Rais Magufuli tuokoe, tunakufa njaa Ujerumani

Serena

Senior Member
Apr 4, 2014
124
125
Mh. Rais wangu Mpendwa Dr. Magufuli,
Pole na majukumu ya kujenga nchi yetu kutokana na changamoto za kujenga nchi yetu. Pamoja na hayo nataka kuchukua fursa hii baada ya uvumilivu wa mda mrefu kukuelezea masikitiko yetu na jinsi tunavyoteseka sisi wananchi wa Tanzania tunaosoma na kuishi hapa Ujerumani. Unaweza ukajiuliza ni kwanini hii barua ya wazi iandikwe kwako na si kwa watendaji walioko chini yako kama waziri wa elimu, katibu mkuu wa wizara, wakurugenzi au makamishina wa elimu. Jibu ni kwamba; HUKO KOTE TUMESHAFIKISHA MALALAMIKO YETU LAKINI HATUKUPATA UFUMBUZI WOWOTE. Lakini pia unaweza ukajiuliza ni kwanini iwe kwa njia ya Jamii Forums? Jibu ni kwamba kama barua, mails, na hata kiongozi wetu kufuatilia malipo yetu toka TCU, HESLB na Wizarani hizo njia hazijazaa matunda na si ajabu ofisi yako haina taarifa hii. Na kwa msingi huo, mimi nikiwa mmoja wa waathirika na ambaye kwa kiasi kikubwa sana nimefanya jitihada za kila namna ikiwemo kuwasiliana na watendaji wakuu wa TCU, HESLB (Mkurugenzi Mtendaji Mr. , na Mkurugenzi wa Fedha Mr....), na wizara ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu, lkn katika njia zote hizo HAKUNA MAFANIKIO NA SASA NI MIEZI MINNE baadhi yetu tunakaa nje ya nchi bila kupata pesa za kujikimu toka Tanzania kupitia HESLB na TCU.

Mh. Rais wangu, sisi waathirika ni wanafunzi tunaosoma huku Ujerumani kupitia mpango maalumu kati ya serikali yetu pendwa na serikali ya Ujerumani kupitia program ya MoEVT - DAAD (ukitaka kujua zaidi kuhusu hii program muulize yule katibu mkuu uliyemuhamisha majuzi kwenda wizara ya sheria kwani anajua kila kitu kuhusu hii programu. Lakini pia waweza kumuuliza yule kamishna wa elimu ambaye ni Prof...., yupo pia mkurugenzi mkuu wa HESLB, na Mkurugenzi wa Fedha wa HESLB. Hao watakuambia A-Z ya program hii kwasababu ni kama miaka 2 sasa toka waliposafiri na timu yao kuja Ujerumani kwa kodi zetu kwa kile walichokiita kuja kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo yetu hasa namna ya kuweza kuwalipa wanafunzi hawa stipend allowances zao kama mkataba unavyoonyesha. Hatahivyo, hatujaona matunda ya safari yao, kwani mpaka sasa matatizo ndiyo yamezidi. Nasema yamezidi kwani kabla ya kuja kwao angalao waliotutangulia walikuwa wakilipwa japo katika kipindi cha mwezi hivi. Hii ni tofauti na sasa ambapo kuna baadhi yetu hawajalipwa Stipend allowances zao za mwezi Oktoba, Novemba, na Desemba 2015. Pamoja nao, wale wote wenye familia huku ujermani wana miezi 3 (Oktoba-Desemba 2015) bila kulipwa pesa hizo.

