Rais Magufuli: Tutanunua Korosho kwa Tsh.3,300/=, JWTZ ihakikishe kila ghala linalindwa na Wakulima wanalipwa haraka bila usumbufu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Leo Rais Magufuli anawaapisha mawaziri wapya walioteuliwa baada ya kufanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri.

Miongoni mwa watakaoapishwa leo ni Mbunge wa Ukonga, Mwita Mwikwabe Waitara baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI. Waitara alikuwa Mbunge wa Ukonga kupitia CHADEMA, akajivua uanachama na kujiunga CCM, akashinda tena.

Miongoni mwa waliohudhuria Uapisho huo ni aliyekuwa Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage ambao nafasi zao zimechukuliwa na Japhet Hasunga pamoja na Joseph Kakunda

My take:
Kama kawaida yake Rais Leo hatachomekea bali ataingia jumla kabisa wapinzani jiandaeni kumkabili na kumkosoa sio kwenye hoja Bali kwenye maneno yake atakayotumia kwenye hotuba ..atazungumzia ishu nzima ya ushoga na kueleza msimamo wa nchi yetu juu ya hili suala.pia atagusia kwa kina ishu nzima ya korosho.


=========================

JAJI MKUU: Nguvu za Serikali zinatokana na Sheria. Mahakama itatoa ushirikiano kwa viongozi wapya(walioteuliwa) > Ingawa haya yanasemwa kuwa mabadiliko madogo lakini ni makubwa kutokana na unyeti wa wizara zilizofanyiwa mabadiliko

JAJI MKUU: Lazima tujipange kwa kuwa na mikakati ya kufanya kazi kiushindani kwa kila sekta na kila wizara Tupitie hata ripoti za Benki ya Dunia zitatusaidia kujua namna gani tujipange kiushindani

SPIKA NDUGAI: Rais anapofanya kazi za kuteua ni kazi ngumu sana hata kutengua watu si jambo rahisi na huwa halifanywi ghafla linachukua muda. Rais nimekuwa naye Bungeni kwa miaka 15, alikuwa na furaha, mcheshi, utani. Tangu Watanzania tumemtwika mzigo sioni akicheka

SPIKA NDUGAI: Wizara ya Kilimo kama tunavyosema Kilimo ni Uti wa Mgongo ni Wizara ambayo tangu uhuru Serikali imewekeza sana hata tukawa na chuo Kikuu cha Kilimo. Wizara ya Kilimo ina wasomi wengi. Kama nchi tumesomesha sana lakini ndio Wizara pasua kichwa

WAZIRI MKUU: Nawapongeza wateule wapya na uteuzi wenu umezingatia vigezo vyote na Rais anatambua uwezo wenu na anatarajia mtatumia uwezo wenu katika Wizara mlizopewa. Wizara hizi 2 (Kilimo &Viwanda) ni muhimu na Rais amekuwa akitaka kuona mafanikio kwenye sekta hizi

WAZIRI MKUU: Tutafanya kazi kwa kushirikiana na hata kwa Mawaziri ambao kwenye Wizara zenu na maelezo ya msingi mtapewa na Makatibu Wakuu wa Wizara zenu. Mchango wa Vyuo vya Kilimo bado hauna tija nchini, hii ni changamoto na kuna haja ya kufanya mabadiliko

WAZIRI MKUU: Mafanikio katika zao la Pamba kwa mwaka jana ni kutokana na maagizo yako Rais. Hatua ulizozichukua kuhusu zao la Korosho ni sahihi. Niliwapa siku 4 wanunuzi wenye nia ya kununua Korosho wafanye hivyo. Mpaka asubuhi hii Makampuni 15 yamejitokeza

WAZIRI MKUU: Kwa jitihada na Ubalozi wa China kuna Kampuni imeleta maombi ya kununua Tani laki 2 na mengine yamejitokeza kwa kutaka kununua Korosho kwa viwango mbalimbali. Kujitokeza kwa Makampuni haya ni jitihada za Mabalozi wa nchi mbalimbali na taasisi za Uwekezaji

RAIS MAGUFULI: Kwa namna ya pekee niwapongeze waliokuwa Mawaziri wa Wizara ya Kilimo na Viwanda kwa kufika kwenu. Kuna gazeti linanikumbusha kuwa Mawaziri 20 nilioanza nao wamebaki 11 na 9 nimewatengua. Nimejiuliza miaka 2 iliyobaki wangapi watakuwepo?

