wwww
JF-Expert Member
- Mar 20, 2012
- 350
- 252
Mgogoro wa Korea Kasikazini na Marekani umetengeneza uzi huu na kuona kuwa kuna umuhimu wa makusudi kabisa wa kuanza kutengeneza zana zetu za kijeshi mapema sana. Ukisoma historia nchi nyingi ambazo tulikuwa nazo kwenye uchumi wa daraja la tatu kama China, Korea, Philipino na nyingine nyingi zimepiga hatua sana za kimaendeleo achilia mbali silaha za kijeshi.
Hatua iliyofikiwa na Korea ya Kasikazini ya kuwekeza kwenye silaha za kujilinda kunaifanya leo ifikie hatua ya kuitishia hata nchi kama Marekani ambayo imeanza kutengeneza silaha zake miongo mingi iliyopita. Hii ni hatua nzuri na mimi binafsi naipongeza sana Serikali ya Korea ya Kasikazini. Ili nchi iwe salama lazima ijilinde dhidi ya adui yeyote yule haijalishi ni mkubwa au mdogo kiasi gani na ni wajibu wa Serikali yoyote kuhakikisha usalama wa watu wake unalindwa kwa nguvu yoyote ile.
Nchi yetu Tanzania ni kubwa sana kieneo na kuna mataifa mengi yanaitamani kuiona ikiwa imemeguka vipande vipande ili kuipunguza nguvu yake. Hivyo ili tuwe na uhakika wa kuilinda mipaka yetu kisawasawa lazima tuwe na silaha za kutosha, kisasa na ambazo adui yetu atapata kigugumizi kutuvamia huku akijua tuna uwezo mkubwa kidhana za kivita.
Tanzania ukimlinganisha na binadamu ni mtu mzima, tuachane na mawazo ya kujiona kama bado ni nchi changa, tumekua sasa tunatakiwa tuanze sasa kujiwekea mazingira mazuri ya kujilinda kama nchi.
Mhe. Rais tuanze kidogo kidogo angalau kwa silaha ndogo kama Pisto, SMG na silaha nyingine za kawaida kabla ya kufikia kwenye silaha za Nyuklia. Tunapaswa kufika huko sasa na sio kesho. Tuanze leo kutengenza. JWTZ linaweza kufanya hivyo kupitia kikosi chake cha NYUMBU au kikosi chochote kile kama ambavyo tunatengenza risasi kwenye kikosi cha Mizinga kule Morogoro. Mhe. Rais tumechelewa sana kuanza, katika umri huu tulitakiwa tuwe tayari tunatengeneza vifaru.
Mhe. Rais nakuomba sana usiwasikilize askari pale Makao Makuu ya JWTZ (NGOME) kuhusu hili watakupotosha kwa sababu wao wanataka tuendelee kununua silaha nje ili wapate commission (10%) zao kwenye bei za silaha zinazonunuliwa nje. Fanya maamuzi leo usingoje kesho, hapo utakuwa umejiwekea historia kubwa sana katika nchi hii na kuiondolea Serikali mzigo mkubwa sana wa kununua silaha nje ya nchi kama tunavyofanya sasa.
Najua kuna Watanzania wataona kama sio kipaumbele lakini hakuna kipaumbele zaidi ya ulinzi katika maisha ya mwanadamu yoyote hapa duniani.
Mhe. Rais nakutakia kila la kheri katika uamuzi huu mgumu utakaokuwa na vikwazo mbele yako, SIMAMA IMARA KATIKA HILI.
Naomba kutoa hoja!!!!!!!!!!!!!!