Rais Magufuli: Tutagawa bure Sukari itakayokuwa imefichwa

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253


Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya walioficha Sukari na kutishia Kuichukua Sukari hiyo na Kuigawa Bure Kwa Wananchi. Rais Magufuli ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara walioficha sukari ili baadae waiuze kwa bei ya juu.

Amesema wafanyabiashara hao wenye tamaa ya pesa walikuwa wakifuata sukari iliyo Expire huko Brazili na kuileta nchini ili watengeneze faida na ndo maana serikali iliwapiga marufuku kuagiza.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akiwasalimia wananchi wa Katesh, Mkoani Manyara. Rais ametoka Mkoani Dodoma leo, anaelekea Mkoani Arusha kwa usafiri wa gari.

Akiongea na mamia ya wananchi hao waliojitokeza kumlaki njiani, Rais Magufuli amewatoa hofu wananchi kuhusu uhaba wa sukari kwa kuwa tayari wako katika mchakato wa kuagiza makontena ya sukari nje ya nchi ili kuwakabili wafanyabiashara walioficha bidhaa hiyo.

Amesema kwa taarifa alizonazo, kuna mfanyabiashara alienda akanunua sukari pale Kilombero zaidi ya tani 3000 na hataki kuzichukua hadi leo

Pia amesema kuna mwingine ana godauni huko Mbagala yenye tani 4000 ambazo hataki kuzitoa ili wananchi wakose sukari.

Rais Magufuli amesema ameviagiza vyombo vya dola viwafuatilie ili ikithibitika sukari waliificha basi ichukuliwe na kugawiwa bure kwa wananchi na pia watapigwa marufuku kufanya biashara yoyote hapa nchini.
 


Awatahadharisha wafanyabiashara wanaoficha sukari,

Asema wanaingiza nchini sukari iliyomaliza muda wa matumizi (expire)

Atadhibiti tatizo la sukari.

Ataleta sukari ya kutosha kwa kushirikiana na Waziri mkuu.

Asema atachukua sukari iliyofichwa na kugawa bure! Awaita wanaoficha sukari, wahujumu uchumi!

Is that the law? Lisu alisema jana kuwa kuna ka-element ka udikteita !! msio fikiri mkambeza. That is dictatorship, wapeleke mahakamani kama wanaficha sukari haki itendeke!
 
Jamani jamani hii nchi ni muhimu kuliko hizi comedy

Acheni kudanganya wananchi

Viwanda vya ndani havina uwezo kuzalisha kukidhi soko ndio maana kuna shortage

Na ndio maana mmeona bora muagize sukari kutoka nje....na hii ilikuwa baada ya kuurupuka na kuzuia importation ya sukari

Acheni kutumia ujinga wa wananchi kuwaaminisha vitu visivyokuwepo

Waoneeni huruma wananchi

Acheni kuwafanyia propaganda

Please stop this before its too late
 
Kumekucha Sokoine huyo kafufuka kupambana na wahujumu uchumi.Muda si mrefu tutaona watu wakitupa magunia ya sukari waliyoficha majumbani kwa kuogopa kutumbuliwa.

Kanyaga moto gari magufuli ongeza mwendo tuko pamoja.Wahujumu uchumi wajiandae kukiona cha mtema kuni

Mbona haya hayakuwepo ua kuficha kabla yake ? Mtu utaficha sukari kwa nini ? Sababu zipi ufiche ?
Hapa kuna uhaba mkubwa , jana baadhi ya supermarket wana limit idadi ya kununua ...kwa sababu hawana ya kutosha sasa mtu afiche ya nini ?
Nadhani kuna watu wanaingiza kusaidia uhaba labda kutoka malawi nk..sasa huko sio kuficha bali
 
Back
Top Bottom