AJABU LA MWAKA:
Mh. Rais, katika suala hili kumekuwa na mambo ya ajabu sana hasa kutoka kwa watendaji wa HESLB (Mkurugenzi wa Fedha). Huyu bwana amekuwa akitudanganya sana toka mwezi Oktoba 2015 kuhusu malipo yetu. Imefikia hatua wanaandaa majina yetu pale ofisini kwao na kiasi tunachopaswa kulipwa na kuonyesha kwamba tayari pesa zimepelekwa Benki. Sisi waathirika tunakaa kama wiki nzima bila kuona pesa kwenye akaunti zetu, na kiongozi wetu huku Ujerumani akifuatilia anaambiwa kuna kosa lilitendeka, hivyo, malipo yatanyika muda sio mrefu. HESLB chini ya Mkurugenzi Mtendaji na Mkurugenzi wa Fedha wametudanganya sasa zaidi ya mara 3 sasa kwamba pesa zimeshatumwa wakati ni UONGO. Hii hali imetusababishia usumbufu mkubwa sana katika mambo yetu ya kielimu na hata kijamii. Hata leo kiongozi wetu huku ujerumani alikwenda wizara ya Elimu baada ya kudanganywa tena na HESLB kwamba tungelipwa pesa zetu wiki iliyopita. Huko kote hakuna mafanikio, kwani bado ameambiwa tuandike tena barua japo suala letu linajulikana sana pale wizarani, TCU na HESLB.

Mh., Rais,
Hakika tunaumia sana na kwa hakika hatujui nini cha kufanya sasa, kwani shule na njaa na usumbufu wa kodi za pango ni mkubwa sana kwetu. Charges nazo zimekuwa nyingi sana na mbaya zaidi sasa tumekuwa ombaomba hadi wametuchoka. Kuna hoja hapa labda kuhusu sisi kutafuta kibarua huku ili tuweze kujikimu, hilo kwanza lina implications katika kusoma kwetu lakini pia mkataba wetu unatuzuia kufanya kazi. Kwa program hii ni kwamba Wizara ya Elimu kupitia TCU na HESLB inatakiwa kutulipa 80% ya Stipend allowances zetu na DAAD ya Ujerumani inalipa 20% pekee. Kwa 20% ya DAAD haitoshi hata gharama ya Chumba achilia gharama ya kula na hata registration fees.

Mh. Rais, kwa namna ya kipekee sana tunaomba utusaidie, kwani tuna hali mbaya sana. Hatujapata Stipend allowances ya Miezi 3 (Oktoba-Desemba 2015) pamoja na Family allowances ya miezi hiyo.

Natanguliza shukrani na tunaangalia mbele kwa matumaini ya suala letu kupata ufumbuzi mapema.

Ahsante sana na nikutakie kila la kheri katika ujenzi wa Taifa letu pendwa la Tanzania.

Ndimi, muhathirika wa HESLB/TCU/Wizara ya Elimu.

Üpdates:
Naomba kwa namna ya kipekee sana nichukue fursa hii kumpongeza Mh. Rais Magufuli kwa kusikiliza kilio chetu, kwani hatimaye tumelipwa pesa/madai yetu. Ahsante sana Mh. Rais wetu mpendwa. Ahadi yetu kwako ni kuwa wazalendo na watiifu kwa serikali yetu na kwa maslahi ya Taifa letu kwa ujumla.

Na kwa wale wote walionibeza, naomba niwashukuu pia, kwani mnajifanya waelewa lakini bado mnalo la kujifunza katika namna ya kufikisha taarifa katika jamii,na hasa pale inapotokeaa kwamba options zingine zimeshatumika bila mafanikio. Ahsanteni sana japo mlitawaliwa na ROHO YA KWANINI? Cha ajabu ni kwamba hadi wale ambao ni sehemu ya beneficiary wa haya madai yetu nao walijifanya wajanja na kupinga hii approach bila kuleta njia mbadala. Sasa hata wao wamepata pesa pamoja na kubeza kote. Ukweli ni kwamba njia zingine za kuandika barua na kupiga simu zilishagoma, hivyo hii option ya JF ilikuwa haiepukiki.

Pia niwashukuru sana wote waliochangia hii mada in a positive way, kwani walionyesha concern yao hasa kwetu tulio nje ya nchi na mateso tunayopitia. Ahsante sana, kwani hamkuwa na roho ya kwanini bali mlitanguliza uhalisia katika suala hili.
 
Hizo kozi mnazosoma huko hazipatikani Tanzania?

Nashindwa kukusaidia, kwani inaelekea huelewi nini maana ya watu kwenda kusoma nje ya nchi moja na wengine kuja kusoma ndani ya nchi nyingine. Kwa ufupi, hii program ilikuwa initiated na serikali yenyewe baada ya kuona umuhimu wa huo utaratibu.
 
Rudini nyumbani...... Hizo kozi huku hazipatikani???
 
Mh. Rais wangu Mpendwa Dr. Magufuli,
Pole na majukumu ya kujenga nchi yetu kutokana na changamoto za kujenga nchi yetu. Pamoja na hayo nataka kuchukua fursa hii baada ya uvumilivu wa mda mrefu kukuelezea masikitiko yetu na jinsi tunavyoteseka sisi wananchi wa Tanzania tunaosoma na kuishi hapa Ujerumani. Unaweza ukajiuliza ni kwanini hii barua ya wazi iandikwe kwako na si kwa watendaji walioko chini yako kama waziri wa elimu, katibu mkuu wa wizara, wakurugenzi au makamishina wa elimu. Jibu ni kwamba; HUKO KOTE TUMESHAFIKISHA MALALAMIKO YETU LAKINI HATUKUPATA UFUMBUZI WOWOTE. Lakini pia unaweza ukajiuliza ni kwanini iwe kwa njia ya Jamii Forums? Jibu ni kwamba kama barua, mails, na hata kiongozi wetu kufuatilia malipo yetu toka TCU, HESLB na Wizarani hizo njia hazijazaa matunda na si ajabu ofisi yako haina taarifa hii. Na kwa msingi huo, mimi nikiwa mmoja wa waathirika na ambaye kwa kiasi kikubwa sana nimefanya jitihada za kila namna ikiwemo kuwasiliana na watendaji wakuu wa TCU, HESLB (Mkurugenzi Mtendaji Mr. , na Mkurugenzi wa Fedha Mr....), na wizara ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu, lkn katika njia zote hizo HAKUNA MAFANIKIO NA SASA NI MIEZI MINNE baadhi yetu tunakaa nje ya nchi bila kupata pesa za kujikimu toka Tanzania kupitia HESLB na TCU.

Mh. Rais wangu, sisi waathirika ni wanafunzi tunaosoma huku Ujerumani kupitia mpango maalumu kati ya serikali yetu pendwa na serikali ya Ujerumani kupitia program ya MoEVT - DAAD (ukitaka kujua zaidi kuhusu hii program muulize yule katibu mkuu uliyemuhamisha majuzi kwenda wizara ya sheria kwani anajua kila kitu kuhusu hii programu. Lakini pia waweza kumuuliza yule kamishna wa elimu ambaye ni Prof...., yupo pia mkurugenzi mkuu wa HESLB, na Mkurugenzi wa Fedha wa HESLB. Hao watakuambia A-Z ya program hii kwasababu ni kama miaka 2 sasa toka waliposafiri na timu yao kuja Ujerumani kwa kodi zetu kwa kile walichokiita kuja kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo yetu hasa namna ya kuweza kuwalipa wanafunzi hawa stipend allowances zao kama mkataba unavyoonyesha. Hatahivyo, hatujaona matunda ya safari yao, kwani mpaka sasa matatizo ndiyo yamezidi. Nasema yamezidi kwani kabla ya kuja kwao angalao waliotutangulia walikuwa wakilipwa japo katika kipindi cha mwezi hivi. Hii ni tofauti na sasa ambapo kuna baadhi yetu hawajalipwa Stipend allowances zao za mwezi Oktoba, Novemba, na Desemba 2015. Pamoja nao, wale wote wenye familia huku ujermani wana miezi 3 (Oktoba-Desemba 2015) bila kulipwa pesa hizo.

