Rais Magufuli: Tunataka Tanzania ianze kutoa misaada hata kwa nchi za Ulaya

Wanasema sisi kuja kufikia kiwango cha nchi za Ulaya kunatakiwa miaka walau 500 huku wao wakiwa 'wamesimama' (yaani hawafanyi maendeleo yoyote).

Unajua pia ukiwa unapitia pitia huko Ulaya unapata kupajua vizuri na watu wake maana sometimes unaweza kuwa na Ulaya ya ndotoni! Haya ngoja tusubiri.
Mkuu usemacho ni kweli nchi ikiitwa imeendelea, imeendelea sio longolongo acha kabisa. Ulaya ulaya tu
 
Huyu mzee anashida kichwani siyo bure ndiyo maana alisema mwaka 2015 sukari ilikuwa inauzwa elfu 5 wakati ilikuwa chini ya 1700. Hii misaada anayosema Tz itowe labda wilayani lakini siyo Ulaya.
 
Tafadhalini BBC, msiripoti Hii habari, ilikuwa ni Utani tu wa Rais wa Wanyonge akitania Wanyonge wake!
 
Nafikiri Geography imekupiga Mtama, Botswana ipo Africa na Masikini kuliko Tanzania
Pohamba are you serious? Nimeishi huko najua kuliko unavyofikiria usije ukafikiri kwa sababu ipo Afrika ndio iwe masikini! Wanathibiti madini yao kuliko kawaida. Kama huna taarifa just google it mkuu!!
 
Pohamba are you serious? Nimeishi huko najua kuliko unavyofikiria usije ukafikiri kwa sababu ipo Afrika ndio iwe masikini! Wanathibiti madini yao kuliko kawaida. Kama huna taarifa just google it mkuu!!

Sio issue ya ku Google Wewe unazungumzia GDP ya Nchi Mie Nazungumzia Welfare ya Local citizens!
 
Sio issue ya ku Google Wewe unazungumzia GDP ya Nchi Mie Nazungumzia Welfare ya Local citizens!
Nakuambia welfare ya general citizens ni nzuri sana narudia tena nimeishi Botswana siyo nimeambiwa na mtu na bahati nzuri hata ulaya nimekaa mkuu mpaka ombaomba wapo ila wanaomba kwa njia tofauti
 
Upinzani ulifanya kosa ambalo watalikumbuka milele kuikataa katiba iliyopendekezwa na bunge la katiba. Ndoto ya Kikwete ilikua akumbukwe angalau kwa kuacha katiba. Leo ungekuta tuna katiba na japo haingekidhi ingekua ni ya kujazia nyama tu. Ile katiba pendekezwa ilikua na mambo mengi mazuri kama tume huru ya uchaguzi, ilikua imepunguza sana madaraka ya rais etc etc. Kwa sasa nadhani mabadiliko ya katiba si jambo la karibuni.
Usichanganye mambo kaka. Katiba iliyopendekezwa ni ipi ambao wapinzani waliikataa?.Katiba iliykataliwa na wapinzani ni ile iliyochakachuliwa , ya Nyoka mwenye makengeza, na RIP, Samuel Sita.
 
umeshindwa kuwapandisha watumishi madaraja na kuwaongezea mishahara,,,eti utoe misaada nje,, non-sens
 
Tatizo muda wote mnahangaika kutafuta X, wakati wenzenu wa ulaya wanatafuta thamani ya X. Mtahangaika kutafuta mchawi bure, mshajiroga wenyewe mchana kweupeee
 
Samahani kwa kuwatoa nje ya mada, hivi, vile vyerehani 25 tulivyosadiwa zuji zuj...aah, I mean juzi juzi vimeshaanza kazi?
 
5197e4e527ac66c8bcccaa0b30534188.jpg
 
Haya maajabu mapya! Yaani we huwezi kuendesha gari lkn unawaaminisha abiria et gari likianza kuondoka tutawabeba abiria wengne mbele,litaondokaje sasa!!!?
Yaan mtu kakiri mwenyewe alikuwa anajarib akasokomezwa lkn anataka kutuaminisha kwamba ana uwezo kutupeleka mbele kimaendeleo kiss hicho,uongo uliokomaa!!!
 
Back
Top Bottom