Rais Magufuli, TANESCO Kigamboni kuna tatizo

RasJah

JF-Expert Member
Nov 5, 2009
703
64
Mh Rais pole na kazi nyingi ofisini.Naandika hapa nikiwa na masikitiko makubwa sana na sikutaka kufanya hivi kwani niliamini ofisi ya tanesco kigamboni ilikuwa bado ina uwezo wa kutusaidia sisi wananchi wa kisarawe 2.

Lakini kwa urasimu uliopo na majibu yao yanayoshawishi mazingira ya rushwa naomba kukueleza kuwa Tanesco Kigamboni hawataki kutupatia umeme wakazi wa Kigamboni kisarawe 2.

Umeme uliopo tulichangishana mwaka jana kuanzia nguzo, nyaya mpaka transformer tuliyopewa na mfadhili mmoja, baada ya hapo umeme ukawa ukaiishia zahanati ya kijiji tu. Lakini tunashukuru kuwa mwezi wa 12 mwaka jana tuliambiwa kuwa kisarawe 2 imepata milioni 72 kwa ajili mradi ambao angalau utasogeza nguzo na kubadilisha transformer kwani ni ndogo.

Tumekuwa tukifatilia kwa karibu sana ili hatimaye waje sasa wasambaze nguzo lakini majibu yao hasahasa huyu anajiyiita meneja msaidizi Deki kuwa wametingwa na kazi ofisini wakipata nafasi watakuja, wakati huohuo watu wenye uwezo wanafungiwa umeme hata jana gari ya Tanesco ilikuwepo kisarawe 2 wakimfungia umeme mteja mmoja.

Kuna baadhi ya wananchi walitaka kuvuta umeme kwa gharama zao meneja anasema hawawezi kwa sababu transformer ni ndogo wasubiri mradi ambao imetegwa hela ya transfomer kubwa na kuongeza njia za umeme, lakini mh tumechoka kusubiri ilhali tunaambiwa pesa ya mradi imeshatoka, tatizo tu hawana nafasi, sio mazingira ya kuomba Rushwa haya mheshimiwa.

Mh Rais tumefatilia sana kupitia viongozi wetu , mpaka diwani, majibu yao wanasema na wao wamechoka sasa manake wakienda ofisini tu meneja anawakimbia.Tumefatilia mpaka wilayani, majibu ni mabovu, na mwisho tumeambiwa mbona tatizo lenu hata waziri anajua kama mnataka nendeni kwa waziri.

Mh Rais tunaomba msaada wako tunahitaji sana umeme, maisha bila umeme ni magumu sana.Nisamehe kwa kama nitakuwa nimekosea Mh Rais, lkn wakazi wa kigamboni kisarawe 2 tunakupenda sana na endeleaa kutumbua majibu likiwemo hili.
 
Mimi nina nyumba yangu imeisha nusu mwaka sasa, nasubiri Tanesco walete umeme, nguzo nahitaji kama nguzo nne tu, nilienda tanesco wakaniambia siwezi kuvuta umeme nguzo nne, nguzo zikizidi tatu huo ni mradi....Dar bila umeme ni jehanam, na sihamii ng'o mpaka umeme uje.Kero za mwenye nyumba zinavumilika.
 
Hiyo ipo ngazi ya Waziri Muhongo
Kama nimemwelewa vzr amesema tanesco kigamboni wamejibu kuwa suala la kisarawe 2 hata waziri anajua, so kama anajua na umeme toka mwaka jana haufika,waziri naye si nijipu
 
Hili la kigamboni ni jipu lililoiva coz hata wakazi wa kigamboni mchikichini ni hivo hivo,umeme unawaka dege umeruka mchikichini unawaka muembe mdogo ni maajabu na kama kawaida majibu ni hamko kwenye budget
 
Mimi ninawasiwasi na utendaji kazi wa TANESCO, wameshindwa kupeleka umeme hata hapa Dar-es-salam sasa huko vijijini utaja fika lini. Yapo maeneo kama Bomba mbili ya Ukonga yameshaendelezwa kwa kiwango kukibwa sana na wapo wananchi wengi sasa hivi wakiwemo wale waliohamishwa kutoka kwenye mabonde hatarishi kule jangwani na kwingineko, lakini pamoja na kuwepo watu wengi umeme bado kupelekwa maeneo haya. Namshukuru Mheshimiwa Waziri alipoeleza kuwa mpamgo upo njiani ambapo TANESCO watashindanishwa na makampuni mengine kuzalisha na kutawanya umeme kwa wananchi ili kuondoa ukiritimba uliopo.
 
