Msishangae hizo pesa zinazochangwa mkasikia zimeamuliwa zinunuliwe madawati. Maana awamu hii kwa vipaumbele tu hatuiwezi.
Kuna ambao wameshashungulikiwa na kuna baadhi bado kama Escrow. Kumbuka serikali hii haina hata mwaka tangia imeingia madarakani lakini imeweza kuwaondoa viongozi wengi waliokuwa wanasababisha kutokea na kuenea.Too low-escrow escrow escrow! Ni mafisadi gani wanashughulikiwa Kama waliohusika na skendali ya escrow wanatanua mitaani?
Kwa kweli sina milioni saba ya kulipa... Ila Mkuu ana maneno mazito! Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali itawasaidia pale waliposhindwa.
Mkuu anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM. Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali, sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya.
Na wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu anasema waache mara moja.
Na kasema wote wanaotumia janga hili kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.
Nashukuru mkuu kama imeisikiliza kiasi cha kuandika neno kwa neno!!Lkn je umeishia kusikiliza hii hotuba ya ITV tu?Au ulipata nafasi ya kusikiliza pia AZAM TWO?Umeona hotuba nzima au ni hii ya vipande vipande?Kwanza napenda nikupongeze Mkuu kwa kujitahidi kutuletea hii habari. Hata hivyo naomba tu niseme kuwa kuna baadhi ya maneno (mekundu hapo juu) umeyaongeza wewe, Mheshimiwa Rais hakuyatamka.
Pili, niliamua kuisikiliza maneno yote ya Mheshimiwa Rais, baada ya kusikiliza kwa makini Zaidi ya mara moja nimejiridhisha kuwa Mheshimiwa Rais ametamka kama ifuatavyo:
"Hii ni mipango ya Mungu, tetemeko haliletwi na Serikali, wala tetemeko haliletwi na CCM. Ni jukumu la sasa hivi sisi kama nchi ni kuhakikisha tunawasaidia wenzetu ambao wamepata matatizo haya. Tusilitumie tetemeko hili kwa njia zingine sijui za kujiimarisha kisiasa, mtu unakwenda unazungukia weee nyumba zilizozunguka, unatoka unatamka huko. Watu wa Kagera wanahitaji msaada, siyo maneno.
Matapeli wapo na wamejipanga kweli; tunachangia Kagera, tunafanya nini, kumbe anachangia tumbo lake. Hili ni lazima tuliangalie na nitoe wito kwa vyombo vya dola, muwafuatilie hawa ambao wamekuwa wanasingizia wanachangia Kagera na nini, wakati wanajichangia wao, washikwe na ikiwezekana wapelekwe kwenye vyombo vya sheria ili wakajibu hizo hoja za kitapeli na wizi wa kuwaibia watu maskini ambao wana shida za kiukwelikweli.
Wananchi waambiwe ukweli, hili tetemeko halikuletwa na Serikali; wote tunasikitika, wote tunalia na ndiyo maana hata sisi Serikali tunajipanga katika kusaidia, tutaendelea kuwasaidia lakini na wao pia wajisaidie. Wasikae wakasubiri tu kwamba ukuta wangu umebomoka hapa hata kuparudishia hataki, anasubiri nasubiri kuna hela za Serikali zinakuja. Tetemeko limetokea, siyo mwisho wa maisha, waanze kujipanga kwa kufanya kazi."
Ni ushauri wangu kuwa tuwe makini tunapoandika mada ili kuepuka kuongeza chumvi au kuhafifisha ujumbe uliotolewa.
Kwaiyo tunaofiwa wote ndugu zetu tuitegemee serikali kutusaidia misaada? Rais kawaambia unwell ili wasibweteke sana
Hamia Somalia. Niko tayari kukusindikiza.Hapa tumeingia cha kike jamani,mbona najuta kua mtanzania.
Kaka ,huyu ni rais ni muhimu angetoa kauli ya faraja.Amezungumza kama MTU Wa kawaida .Wabongo mi nawajua sana kwa kupenda kuteleza,wengine nyufa tu,wanasubiri serikali ije iwajengee
Nami namuunga mkono.Uko sawa Amri jeshi wetu My.John Joseph Pombe Magufuli.
Kwa hiyo unataka kusema kuwa hicho ndicho kilichomfanya asiende!!?unashangaa? wapo wanasiasa tena wakubwa wanataka ionekane kama serikali na ccm ndio wameleta tetemeko bukoba. baada ya tetemeko wamefika bukoba kama mshale hadi after shocks zimewakuta bukoba. kufika tu wakaanza kumlaumu rais kwamba hajafika bukoba na kulaumu serikali.
Rais ametoa ukweli wenye uchungu! Ni kweli c wote wenye uwezo wa kununua hata bati 2 ila wale wenye UWEZO waonyeshe njia ya kusaidiwa! Siamini kuwa umejenga boma afu serikali ikashindwa kukuchangia bati za kuezekea!! Naomba nisieleweke vibaya ila tu serikali inatakiwa kupeleka hiyo misaada haraka sana kabla mvua hazijaanza kunyesha!Kuna usahihi katika kauli ya Rais hasa kwa wale wanaoutumia haya Majanga kama njia ya kubweteka, maana majanga yameshatokea na maisha yatendelea na serikali haitaweza kusaidia kila mtu , mfano wale wanaotaka wajengewe Nyumba na serikali.
hata hivyo kuna ambao hawataweza kufanya shughuli zao za kila siku mpaka mambo yawe shwari.
Mkuu hapo ndipo unapo_miss target; kilicho mbele yetu hapa jamvini ni maneno aliyoyatoa ambayo yameleta ukakasi mwingi miongoni mwetu.Makoye Matale
Rais kafika BK kujiinea mwenyewe wapiga kura wake wanavyo teseka na wengine kufiwa zaidi ya kaya 15?
Kumtetea kwako hakuna maana yyt