RAIS MAGUFULI: Katika kazi hizi za kuleta maendeleo na kufikia malengo sio lazima wote mfike. Kuna mambo ambayo tulijiwekea malengo ya kuyafikia ikiwemo sekta ya Kilimo na Viwanda. Wizara hizi zinauwezo wa kutatua changamoto ya ajira

RAIS MAGUFULI: Sekta ya Kilimo na Viwanda ni sekta nyeti na mara nyingi nimekuwa nikigombana na Waziri Mkuu nikimuuliza mbona hiki hakiendi? Mara nyingine nampigia simu saa 8 usiku nikimtuma huku na huku kwasababu ndio kiranja wa Mawaziri

RAIS MAGUFULI: Nimekuwa nikiona Wizara zinazofanya kazi vizuri. Ukienda TAMISEMI kuna vijana wanafanya vizuri, Seleman Jaffo. Nimetoa mfano wa huyu kwasababu ndio kijana mdogo na nimesikia ana wake wanne

RAIS MAGUFULI: Limetokea suala la Kahawa nilimtuma Waziri Mkuu akaenda kulishughulikia. Tena wengine wanaovuka mpaka kwenda kuuza Kahawa wanatokea kwa Waziri Mwijage nikajiuliza au ameegemea kwenye Viwanda amesahau Biashara?

RAIS MAGUFULI: Kuna kiwanda kilikuwa kimekaa bila ya uzalishaji nikamtuma Waziri Mkuu akaenda kutatua Mpaka nikamwambia sasa nitakufanya uwe Waziri wa Viwanda au Kilimo

RAIS MAGUFULI: Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazozalisha Korosho kwa wingi Duniani. Tumebahatika kupata Bunge kama chombo cha kutunga sheria, taasisi na Bodi mbalimbali lakini linapokuja suala la mazao ya Watanzania siwaoni wakifanya juhudi

RAIS MAGUFULI: Mkurugenzi wa TANTRADE hajui kama anatakiwa kutafuta masoko ya mazao yetu au yeye anasubiri tarehe 1 mwezi wa 7 ili afungue maonesho ya saba saba. Mkurugenzi wa TANTRADE anasubiri kupokea viingilio vya maonesho ya saba saba

RAIS MAGUFULI: Kulikuwa na kikao kilichoitishwa na Waziri Mkuu na Mimi nikaona nivamie na Waziri Mkuu hakunifukuza nikafurahi. Niliyoyasikia humo yaliniumiza, Mwakilishi wa Bodi ya Korosho nilimuuliza bei ya Korosho akasema Tsh. 1,000 na Bei elekezi waliyoitoa ni 1,500

RAIS MAGUFULI: Niliangalia mataifa mengine nikaona bei ya Korosho imeshuka kidogo India. Nikaona Bodi ya Korosho haipo kwaajili ya manufaa ya Watanzania. Nikawapa bei elekezi ya Tsh. 3000 lakini siku ya mnada waliongeza shilingi 1 aliyeongeza zaidi alinunua kwa 3016

RAIS MAGUFULI: Nikagundua huu ni mchezo uliopangwa ili mvua ikianza wakainunue Korosho kwa bei ya chini kwasababu Wakulima wataogopa kuharibikiwa. Lakini kwenye hili sikuona statement ya Waziri wa Kilimo wala Viwanda

RAIS MAGUFULI: Nimeamua yafuatayo. Walioleta mapendekezo kwako achana nao watakuja kuleta masharti. Wanaoendelea kuja wala wasihangaike nimeshafunga. Korosho tunanunua wenyewe.

RAIS MAGUFULI: Nimepiga mahesabu ingawa Mimi si mchumi, ukibangua Korosho Kg 3 unapata Kg 1 ukichukua Tani laki 2 utapata Kg elfu 73 na ukigawa kwa Watanzania kila Mtu anapata Kg 2 na Korosho zitakuwa zimeisha

RAIS MAGUFULI: Ile Korosho tutainunua kwa Tsh. 3300 na kila Mkulima alipwe bila ya kukatwa hela yoyote. Maghala yote yalindwe na JWTZ na wameshakaa tayari kusimamia zoezi hili ili Korosho mbaya kutoka nchi jirani huwa inaletwa

RAIS MAGUFULI: Korosho nyingine itapelekwa kwenye Kiwanda kilichopo Lindi kilichorudishwa kwa Serikali juzi kinauwezo wa kubangua tani 73 elfu. Na kuanzia leo Kiwanda hiki nimelipa Jeshi na wao wakishindwa kikiendesha nitawapa wengine. Jeshi liende likakizingire

RAIS MAGUFULI: Korosho yetu ni daraja la kwanza duniani lakini Wananchi wanaishi maisha ya chini na mabodi yapo tu. Tunabaki kuwasikiliza matapeli wanaozungumza kwenye vyombo mbalimbali kwa faida zao na wanaowatuma

RAIS MAGUFULI: Niliowateuwa mkaanze kufanya kazi leo. Tatizo hamfanyi kazi kwa kushirikiana nendeni mkaanzishe ushirikiano. Benki ya Wakulima watatoa fedha na Jeshi litaichukua Korosho na hakuna itakayoibiwa Mimi nawajua. Jeshi likabangue kwa namna watayoona inafaa

RAIS MAGUFULI: Taasisi ya Uwekezaji ihamie kwa Waziri Mkuu na itakapokuwa chini ya Waziri Mkuu hata Mimi nitakuwa na uwezo wa kusimamia. Kuna wawekezaji wa ajabu wamekuja nchi hii. Mtu anakwambia anawekeza Bagamoyo lakini anakwambia usiwekeza hadi Pangani

RAIS MAGUFULI: Tusifikirie wawekezaji wanakuja kutusaidia. Kuna mambo ya ajabu kabisa tena mkataba unawapa kwa miaka 99. Tumekuwa na Bodi zisizofanya kazi.

