VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Uliona mbali sana kukataza mikutano ya kisiasa ya hadhara.Najua uliwalenga hasa wapinzani katika katazo lako hilo. Ukafanikiwa.
Kwa makosa yanayofanywa na Serikali yako kuanzia katika Wizara hadi kule vijijini, wapinzani wangekuwa wanakukosoa na 'kukuumbua' sana. Uliona mbali kuwanyima 'forum',lakini si JF.
Katika kampeni za chaguzi ndogo ambazo zinarindima hivi sasa, angalau wapinzani wamepata upenyo wa kurusha maonyo na 'kuonesha mitonyo'. Akina Zitto wanarusha makombora bora.
Rais nakupongeza. Kwa 'blanda' za Serikali yako, kila uchao ingekuwa kujibu makombora ya wapinzani tu. Serikali yako isingejimwaga itakavyo kama sasa. Mikutano ni yenu tu kwasasa.
Mwafaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam