Levels baby
JF-Expert Member
- Sep 26, 2019
- 831
- 768
Nimeleta bandiko hili sababu toka juzi nimekuwa na survey kwenye mkoa wa Pwani kwa ajili ya uwekezaji ambao tumeamua kama familia ya mzee Mundele tuwekeze katika nchi yetu na tuonyeshe uzalendo katika sera ya Rais wetu mzalendo Dr. John Pombe Joseph Magufuli, lakini nilichokikuta kiukwel nimekata tamaa.
1. Juzi baada ya kurudi kutoka katika mihangaiko ya kazi huko Kanda ya Ziwa mzee wangu akaniambia kafanye tulichongea (kitafuta eneo la uwekezaji yaani kiwanda kidogo).
Sasa kidume nikatua Mkuranga huku nimewaweka sawa watu wangu na baadhi ya vijana wanaojua maeneo ili tusaidiane lakini nilichokikuta kwa walionitangulia ni maigizo ya kutosha.
Yaani nakuta huko watu wamejenga majengo tena hayajaisha wameyaacha wanacheza tu nyani nikasema hawa viongozi wanaomwambia Rais tuna viwanda 400 Pwani wanamdanganya mzee wa watu.
2. Kali kuliko yote leo hapo Kibaha Zegereni viwandani ndio nimekuta vituko vya kutosha zaidi kuliko vya jana Mkuranga mpaka muda huu namuhadithia mshua anasema ni kwamba Rais anadanganywa au anadanganya.
Na mzee anasema alivyoona zile pambio akajua kuna michezo sio bure.
USHAURI:
Kwa hali tuliyoiona kiukweli Rais wangu hiyo sera tuitupie mbali hatuiwezi labda ajae lakini sisi hatuwezi tusha prove failure pakubwa sana sasa turudishe sera za mtoto wa mkulima (Pinda).
Maana huko ndio tutakuweza nguvu zote tupeleke huko kiasi kwamba mbegu zipatikane kwa urahisi, mbolea ya ruzuku kwa urahisi, tutafutie wananchi wetu masoko ya nje kwa timu maalum hili tutaliweza vizuri sio la viwanda.
Viwanda (hatuviwezi kwa sasa hatukuwa na mkakati mzuri labda aandaliwe Rais ajae nae ashaurike ili afikie malengo).
Sent using Jamii Forums mobile app