Rais Magufuli, ukitaka kwenda haraka, nenda Peke yako; ukitaka kwenda mbali, twende wote!

Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
17,104
26,070
Tanzania tunasafiri ndani ya basi moja lakini kila mtu ndani ya basi ana malengo tofauti!

Kuna ambao wanataka kwenda haraka haraka, kuna ambao wanataka kwenda mbali na kuna ambao hawajui!

Wanaotaka kwenda haraka,hawa hawajali gari linakwendaje, mashimo na kona kwao wanafumba macho bila kujua wanaacha maumivu kiasi gani!

Kundi hili kama wanatoka Dar kwenda Dodoma, basi wako radhi gari liharibikie Kibaha na waanze kutembea kwa mguu kumalizia sehemu kubwa ya safari iliyobaki! Hapa kwenye kundi hili namuweka JPM.

Baadhi ya wahanga wa gari kutokana na mwendokasi usioangalia hali ya barabara ni hawa:
*Wanasiasa hasa wa upinzani
*Wanafunzi UDOM-vlaza na kufukuzwa kama mbwa
*Wananchi waliobomolewa makazi
*Wahanga wa maafa kagera
*Waandishi wa habari-sheria mbovu ya habari
*Wafanyakazi-wengi hawajapanda madaraja hasa
*Wahitimu vyuo vikuu na ajira
*wananfunzi vyuo vikuu na vigezo vipya vya mikopo vilivyowaacha zaidi ya asilimia 60 bila mikopo!
*Watanzania kwa ujumla ambao Wamepata maumivu mbalimbali

Hayo makundi bila shaka yameachwa kwenye sintofahamu huku JPM akizidi kuchanja mbuga! Anaenda mbele huku ameliacha kundi kubwa limekata tamaa na hawajui kesho yao! Kiufupi wamejaa hofu na simanzi na katika gurudumu la maendeleo hawataweza kushiriki ipasavyo!

Rais JPM,if u want to go fast go alone, if u want to go far lets go together!
 
Tumuache Rais afanye kazi,mambo mengi anayofanya tuliwahi kuyalalamikia,leo tumesahau na wanajitokeza watu kumlaumu,tulipiga kelele kua nchi imekua na Miungu watu,nchi imejaa mafisadi,watumishi wanagawiana per diem hata kama hawajasafili,shirika la ndege wameliua,dharau za watumishi makazini.
Leo mkuu anahangaika na hayo kuyaweka sawa waTanzania wanarudi kutetea yale waliyoyalalamikia.ni kama hatujielewi elewi hivi.
 
Tanzania tunasafiri ndani ya basi moja lakini kila mtu ndani ya basi ana malengo tofauti!...

Rais JPM,if u want to go fast go alone, if u want to go far lets go together!

Bome-e: kichwa cha bandiko lako kilinishawishi kusoma yaliyomo, lakini umehitimisha tofauti na maudhui yake.

Mifano uliyoitoa ni ya watanzania (abiria kwenye bus) wanaopenda kufika haraka, tofauti na Rais na watanzania wengine wanaopenda kwenda kwa mwendo wa usalama.

Pamoja na miaka zaidi ya 50 ya uhuru, katika mwaka mmoja wa utawala wa Magufuli:
* Wanafunzi wa elimu ya juu wote wanataka mikopo ghafla.
* Wahitimu wanahitaji ajira papo kwa papo.
* Waajiriwa wanahitaji mishara minono.
* Wananchi wanatarajia kuondokana na umaskini ghafla.
* Wanasiasa na wanahabari wanataka uhuru usio na mipaka.
* na kadhalika

TUWE WAKWELI NA HALI HALISI YA NCHI KABLA YA UTAWALA HUU NA SASA
 
Back
Top Bottom