AJABU LA MWAKA:
Mh. Rais, katika suala hili kumekuwa na mambo ya ajabu sana hasa kutoka kwa watendaji wa HESLB (Mkurugenzi wa Fedha). Huyu bwana amekuwa akitudanganya sana toka mwezi Oktoba 2015 kuhusu malipo yetu. Imefikia hatua wanaandaa majina yetu pale ofisini kwao na kiasi tunachopaswa kulipwa na kuonyesha kwamba tayari pesa zimepelekwa Benki. Sisi waathirika tunakaa kama wiki nzima bila kuona pesa kwenye akaunti zetu, na kiongozi wetu huku Ujerumani akifuatilia anaambiwa kuna kosa lilitendeka, hivyo, malipo yatanyika muda sio mrefu. HESLB chini ya Mkurugenzi Mtendaji na Mkurugenzi wa Fedha wametudanganya sasa zaidi ya mara 3 sasa kwamba pesa zimeshatumwa wakati ni UONGO. Hii hali imetusababishia usumbufu mkubwa sana katika mambo yetu ya kielimu na hata kijamii. Hata leo kiongozi wetu huku ujerumani alikwenda wizara ya Elimu baada ya kudanganywa tena na HESLB kwamba tungelipwa pesa zetu wiki iliyopita. Huko kote hakuna mafanikio, kwani bado ameambiwa tuandike tena barua japo suala letu linajulikana sana pale wizarani, TCU na HESLB.

Mh., Rais,
Hakika tunaumia sana na kwa hakika hatujui nini cha kufanya sasa, kwani shule na njaa na usumbufu wa kodi za pango ni mkubwa sana kwetu. Charges nazo zimekuwa nyingi sana na mbaya zaidi sasa tumekuwa ombaomba hadi wametuchoka. Kuna hoja hapa labda kuhusu sisi kutafuta kibarua huku ili tuweze kujikimu, hilo kwanza lina implications katika kusoma kwetu lakini pia mkataba wetu unatuzuia kufanya kazi. Kwa program hii ni kwamba Wizara ya Elimu kupitia TCU na HESLB inatakiwa kutulipa 80% ya Stipend allowances zetu na DAAD ya Ujerumani inalipa 20% pekee. Kwa 20% ya DAAD haitoshi hata gharama ya Chumba achilia gharama ya kula na hata registration fees.

Mh. Rais, kwa namna ya kipekee sana tunaomba utusaidie, kwani tuna hali mbaya sana. Hatujapata Stipend allowances ya Miezi 3 (Oktoba-Desemba 2015) pamoja na Family allowances ya miezi hiyo.

Natanguliza shukrani na tunaangalia mbele kwa matumaini ya suala letu kupata ufumbuzi mapema.

Ahsante sana na nikutakie kila la kheri katika ujenzi wa Taifa letu pendwa la Tanzania.

Ndimi, muhathirika wa HESLB/TCU/Wizara ya Elimu.
kufeni tu maana hakuna namna raisi kapiga marufuku safari za nnje nia yake ni kubana matumizi nyinyi hamtaki mbona vyuo viko vingi bongo ila mlitaka mashauzi serikali kwa sasa haina hela pesa zote zipo kwenye miradi kwa kuwasaidia subirini sikuu tukifuta pesa zake ndizo tutakazo watumia kama nauli sio za kujikimu
 
Nendeni ubalozini,kila kitu kaachiwa balozi. Ngosha hana habari na yanayoendelea huko nje. Tuko bize kuvunja nyumba/vibanda vilivyojengwa maeneo hatari. Poleni sana watanzania wenzetu,mnateseka huko ughaibuni.

ahsante sana mzee kwa ushauri.
 