Mh Rais pole na kazi nyingi ofisini.Naandika hapa nikiwa na masikitiko makubwa sana na sikutaka kufanya hivi kwani niliamini ofisi ya tanesco kigamboni ilikuwa bado ina uwezo wa kutusaidia sisi wananchi wa kisarawe 2.

Lakini kwa urasimu uliopo na majibu yao yanayoshawishi mazingira ya rushwa naomba kukueleza kuwa Tanesco Kigamboni hawataki kutupatia umeme wakazi wa Kigamboni kisarawe 2.

Umeme uliopo tulichangishana mwaka jana kuanzia nguzo, nyaya mpaka transformer tuliyopewa na mfadhili mmoja, baada ya hapo umeme ukawa ukaiishia zahanati ya kijiji tu. Lakini tunashukuru kuwa mwezi wa 12 mwaka jana tuliambiwa kuwa kisarawe 2 imepata milioni 72 kwa ajili mradi ambao angalau utasogeza nguzo na kubadilisha transformer kwani ni ndogo.

Tumekuwa tukifatilia kwa karibu sana ili hatimaye waje sasa wasambaze nguzo lakini majibu yao hasahasa huyu anajiyiita meneja msaidizi Deki kuwa wametingwa na kazi ofisini wakipata nafasi watakuja, wakati huohuo watu wenye uwezo wanafungiwa umeme hata jana gari ya Tanesco ilikuwepo kisarawe 2 wakimfungia umeme mteja mmoja.

Kuna baadhi ya wananchi walitaka kuvuta umeme kwa gharama zao meneja anasema hawawezi kwa sababu transformer ni ndogo wasubiri mradi ambao imetegwa hela ya transfomer kubwa na kuongeza njia za umeme, lakini mh tumechoka kusubiri ilhali tunaambiwa pesa ya mradi imeshatoka, tatizo tu hawana nafasi, sio mazingira ya kuomba Rushwa haya mheshimiwa.

Mh Rais tumefatilia sana kupitia viongozi wetu , mpaka diwani, majibu yao wanasema na wao wamechoka sasa manake wakienda ofisini tu meneja anawakimbia.Tumefatilia mpaka wilayani, majibu ni mabovu, na mwisho tumeambiwa mbona tatizo lenu hata waziri anajua kama mnataka nendeni kwa waziri.

Mh Rais tunaomba msaada wako tunahitaji sana umeme, maisha bila umeme ni magumu sana.Nisamehe kwa kama nitakuwa nimekosea Mh Rais, lkn wakazi wa kigamboni kisarawe 2 tunakupenda sana na endeleaa kutumbua majibu likiwemo hili.
ndugu mtoa hoja mradi wa kuunganishiwa umeme wananchi wa kigamboni eneo la kisarawe 2 ni mradi ambao kwenye action plan ya Tanesco wilaya ya kigamboni umepangwa kuanza mapema may yaani mwezi ujao na utakamilika baada ya wiki mbili mpaka tatu hivyo ifikapo tarehe za katikati ya ya mwezi may kisarawe 2 yote itakuwa na umeme.
mradi huu utajumuisha uwekwaji wa nguzo na kutoa transfoma ndogo ya 50KVA iliyokwepo na kuweka nyingine kubwa zaidi ya 200KVA itakayoweza kuhimili ongezeko la idadi ya wateja watakaoongezwa katika kisarawe 2.
ndugu mtoa hoja ni vyema ukafuatilia mambo vizuri na kupata taarifa zote kabla ya kuja kupotosha wengine huku kwenye mitandao.

SI KWELI kuwa Tanesco imegoma kuwaletea umeme bali mradi wa kisarawe 2 katika ratiba nzima ya mwaka ya Tanesco kigamboni, ulipangwa kutekelezwa mwezi ujao ni vyema kuwa na subira muda si mrefu usiopungua mwezi mmoja eneo lote la kisarawe 2 litaunganishwa na umeme wa Tanesco.
 
Na kama Tanesco ikilazimisha kuwafungia umeme watu wa kisarawe 2 kama unavyotaka ndugu mtoa hoja kabla ya mradi huo mdogo wa wikimbili kukamilika na transfoma kufungwa lenye uwezo mkubwa zaidi wa 200KVA, matokeo yake ni kwamba transfoma hilo dogo lililopo sasa hivi litazidiwa nguvu ama kufa kabisa na kupelekea wateja wengine zaidi ya 100 wanaohudumiwa na transfoma hili kukosa umeme kabisa au kupata umeme mchafu kwa watumiaji wote wa transfoma hili.

hivyo tuwe na subira jaman Tanesco kigamboni inatambua kilio chenu na bajet ya mradi ilishaombwa na ipo tayari na mradi utaanza May. sio kulazimisha kujenga njia za umeme kwa kutumia vishoka na ambazo hazijakidhi viwango na kulazimisha Tanesco kupitisha umeme.
 
