Rais Magufuli: Tutagawa bure Sukari itakayokuwa imefichwa

si
Hiyo sukari itafika lini? Hiyo iliyofichwa itagawiwa kwa kufuata taratibu zipi? Anawashughulikiaje TFDA na TBS? Sukari iliyofichwa ya Tanzania au ya nje? (Tukumbuke kuna waliokuwa na stock lilipotoka katazo)
sizani kama raisi amesema wanaingiza expired sugar ila amesema inayokaribia ku expire...so hapo tfda sio rahisi kubaini mchezo huo...tunapaswa kusikiliza konachosemwa kuliko kuongea yakwetu tu...ila pia lazma rais akubali alikosea kuzuia kuingizwa sukari coz ninavyoona viwanda vya ndani hajitoshelezi kabisa hvyo soln ni defensive mechanism kwamba sukari ilyokuwa inaingizwa ilikuwa inakaribia ku expire....
 
Nchi haiendeshwi kwa mipasho na kukurupuka, watu wanateseka we unaleta mipasho!!!
Kwa hisani ya KikulachoChako napaste

Unajua mkuu mimi muda nawashangaa wanasiasa hasa wa vyama vya upinzani.....daima wao wanajitanabaisha kuwa wanawatettea wanyonge na kuwapigania.....yanapofanywa maamuzi ya kuwatetea wanyonge hao hao tena wanapinga....yaani ni kama wamerukwa na akili hawajui wanataka nini.....
 
Uhaba wa sukari ni wakutengenezwa na wafanyabiashara wakubwa,waiweke sokoni yote tujue kama uhaba utakuwepo.Namuunga mkono JPM akikamata agawe bure kwa utaratibu maalum
kwanini serelikari sasa imeagiza inje wakati sukari ipo imefichwa na uwezo wa kuchukua upo,think big.
 
Mkuu me kuna kitu nashindwa kuelewa, watu wanasema kuzuia sukari kutoka nje ni kwa sababu ya kukuza viwanda vya nyumbani, lakini ukichunguza hivi viwanda vingi vimebinafsishwa kwa wageni so indirectly hizi subsidiaries zinapeleka profits kwao.

Kingine nachoshindwa kuelewa ni kuna mahusiano gani kati ya kuhifadhi sukari na kuhujumu uchumi, nikifikiria kwa haraka haraka tu naona Mo na Bakhressa wana viwanda vingi vinavyoproduce products zinazotumia sukari, so kama na wao wamepredict scarcity it makes sense kuhifadhi iyo raw material so as not to hinder production considering importation is prohibited.

Natumai Mr President alikaa chini na kuconsult stakeholders wote wanaohusika kwenye supply chain ya sukari na majority wakaridhia na maamuzi ya kuzuia kuagiza sukari after raising their concerns, if such procedures were not followed I guess somebody is playing the blame game.
hujanielewa...sijakataa kutumia sukari ya ndani...Ila Unapoanza kuzuia hakikisha umeweka plan ya ku cover hilo gap ili kuepuka kuumiza wananchi wako

Sasa wewe unakurupuka bila hata kupata facts alafu unawatesa wananchi bila sababu...**** mikoa hapa nchini sukari kwa sasa ni shs 4000
 
kwanini serelikari sasa imeagiza inje wakati sukari ipo imefichwa na uwezo wa kuchukua upo,think big.

Ndio maana nimesema zoezi la kutafuta sukari iliyofichwa litachukua muda na nchi haina sukari sokoni kwahiyo lazima serikali ijue kwa uhakika sukari inayotakiwa ni ya kiasi gani kila mwezi,then waagize kwa uhakika
 
mmmh !!! ataleta sukari toka wapi?? si alikataza yeye mwenyewe tena kwa mbwembwee na sauti kali, ajifunze kuacha kukurupuka kisha kuwabenesha mzigo wengine.
sasa mnamhujumu ili mseme kakurupuka ,,,kaazi kweli kweli
 
Is that the law? Lisu alisema jana kuwa kuna ka-element ka udikteita !! msio fikiri mkambeza. That is dictatorship, wapeleke mahakamani kama wanaficha sukari haki itendeke!

Mahakama jamaa watapeta wanatoa hela tu anashinda mapema sana. Dawa ni ky deal nao ivo tu.
 


Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya walioficha Sukari na kutishia Kuichukua Sukari hiyo na Kuigawa Bure Kwa Wananchi. Rais Magufuli ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara walioficha sukari ili baadae waiuze kwa bei ya juu.

Amesema wafanyabiashara hao wenye tamaa ya pesa walikuwa wakifuata sukari iliyo Expire huko Brazili na kuileta nchini ili watengeneze faida na ndo maana serikali iliwapiga marufuku kuagiza.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akiwasalimia wananchi wa Katesh, Mkoani Manyara. Rais ametoka Mkoani Dodoma leo, anaelekea Mkoani Arusha kwa usafiri wa gari.

