Rais Magufuli tupia macho chama cha walimu.

mugua

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
205
120
Mheshimiwa Rais kwanza pole kwa majukumu.Mpaka sasa umesafisha nyumba kiasi cha kutosha.

Walimu tunakuomba utupie macho chama hiki,chama kina vitega uchumi,hakuna sababu ya wanachama kuendelea kukatwa 2% toka kwenye mishahara yao.

Kila mwanachama ana hadhi sawa na mwenzake,kwanini tuchangie kwa viwango tofauti vinavyosababishwa na kutofautiana mishahara?

Walimu wanachama hatusikilizwi na viongozi wa chama hasa kwenye hoja ya kupunguza makato.

Viongozi hawakubali mtu kujiondoa uanachama,kwa nini?

Mh,Rais wakati huu unapofikiria kuboresha maslahi ya wafanyakazi ,fikiria pia kupunguza makato yanayofanywa na vyama vya wafanyakazi hususani walimu.

Tunakuomba uingilie ili haya yafanyike,

1,Wanachama tuchangie sh,elf kumi mara moja kwa mwaka.

2.Kuwe na uhuru wa kujiunga na kujitoa.

3.Kukatwa kwa % kukomeshwe.

Tunawasilisha.
 
Back
Top Bottom