Mwezi wa pili nilikuja na diwani zahoor hapo tanesco lakini hamkutoa hilo jibu,yule mzee deki meneja msaidizi alisema wametigwa na kazi ofisini na watakuja wakati wowote wakipata nafasi, leo baada ya malalamiko unakuja na story ndeeeeeefu.tatizo lenu mnakuwa kama miungu watu wateja wakija ofisini, ila mkisikia magufuli, haja kubwa inawabana, mnaboa sana nyie nawachukia sana tanesco, nyumba yangu inachakaa ina nusu mwaka sasa, lkn siwezi kuhamia kwa sababu ya tanesco
 
Mwezi wa pili nolikuja na diwani zahoor hapo tanesco lakini hamkutoa hilo jibu,yule mzee deki manaje msaidizi alisema wametigwa na kazi ofisini na watakuja wakati wowote, leo baada ya malalamiko unakuja na story ndeeeeeefu.tatizo lenu mnakuwa kama miungu watu wateja wakija ofisini, ila mkisikia magufuli, haja kubwa inawabana, mnaboa sana nyie.
samahani kwa usumbufu wote ulioupata ndugu mteja lakini kwa mipango iliyopo eneo lako kisarawe 2 litapatiwa umeme mwezi ujao kisarawe 2 yote itakuwa imeunganishwa na umeme wa uhakika na usiosumbua kwa kuongezewa transfoma mpya na nguzo kuingia mtaani kwako. kama una swali lingine lolote lihusulo Tanesco na huduma zetu kwa Ujumla karibu saana na asante kwa kuendelea kuhitaji huduma zetu. tuko kwaajili yenu wateja.
 
Halafu mleta mada umeeleweka vizuri sana na naona ndg mawazo John kakujibu vizuri kwani suala la umeme ni more technical than siasa.tujaribu kuwaelewa wataalamu wetu pale wanapotuelewesha ukisema waharakishe kwa kufanya kazi kwa uoga km unavyosema ni jipu tutasababisha athari kubwa sana ktk jamii.
 
samahani kwa usumbufu wote ulioupata ndugu mteja lakini kwa mipango iliyopo eneo lako kisarawe 2 litapatiwa umeme mwezi ujao kisarawe 2 yote itakuwa imeunganishwa na umeme wa uhakika na usiosumbua kwa kuongezewa transfoma mpya na nguzo kuingia mtaani kwako. kama una swali lingine lolote lihusulo Tanesco na huduma zetu kwa Ujumla karibu saana na asante kwa kuendelea kuhitaji huduma zetu. tuko kwaajili yenu wateja.
Majibu yako yanatia faraja sana mr mawazo, lkn ubabaishaji muache jamani, sisi watanzania wenzenu tunaumia sana, kisarawe 2 ni kilometer 15 kutoka ikulu ya magufuli lkn hakuna umeme, Dar na joto hili tunaishije bila umeme, hebu mu aapply basi hata human factor basi kama hamtaki maendeleo ya umeme.
 
Mwezi wa pili nilikuja na diwani zahoor hapo tanesco lakini hamkutoa hilo jibu,yule mzee deki meneja msaidizi alisema wametigwa na kazi ofisini na watakuja wakati wowote wakipata nafasi, leo baada ya malalamiko unakuja na story ndeeeeeefu.tatizo lenu mnakuwa kama miungu watu wateja wakija ofisini, ila mkisikia magufuli, haja kubwa inawabana, mnaboa sana nyie nawachukia sana tanesco, nyumba yangu inachakaa ina nusu mwaka sasa, lkn siwezi kuhamia kwa sababu ya tanesco
Mwezi wa pili nilikuja na diwani zahoor hapo tanesco lakini hamkutoa hilo jibu,yule mzee deki meneja msaidizi alisema wametigwa na kazi ofisini na watakuja wakati wowote wakipata nafasi, leo baada ya malalamiko unakuja na story ndeeeeeefu.tatizo lenu mnakuwa kama miungu watu wateja wakija ofisini, ila mkisikia magufuli, haja kubwa inawabana, mnaboa sana nyie nawachukia sana tanesco, nyumba yangu inachakaa ina nusu mwaka sasa, lkn siwezi kuhamia kwa sababu ya tanesco
Pole sana kwa usumbufu na majibu ya karaha uliyoyapata?jee ushawahi kuonana na Meneja wa Kigamboni?
 