Poleni Sana ila Ndio Ukubwa huo Challenge ya Maisha tu hiyo ili Mkomae hilo ni Somo la Kusurvive nadhani mmefaulu vizuri mkirejea hamna haja ya kwenda JKT kazni moja kwa moja....

Ila Sijui kama Mlipata Ruhusa ya kusafiri Nje.. Kosa la Kwanza... nadhani atawasikia kilio chenu hayo ndio majipu madogo madogo aliyokuwa anayataka... Sasa mkirejea mfundishe na wengine muache dharau kwani Dharau huwa zinarithishwa so msione hali hiyo ndio na nyie mtakuja wafanyia wengine hivyo hivyo mbona walimu wananyongwa na wametulia tu wamebakia kuimba Raisi Utatuachaje... wakati Mwenzao anakumbukia Bakora alizocharazwa Shuleni...
 
Hapo HESLB pameshaoza!!!! Inasemekana kuwa senior decision-makers wa hiyo bodi huwa wanapeleka hizo pesa kwenye mabank for fixed accounts kwa maslahi yao binafsi kimagumashi. Ndo maana kuzipata ni mbinde, ni mpaka wanafunzi wagome, waandamane, ndo pesa inatolewa fasta.

In short, hili linchi linanuka uvundo kila idara ya serikali. Na hakuna pa kwenda kupeleka malalamiko ukapata msaada urgently coz "chain of command" mostly ishaoza inanuka uvundo!! Africa the 'black' continent!

Poleni sana wakuu. Stay firm huko mliko!

-kaveli-
 
Kwanza poleni sana kwa hii kadhia. Wachangiaji wengi katika huu uzi ni wapuuzi, wapinga maendeleo na sadists, ambao wengi ile kuona uko unasoma elimu ya juu kiroho kinawadunda. Ndo maana utapigwa madongo. Hii haishangazi sana maana watz siku hizi mtanzania mwenzetu akipata ajali wenyewe wanawahi kummalizia ili wapore chochote alicho nacho. Sijui hii roho ya kinyama ilianzia wapi haswa.

Kuhusu tatizo lenu, nafikiri JPM atakuwa na taarifa au wahuni wa pale Heslb au wizarani wanficha. Kikubwa ni kuwa tumieni njia stahiki kuwasiliana na ikulu ili kilio chenu kipate ufumbuzi. Poleni tena. Narudi kwa mitanzania yenye roho mbaya.. ni aibu kubwa kumdhihaki mtanzania mwenzako aliyeko katika shida.. kimsingi ni ujuha kufanya hivyo. Najua hasira zenu ni ile kwa nini mmekosa na wengine wamepata..

Isiwe tabu, na nyinyi jibidiishe mtafanikiwa. Mambo mnayofanya yanaliaibisha taifa na hamuongezewi chochote kwa kufurahia shida na mataabiko ya ndugu zenu. Sijui watanzania siku hizi wanapiga viroba sana? Acheni hizo.. aaaiibuu
 
Naongeza size wasome vizuri

Nawashukuru wote mliochangia hii mada iwe kwa muono chanya au hasi. Hatahivyo, ukweli ni kwamba serikali iliingia hii program kabla ya sisi wahathirika kuingia mkataba huo. Hivyo, ni jukumu la serikali yetu kupitia HESLB na TCU kuhakikisha kwamba tunapata stahiki yetu, kwani initiators wa huu mpango ni serikali na sio sisi. Kwa wale wenye roho mbaya wanaobeza sisi kuja kusoma nje ya nchi wanapaswa kujua kwamba sisi tuliletwa na serikali kwakuwa ulikidhi vigezo vya nchi zote mbili (Tanzania na Ujerumani), hivyo ni jukumu la serikali yetu kuheshimu sehemu ya mkataba. Kwa upande wa ujerumani, wao kupitia DAAD wanatimiza upande wao bila shida na kwa wakati.
 
Back
Top Bottom