wauza madawa aliyo nayo..

List yote Niko nayo na nitawapiga risasi wote wanaouza madawa ya kulevya bila kujari ni watu wakubwa Serikalini au ni mfanyabishara mkubwa.....

Naomba rais Magufuli aige misimamo ya huyu jamaa njia za kupambana na wahujumu uchumi kupitia kuuzwa kwa madawa ya kulevya na kuua vijana wetu imefikia pabaya sana.

Hizi ndio issue za Ku deal nazo nafikiri umemsikia.

Hao ndio strong leader tunaowataka wanao deal na issue sio ku deal na wapinzani..
Hivi sasa tu mnalia mnalengwa wapinzani,akifanya hiyo si ndio chadema yote itahamia ulaya na marekani kupeleka fitna
 
Kweli kabisa.

Sijawahi kumsikia akizungumzia vita ya madawa ya kulevya toka siku ile azindue bunge.

Hayupo serious kwenye issues za muhimu..

Kazi kukimbizana na Lema na yule dogo wa Ifakara.
Kama mafisadi tu kutumbuliwa watu wanalalamika kwamba anakiuka haki za binadamu sembuse kuwauwa wauza madawa si itakuwa hatari??
 
Back
Top Bottom