Mimi ninawasiwasi na utendaji kazi wa TANESCO, wameshindwa kupeleka umeme hata hapa Dar-es-salam sasa huko vijijini utaja fika lini. Yapo maeneo kama Bomba mbili ya Ukonga yameshaendelezwa kwa kiwango kukibwa sana na wapo wananchi wengi sasa hivi wakiwemo wale waliohamishwa kutoka kwenye mabonde hatarishi kule jangwani na kwingineko, lakini pamoja na kuwepo watu wengi umeme bado kupelekwa maeneo haya. Namshukuru Mheshimiwa Waziri alipoeleza kuwa mpamgo upo njiani ambapo TANESCO watashindanishwa na makampuni mengine kuzalisha na kutawanya umeme kwa wananchi ili kuondoa ukiritimba uliopo.
mpaka sasa makao makuu yote ya mikoa 24 ya Tanzania yameshaunganishwa umeme na makao makuu ya wilaya zote 130 kati ya wilaya 133 yameshaunganishwa umeme kasoro wilaya 3 tuu ambazo ni mpya zilizogawanywa hivi karibuni.
katika miradi ya umeme vijijini mpaka kufikia katikati ya mwaka huu tayari vijiji 2000 vitakuwa vimeunganishwa na umeme wa Tanesco nchi nzima, sasa UNAWEZAJE KUSEMA TANESCO IMESHINDWA KUPELEKA UMEME VIJIJINI NDUGU? acha kupotosha wanajamvi humu
 
ndugu mtoa hoja mradi wa kuunganishiwa umeme wananchi wa kigamboni eneo la kisarawe 2 ni mradi ambao kwenye action plan ya Tanesco wilaya ya kigamboni umepangwa kuanza mapema may yaani mwezi ujao na utakamilika baada ya wiki mbili mpaka tatu hivyo ifikapo tarehe za katikati ya ya mwezi may kisarawe 2 yote itakuwa na umeme.
mradi huu utajumuisha uwekwaji wa nguzo na kutoa transfoma ndogo ya 50KVA iliyokwepo na kuweka nyingine kubwa zaidi ya 200KVA itakayoweza kuhimili ongezeko la idadi ya wateja watakaoongezwa katika kisarawe 2.
ndugu mtoa hoja ni vyema ukafuatilia mambo vizuri na kupata taarifa zote kabla ya kuja kupotosha wengine huku kwenye mitandao.

SI KWELI kuwa Tanesco imegoma kuwaletea umeme bali mradi wa kisarawe 2 katika ratiba nzima ya mwaka ya Tanesco kigamboni, ulipangwa kutekelezwa mwezi ujao ni vyema kuwa na subira muda si mrefu usiopungua mwezi mmoja eneo lote la kisarawe 2 litaunganishwa na umeme wa Tanesco.
Mhh! Si kweli ndugu usiwatete TANESCO ni shirika ambalo limejaa urasimu sana kwa watendaji wake hawajui kuwa umeme ni haki ya kila mtu, imekuwa kero sana usambazaji wake. Kwa sasa umeme haupatikani mpaka eidha utoe hongo au unapoishi ni karibu na Kigogo wa serikali (mfano, Mkurugenzi, mkuu wa mkoa, mkuu wa jeshi Waziri Mbunge n.k)kama huku kwetu Toangoma (Mtaa wa Malela) kamati nyingi zimeundwa kufuatilia lkni mpaka sasa hakuna kinachoendelea; unasikia tu kwa mbaali umeme umepelekwa sijui, mkuu wa mkoa, siju mkurgenzi wa nini, Mbunge, au waziri, kama amejenga maeneo ya karibu na unapoishi lakni kwa watu wa kawaida umeme hauletwi hata kama unamudu gharama zote stahili.
Kwa kifupi umeme umekuwa kwa
1. Wanapoishi viongozi wakubwa wa serikali hata yuko pekeyake porini!
2. Au utoe rushwa ndipo upate hiyo huduma
Natoa hoja!!
 
