Mh,Raisi,ulipokuwa wilayani Arumeru kuzindua mradi mkubwa wa maji, ulitamka maneno magumu na mazito kwa akili za wengi kuyaelewa! Lakini kwetu sisi tuliona pengine kilio na machozi yetu ya muda mrefu, ya zaidi ya miaka 26, ya kukandamizwa,kupigwa,kufungwa na kudhulumiwa ardhi yetu yamefika kitini mwa Mwenyezi Mungu. Naye anataka kupitia kwa mkono wako ayafute machozi yetu!!
Mh,Raisi wetu mpendwa,mbali migogoro kadhaa inayosumbua wilaya yetu, upo mmoja ambao usingelipaswa hata kidogo kuwepo.Nao Ni wa shamba la Arusha Coffee estate ex.112. lililoko katika kitongoji Cha Maksoro na Moivaro,katika Kijiji Cha Nguruma wilayani Arumeru!
Shamba hilo lenye eka 721 katika hali isiyo ya kawaida,limeshafutwa (revocade) Mara 2.mwaka 1990 na baadae 2001.sababu ya kufutwa Mara mbili Ni kukengeushwa kwa maagizo halali ya serikali kuu na kutoa shamba hilo kwa mtu mmoja badala ya kuwapa wananchi Kama ilivyokuwa imeagizwa!
Na hapa ndipo, chanzo kikuu Cha madhila mabaya na maovu makubwa mno yalipo Anza kutupata wananchi tuliokuwa tayari tumeshajenga makazi ya kudumu hapo.watesi wetu walitumia nguvu ya dola na hata vijana wa kukodi kutuhamisha,kubomoa,vipigo kesi za kumbikwa nk, ilimradi tusalimu amri. Kwa jinsi mateso na kilio Cha wanachi kilipoongezeka, hatimae serikali ya mweshimiwa Mkapa, ilionelea ifute kwa upya kwa kufuata hatua zote za kisheria(nyaraka zote tunzo), na mnamo mwaka 2001 serikali kuu ikawaagiza serikali ya wilayani ya AruMeru kugawia wananchi shamba hilo bila Jambo jingine lolote...!!(kwa maneno mengine mgogoro wa shamba hilo ulimalizwa tangu 2001)
Rais huwezi Amini,mpaka sasa haki hiyo haijatolewa!!!!!na hakuna sababu yeyote ya msingi.
Raisi wetu,katika kufuatilia haki hiyo iliyowazi, tulibahatika kufika Dodoma tukiwa na aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji hicho (CCM)kwa kipindi chote Cha mgogoro, na ambàye Ni makamu kamati hii,Mzee Charles Amosi, tukafanikiwa kukutana na Mh.Ashasante Nditie,kipindi hicho akiwa mwenyekiti kamati ya ardhi ya Bunge,na sasa naibu waziri. Pia mh. William Lukuvi waziri wa ardhi.kwa pamoja na kwa namna tofauti walitusaidia Sana.
Waliridhishwa na vielelezo na documents zetu zote.Mh. Lukuvi, kiukweli alihuzunishwa na madhila tulofanyiwa na akasema hakukuwa na sababu yeyote ya kwamba kwanini tusiwe tumeshagawiwa ardhi hiyo,na pia hakukuwa na sababu hata ya Rais Mkapa kufuta hati kwa Mara ya pili.kutokana na uzito wake, aliahidi atakapopata nafasi nzuri atakuja mwenyewe kutukabidhi na kuwashuhulikia waliofanya mchezo huo muovu.lakini mpaka sasa bado hatujafanikiwa!
Mh, Raii,pamoja na hayo yote, tulishawashinda Hawa watesi wetu Mara kadhaa mahakamani,pale walipotushtaki kwa kuingia kwa sehemu katika shamba hilo. Kila Mara walishindwa kwa kupeleka nyaraka za kufoji.na hivyo Mahakama kutupilia mbali mashtaka na haki kubaki kwa wananchi.! Kwa huzuni bado hutapewa haki hiyo!
Mh Rais, kilio chetu kwako, useme neno tu, kwa Hawa wateule wako hapa wilayani, mh Jerry Muro na mkurugenzi wake ambao ndo wenye dhamana hiyo kisheria, ili tupate kupona!! Maana tunawindwa usiku na mchana sisi tuliojitoa mhanga kwa ajili ya wananchi wetu, wakiwemo yatima na wajane!
Nimalizie kwa kukushukuru, na kuomba radhi kwa kutumia njia hii.hakuweza kupata namna nzuri zaidi ya kukufikia.:tunaamini hata wasaidizi wako wakiona watakuletea mezani kwa uone maajabu yanayotendewa watu wako huku chini)
Mungu akubariki Sana!!
Ni Mimi Mchungaji Eliudi Kaaya
(0756579200)
Mwenyekiti kamati ya mgogoro huo!
kjh