RAIS MAGUFULI: Sitajali kubadilisha Mawaziri kila wakati hata kama watakuwa wanabadilishana kila baada ya miezi 5. Zao la Korosho limeingiliwa sana hata Wanasiasa walikuwa wanaweka watu wao na kufanya biashara ya 'Kagomba'. Na ndio wasemaji wakubwa wa watu wa huko

RAIS MAGUFULI: Nawapenda wote lakini kwenye ukweli lazima tuambiane. Benki Kuu mwende mkalisimamie hili kuna watu wanataka kuleta fedha za utakatishaji kwenye benki zetu. Wengine walitaka kuingiza Bilioni 150 kupitia benki flani kwahiyo Gavana endelea kubana hivyo hivyo

RAIS MAGUFULI: Unisamehe Jaffo nimekusifu hadharani na Utumishi nimeona nimuongezee Mzee wetu Mkuchika kwasababu alibaki peke yake hata Mtu wa kumtuma alikuwa anakosa. Jaji Mkuu nitakuletea majina ya Majaji wanaochukua rushwa

RAIS MAGUFULI: Jaji Msofe tumekuteua kwasababu umestaafu kwa rekodi nzuri. Pia Jaji Mkuu ninakushukuru kwa ushauri wako na nitakuletea majina ya wanaofanya vibaya. Mawaziri mlioteuliwa msidhani mtapendwa na baadhi ya Wabunge

RAIS MAGUFULI: Baada ya kutangaza mabadiliko Dkt. Tizeba alinipigia simu, nikajiuliza nipokee au nisipokee maana nisije nikaonge kitu watu wakazimia. Lakini alikuwa akinishukuru kwa kuhudumu kipindi chote bila ya kuishia jela

RAIS MAGUFULI: JWTZ nendeni mkafanye kazi hakuna mlilowahi kushindwa. Ukuta wa Mirelani mlijenga miezi 3 badala ya 6. Hii oparesheni ya Korosho haiwezi kuwashinda. Pangeni vikosi vya kubangua Korosho, tukikosa wanunuzi tutazila maana ni kilo 2 tu kwa kila Mtanzania

RAIS MAGUFULI: Wakulima wa Zabibu wanalalamika na Wizara ya Fedha, Viwanda na Kilimo zipo kwanini wanashindwa kutatua. Sio kila kitu mpaka Mimi niseme. Sasa hili la Zabibu mwende mkalimalize sio mpaka niseme mkalimalize

RAIS MAGUFULI: Hao wanaosema tunatumbua ni wachonganishi. Waziri Mkuu nenda ukasimamie hili bei ya Korosho ni Tsh. 3300 hata tukipata hasara potelea mbali. Kokoa kule Kyela mkaifuatilie kwasababu Wananchi wananiandikia 'vimeseji'

RAIS MAGUFULI: Makatibu Wakuu wa Wizara nilizozifanyia mabadiliko msifikirie nimewasahau au kwamba ninyi ndio mmetulia sana. Kuna mambo yanakwama kwasababu ya Makatibu Wakuu. Mwende Mkabadilike
 
Kama kawaida yake mh. Rais Leo hatachomekea Bali ataingia jumla kabisa wapinzani jiandaeni kumkabili na kumkosoa sio kwenye hoja Bali kwenye maneno yake atakayotumia kwenye hotuba ..atazungumzia ishu nzima ya ushoga na kueleza msimamo wa nchi yetu juu ya hili suala.pia atagusia kwa kina ishu nzima ya korosho.

Tutasikia pia Makosa ya Kidata mpeni tu MIC
 
Kama kawaida yake mh. Rais Leo hatachomekea Bali ataingia jumla kabisa wapinzani jiandaeni kumkabili na kumkosoa sio kwenye hoja Bali kwenye maneno yake atakayotumia kwenye hotuba ..atazungumzia ishu nzima ya ushoga na kueleza msimamo wa nchi yetu juu ya hili suala.pia atagusia kwa kina ishu nzima ya korosho.
Siungi mkono suala la ushoga... ila kuna namna nyingi za ku deal na adui yako, na ukizingatia kwamba adui amekuzidi uwezo... Ubabe si njia nzuri...
 
Back
Top Bottom