Akiongea na mamia ya wananchi hao waliojitokeza kumlaki njiani, Rais Magufuli amewatoa hofu wananchi kuhusu uhaba wa sukari kwa kuwa tayari wako katika mchakato wa kuagiza makontena ya sukari nje ya nchi ili kuwakabili wafanyabiashara walioficha bidhaa hiyo.

Amesema kwa taarifa alizonazo, kuna mfanyabiashara alienda akanunua sukari pale Kilombero zaidi ya tani 3000 na hataki kuzichukua hadi leo

Pia amesema kuna mwingine ana godauni huko Mbagala yenye tani 4000 ambazo hataki kuzitoa ili wananchi wakose sukari.

Rais Magufuli amesema ameviagiza vyombo vya dola viwafuatilie ili ikithibitika sukari waliificha basi ichukuliwe na kugawiwa bure kwa wananchi na pia watapigwa marufuku kufanya biashara yoyote hapa nchini.

Tanzania hakuna wafanyabiashara wengi wanaojiita wafanyabiashara ni madalali na madhurumati wakubwa.Sema watu wengi washadhurumiwa ila wanaogopa kusema kwa kuogopa tindikali.A true Businessman honors business ethics and has all relevant documents and practical history of his Business.Sasa kama huamini wewe wakamate hao wanaojiita wafanyabiashara wakuelezee historia za utajiri wao,utachoka.Wengi wapigaji wa mjini tu.
 
mmmh !!! ataleta sukari toka wapi?? si alikataza yeye mwenyewe tena kwa mbwembwee na sauti kali, ajifunze kuacha kukurupuka kisha kuwabenesha mzigo wengine.
Hata hujui unachokisema,rais alisema kibali cha kuleta sukari toka nje kitatolewa na rais au makamu pale itakapoonekana inafaa kufanya hivyo,na ndo anavyofanya hivi sasa.
 
Jamaa mnafiki sana huyu miezi minne sasa tangu apige marufuku uingizaji wa sukari nchini na hakuwahi hata siku moja kusema sukari ile ilikuwa imeexpire. Leo kakurupuka kama kawaida yake kutaka kuudanganya umma wa Watanzania na kama walivyo baadhi ya Wadanganyika wataamini uongo huu ili kujustfy uamuzi wake wa kukurupuka. Wadanganyika ndivyo walivyo!

hahahahahah...Eti sukari iliyo isha muda inatumika....TFDA wanafanya kazi gani?
 
Jamani jamani hii nchi ni muhimu kuliko hizi comedy

Acheni kudanganya wananchi

Viwanda vya ndani havina uwezo kuzalisha kukidhi soko ndio maana kuna shortage

Na ndio maana mmeona bora muagize sukari kutoka nje....na hii ilikuwa baada ya kuurupuka na kuzuia importation ya sukari

Acheni kutumia ujinga wa wananchi kuwaaminisha vitu visivyokuwepo

Waoneeni huruma wananchi

Acheni kuwafanyia propaganda

Please stop this before its too late

Ndugu yangu kuwa mtazamaji tu.. Hapo umeongea point lakini usishangae ukatukanwa na kubezwa.... Nchi hii kama unajiweza fanya mambo yako acha wafu wazikane... Hakuna namna. We sukari imefika 3200 kg!!! Leo nimemshuudia mtu akimfuata mmbeba mizigo alie beba sukari akimuomba ampeleke kwa mwenye hiyo sukari amuuzie!!!!
 
thubutu agawe sukari ya wafichaji bureee: WALIOFICHA SUKARI WATATETEWA NA WAKILI "MSOMI" TUNDU LISU
Kwa hiyo Lissu yuko pamoja na wanawatakia maisha magumu watanzania! OK ndio maana anabwabwaja sana wakiguswa mafisadi.
 
Mbona haya hayakuwepo ua kuficha kabla yake ? Mtu utaficha sukari kwa nini ? Sababu zipi ufiche ?
Hapa kuna uhaba mkubwa , jana baadhi ya supermarket wana limit idadi ya kununua ...kwa sababu hawana ya kutosha sasa mtu afiche ya nini ?
Nadhani kuna watu wanaingiza kusaidia uhaba labda kutoka malawi nk..sasa huko sio kuficha bali
Hebu jaribu kusoma uchumi kuhusu "Theory of the firm" particularly "Demand and Supply" V/s "The Price".....! Utaona ni kwa nini mfanyabiashara akiamua kupandisha bei ya vitu ili kutengeneza faida kubwa kwa muda mfupi hucheza pia na supply....! Ndio hapo utajua kwanini wanaficha....!
 
wakubali tu kwe hili la sukari nchi haikuiandaa sema tu mizuka na siasa zilitumika,asa hao watu wawili waliojulikana wameficha sukar ndo wameleta uhaba nchi nzima? mbona serikali imekua haieleweki?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom