Rais Magufuli ukipenda kiondoe kikombe hiki

Rais Magufuli ukipenda kiondoe kikombe hiki

ukawa2020

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2016
Posts
339
Reaction score
1,315
Ni ukweli usiopingika kwamba Tarehe 1.9.2016 hakuna namna ya kuzuia mikutano na maandamano yasifanyike nchi nzima

Pia niukweli usiopingika kuwa police watatumia nguvu nyingi kudhibiti waandamanaji

Na ni ukweli usiopingika kuwa damu itamwakika na watu watapoteza maisha

Mh, rais huku mtaani hamasa ya watanzania kuandamana ni kubwa mno kiasi inafikia au imezidi kipindi umetangazwa kuwa mshindi wa urais, na hakuna namna ya kuwazui

Kwa nukta hii, nakuomba na kukusihi Mh rais ukipenda kikombe hiki ukiepuke kwa kukubali kukaa Meza moja na CHADEMA mmalize tofauti hizi na tulijenge taifa letu kwa kudumumisha amani ya nchi hii.
( ieleweke tu wazi amani ni tunda la haki)

Mimi naendelea kukusihi huku nikijenga UKUTA
 
Kukaa meza moja ni jambo zuri maana aya siyo mashindano kwamba anatafutwa mshindi. Kinga ni Bora siku zote kuliko tiba
 
Naona mnajaribu nguvu ya vyombo vya dola...subirini muone
 
Kwenye maandamano hayo watawaacha wake zao na watoto wao sehemu salama mchumia juani mwenzangu na mimi utawekwa kipaumbele huku umeshikishwa bango la ukuta .... Daaaaaaah hizi siasa maji taka zinageuka kibiriti cha kuchoma amani yetu.
 
Mmeamua kushika ukuta wenyewe suluhu ya nini, tulieni tu
 
Naona mnajaribu nguvu ya vyombo vya dola...subirini muone
Acha ujinga, hakuna chombo cha dola chenye nguvu kuliko wananchi. Ni jambo la kufuata tuu sheria na katiba basi! Asiye fuata achukuliwe hatua.
Kama wananchi wakienda kwenye mikutano ni kuvunja katiba basi polisi wawakamate na kuwafikisha kwenye haki. Lakini kama polisi nao kuwashambulia mikutanoni ni kuvunja sheria basi itabidi tulishawishi jeshi letu liingilie kati kama la Misri kuwalinda raia walioapa kuwalinda.
Ulinzi wa raia sio wa polisi pekee, na kama liliwexekana Misri hata huku lawezekana kwani hao jeshi ni watoto wetu. Kaka zetu , wajomba na jirani zetu na anayedhani hawana roho na aendelee kuamini hivyo
 
mtaa upi huo?? huku mtaani kwetu watu wapo bize na kazi
 
Kwenye maandamano hayo watawaacha wake zao na watoto wao sehemu salama mchumia juani mwenzangu na mimi utawekwa kipaumbele huku umeshikishwa bango la ukuta .... Daaaaaaah hizi siasa maji taka zinageuka kibiriti cha kuchoma amani yetu.

Kila raia ana haki ya kuchagua chama,kama watoto wake ni ccm utasemaje?
 
Acha ujinga, hakuna chombo cha dola chenye nguvu kuliko wananchi. Ni jambo la kufuata tuu sheria na katiba basi! Asiye fuata achukuliwe hatua.
Kama wananchi wakienda kwenye mikutano ni kuvunja katiba basi polisi wawakamate na kuwafikisha kwenye haki. Lakini kama polisi nao kuwashambulia mikutanoni ni kuvunja sheria basi itabidi tulishawishi jeshi letu liingilie kati kama la Misri kuwalinda raia walioapa kuwalinda.
Ulinzi wa raia sio wa polisi pekee, na kama liliwexekana Misri hata huku lawezekana kwani hao jeshi ni watoto wetu. Kaka zetu , wajomba na jirani zetu na anayedhani hawana roho na aendelee kuamini hivyo
Ina maana mnaanzisha tifu kwa kutegemea undugu na vyombo vya dola?

Unasahau vipi kwamba command in chief ni mmoja tu?

Polisi washatoa tamko ninyi mnajibishana nao mnatarajia nini...je huu mnaoandaa sio uhaini?
 
eti acheni wananchi wafanyekazi yeye kesho amewatangazia wananchi kuacha kufanyakazi na kwenda kumshangaaa huko sengerema
 
Kama rais anawapenda watu wake hawezi kuruhusu damu imwagike kwa sababu tu wananchi wanadai afuate katiba, la sivyo atakuwa ni rais wa aina yake
 
Naona mnajaribu nguvu ya vyombo vya dola...subirini muone

Hii nguvu ya dola ingeweza kutumika kuleta viwanda mbona ingekuwa bonge la sifa. Unajisifia una nguvu ya dola huku kuna mikataba ya kinyonyaji wageni wanakuja wanapiga hela huku unajisifu na nguvu ya dola ya kumuumiza mtanzania mwenzako!!! Kweli waafrika tumekosa akili.
 
Vipi kuhusu kutumia nguvu ya Ukuta katika ujenzi wa viwanda?
 
Kuna maana nyingi sana inayoelezea Democracy kama ifuatavyo;
1. Demcracy comes from two Greek words Demo which means People" and Cratos which means Power"
Simply Democracy can be defined as Peoples Power.
2.Demcracy may be defined as the system of the governnent and leadership in which the supreme power belongs to the people.
3. Abraham Lincolin's Defined Democracy is the power of the people,by the people for the people.
Yote kujaribu kutoa tafsiri mbalimbali na maana ya Demokrasia ni kwamba hakuna nguvu kubwa inayoweza shinda nguvu ya wananchi wakiamua.
 
Ina maana mnaanzisha tifu kwa kutegemea undugu na vyombo vya dola?

Unasahau vipi kwamba command in chief ni mmoja tu?

Polisi washatoa tamko ninyi mnajibishana nao mnatarajia nini...je huu mnaoandaa sio uhaini?
Hivi unadhani Mubarak hakuwa Commander in chief? Tena wa jeshi kubwa Afrika lakini sasa hivi alikuwa anawekwa kwenye cage kama nyani kwa nini? Hakuheshimu katiba na sheria na kujiona kamanda mkuu. Hayo hayo Gaddafi,Amin na wengine.
Mikutano haizuiwi kwa kauli bali sheria na katiba tuu, acheni jamani kumpa kichwa mtu na kumponza kisa kujiona kidume hakuna wa kumchezea. Ukiingia ofisi kuu kwa hiari ya watu tena kwa kuwabembeleza wakukubali ni tofauti na kina Kagame au Museveni ambao walilala kwenye mahandaki na kula mpaka nyama ya fisi porini kutafuta vyeo hivyo.
 
Chaneli gani itarusha hayo maandamano, mie ninunue popukoni siku hiyo nijilie kwa kuangalia kinachojiri?
 
Vipi kuhusu kutumia nguvu ya Ukuta katika ujenzi wa viwanda?
Waliwaongopea wananchi watawajengea viwanda? Wao wanataka katiba ifuatwe. Hao waliowaahidi wananchi viwanda mbona viwanda hamna na bado katiba inawashinda kuitii?
 
Back
Top Bottom