Majibu yako yanatia faraja sana mr mawazo, lkn ubabaishaji muache jamani, sisi watanzania wenzenu tunaumia sana, kisarawe 2 ni kilometer 15 kutoka ikulu ya magufuli lkn hakuna umeme, Dar na joto hili tunaishije bila umeme, hebu mu aapply basi hata human factor basi kama hamtaki maendeleo ya umeme.
usijali ndugu Mkada yote hayo tunaelewa na nafahamu kisarawe 2 ilifika muda mkaamua kujijengea line yenu wenyewe kwa kutumia mafundi wenu lakini ikaonekana haijakidhi vigezo na ingeweza kuleta madhara kwenu badae kama Tanesco wangeingiza umeme katika laini hiyo na ilijengwa katika eneo ambalo Tanesco ndio walitegemea kupitisha laini kwaajili ya kuwaletea umeme hapo hapo kisarawe 2, asnteni kwa uvumilivu wenu na tunaomba muendelee kutuvumilia kidogo kwa hivi visiku vichache Mafundi wetu kigamboni hapo mtawaona sait wakichakarika kuwafikishia huduma mwezi ujao ndugu mteja. kama una kero nyingine ihusuyo huduma za Tanesco karibu sana.
 
Na kama Tanesco ikilazimisha kuwafungia umeme watu wa kisarawe 2 kama unavyotaka ndugu mtoa hoja kabla ya mradi huo mdogo wa wikimbili kukamilika na transfoma kufungwa lenye uwezo mkubwa zaidi wa 200KVA, matokeo yake ni kwamba transfoma hilo dogo lililopo sasa hivi litazidiwa nguvu ama kufa kabisa na kupelekea wateja wengine zaidi ya 100 wanaohudumiwa na transfoma hili kukosa umeme kabisa au kupata umeme mchafu kwa watumiaji wote wa transfoma hili.

hivyo tuwe na subira jaman Tanesco kigamboni inatambua kilio chenu na bajet ya mradi ilishaombwa na ipo tayari na mradi utaanza May. sio kulazimisha kujenga njia za umeme kwa kutumia vishoka na ambazo hazijakidhi viwango na kulazimisha Tanesco kupitisha umeme.
Asante kwa majibu yako kwa mdau wa Makao makuu ya Kata ya Kisarawe 2.
Pamoja na majibu yakao mazuri.Nami pia ni mkazi wa Kata ya kisarawe 2 eneo la Mwasonga. Umeme mkubwa umeshafika na hata baadhi ya wateule wachache wamewekewa transfoma na kufikishiwa umeme majumbani na karakana zao.
Naomba kujua, jee... ni lini na sie akina kapuku tutasambaziwa?
Naomba kutoa hoja.
 
Mhh! Si kweli ndugu usiwatete TANESCO ni shirika ambalo limejaa urasimu sana kwa watendaji wake hawajui kuwa umeme ni haki ya kila mtu, imekuwa kero sana usambazaji wake. Kwa sasa umeme haupatikani mpaka eidha utoe hongo au unapoishi ni karibu na Kigogo wa serikali (mfano, Mkurugenzi, mkuu wa mkoa, mkuu wa jeshi Waziri Mbunge n.k)kama huku kwetu Toangoma (Mtaa wa Malela) kamati nyingi zimeundwa kufuatilia lkni mpaka sasa hakuna kinachoendelea; unasikia tu kwa mbaali umeme umepelekwa sijui, mkuu wa mkoa, siju mkurgenzi wa nini, Mbunge, au waziri, kama amejenga maeneo ya karibu na unapoishi lakni kwa watu wa kawaida umeme hauletwi hata kama unamudu gharama zote stahili.
Kwa kifupi umeme umekuwa kwa
1. Wanapoishi viongozi wakubwa wa serikali hata yuko pekeyake porini!
2. Au utoe rushwa ndipo upate hiyo huduma
Natoa hoja!!
uko mkoa gani na wilaya gani ndugu Mtoomondo?
 
Hiyo ipo ngazi ya Waziri Muhongo
Sio muhongo, hata akienda kwa meneja wa wilaya au mkoa wa temeke atapata ufumbuzi.

Kwa hali ilivyo sasa mtu hata mke wake asipompikia atataka magufuri akamshughulikie,yani unakuta uchafu umetupwa barabarani watu wanataka magufuri akawashughulikie wenyeviti aa mtaa/vitongoji. Hii ni hatari.
 
Mimi nina nyumba yangu imeisha nusu mwaka sasa, nasubiri Tanesco walete umeme, nguzo nahitaji kama nguzo nne tu, nilienda tanesco wakaniambia siwezi kuvuta umeme nguzo nne, nguzo zikizidi tatu huo ni mradi....Dar bila umeme ni jehanam, na sihamii ng'o mpaka umeme uje.Kero za mwenye nyumba zinavumilika.
Walikusaidia au aalikushauri vizuri maana kuanzia nguzo nne gharama hua kubwa sana, ila kama unadhani una uwezo unaenda unalipia hua mradi inawesa hata kufika milioni 5 unawekewa umeme. Nenda wambie uko tayari kulipia mradi unapewa umeme.
 
Back
Top Bottom