Rais Magufuli, tembelea Wizara ya Maji ujionee madudu

Rais Magufuli, tembelea Wizara ya Maji ujionee madudu

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,621
Reaction score
14,577
Kwa mtindo anaoufanya Rais Magufuli, wengi tuna uhakika sasa serikali itaamka toka usingizi wa pono uliodumu miaka kadhaa sasa.
Matembezi ya Ulaya kwa Makatibu wakuu, Mawaziri na hata ma kamishena na wakurugenzi mawizarani sasa yatakoma, kama si kuisha kabisa.

Wafanyakazi serikalini hawafanyi kazi for lack of supervision.

Wasimamizi wako busy kujitajirisha na marupurupu ya safari nyingi na alawansi.

Si mara moja nimesafiri nje kwa hela yangu.Utakuta Business Class na First Class zimejaa wafanyakazi wa serikali, wakurugenzi na hata mawaziri.

Wizara moja ambayo inasikitisha kuliko ni wizara ya Maji.

Na hili si jungu wala hadithi za kutunga.

Hela inayotengwa kwenye bajeti haifiki kabisa mikoani, hela inaishia kwenye warsha , kongamano na hata mikutano isiyo na tija kwa wananchi.

Kuna mkoa fulani ambao redio ya jamii ilifanya utafiti na kukuta kwa miaka zaidi ya mitatu na katika wilaya karibu zote, fedha za miradi ya maji kwa wananchi haifiki kabisa mkoani.

Hiyo ni licha ya fedha kutengwa na kufika Wizara ya Maji.

Mheshimiwa Magufuli , tunaomba ufike hapo ujionee mwenyewe.
 
Kukosekana visima ndio huwa sielewi kabisaaaa. . . . .Watu binafsi wanapiga deepwells kijiji kizima kinakosa hata moja??!!!
Upepo upo na jua kali kama pasi. . . .. uko sawa masopakyindi

Eti waziri profesa. . . . .
Ni muda tu . . . .vilio vya wananchi vimesikika
 
Last edited by a moderator:
Kwenye maji kama inawezekana ndipo angeanzia, Tanzania tuna maji mengi sana lakini tatizo la maji ni kubwa kuliko uwingi wa maji tuliyo nayo.
 
Wizara ya Maji ni kichefu chefu..
JPM chonde chonde wazukie.

Kama kuna wizara ina madudu ya kufedhehesha, basi Wizara ZYa Maji imetia fora.

Kwenye maji kama inawezekana ndipo angeanzia, Tanzania tuna maji mengi sana lakini tatizo la maji ni kubwa kuliko uwingi wa maji tuliyo nayo.

Nasikia kuna idara moja wamejaa watu wa kabila Fulani tu,ni hatari

Hali ya hatari sana hii.
Na hao wahusika utawakuta nao wanailalamikia serikali kuwa haiwajali wananchi wala kuwaletea maendeleo, wakati hapo walipo wao ndio serikali haswaa...na wavuruga maendeleo ni hapo hapo.
 
Last edited by a moderator:
Kukosekana visima ndio huwa sielewi kabisaaaa. . . . .Watu binafsi wanapiga deepwells kijiji kizima kinakosa hata moja??!!!
Upepo upo na jua kali kama pasi. . . .. uko sawa masopakyindi

Eti waziri profesa. . . . .
Ni muda tu . . . .vilio vya wananchi vimesikika

Huyo Profesa Maghembe ndo alikuwa uozo wa kutupwa, heri hata naibu wake.
Sijui mara ya mwisho ni lini alitembelea miradi hewa vijijini.
 
Last edited by a moderator:
shida sio wizarani...shida ipp hazina kubadilisha matumizi ya fedha za bajeti..
 
Huyo Profesa Maghembe ndo alikuwa uozo wa kutupwa, heri hata naibu wake.
Sijui mara ya mwisho ni lini alitembelea miradi hewa vijijini.

Katika mawaziri wa Maji Maghembe amejitahidi sana..sehemu alipopewa hela miradi imefanyika..
 
Katika mawaziri wa Maji Maghembe amejitahidi sana..sehemu alipopewa hela miradi imefanyika..
Fuatilia mada, hatumpigi vita si ajabu tatizo lake ni ufuatiliaji miradi, hata iwe midogo iasi gani.
Nimesema kuna mkoa ambao fedha ilitengwa, na ikafika wizarani na bado fedha hiyo ikayeyukia kwenye mafaili na haikufika katika vijiji vilivyotrajiwa kunfaika na miradi hiyo.
 
Katika mawaziri wa Maji Maghembe amejitahidi sana..sehemu alipopewa hela miradi imefanyika..
Mkuu uzembe huwa haujifichi.
Mbona wizara ya ujenzi ilifanya na kutekeleza miradi ya ujenzi hata kwa kuianza tu, na wakaendelea kungojea fedha toka wizara ya fedha.
Tatizo la umangimeza linarudisha nyuma wizara hii, na kwao ni business as sual.
Wizara inahitaji kutikiswa, na wizara hii ina miradi mikubwa tu kama wizara ya ujenzi.
 
Back
Top Bottom