Rais Magufuli: Sitaongeza mishahara kwa Watumishi wa Umma mpaka uzalishaji uongezeke

Yaani huyu Bunge lingekua na watu wenye Akili basi lingempigia kura ya kuto kua na imani nae, haiwezekani nchi inaendeshwa na mtu muongo na bado anachekewa chekewa tu
Anakuwa na ujasiri wa kutopigiwa kura kwa sababu bunge limejaa wachumia tumbo wa CCM. Na anakuwa na uhakika zaidi kwa sababu TUCTA inaongozwa na makada wa CCM jambo ambalo linaifanya TUCTA kuwa kitengo cha CCM kama ilivyo UVCCM au jumuiya ya wazazi.
 
katika hili namuunga mkono MH MAGU 100% wafanyakazi wa serikali mlizoea kupiga soga sana pasipo kuproduce.. Watanzania tujifunze pia katika hili, kazi sio charity organization hapana kazi ni sehemu ya uzalishaji inayohitaji kuona faida mwisho wa siku ili biashara husika ijiendeshe na tuweze pia kukulipa mshahara na kulipa wengine na kukuza biashara pia ili tuajiri wengine,,,,
Makusanyo ya TRA yameongezeka mara 3 zaidi. Hii sio productivity?
 
Anakuwa na ujasiri wa kutopigiwa kura kwa sababu bunge limejaa wachumia tumbo wa CCM. Na anakuwa na uhakika zaidi kwa sababu TUCTA inaongozwa na makada wa CCM jambo ambalo linaifanya TUCTA kuwa kitengo cha CCM kama ilivyo UVCCM au jumuiya ya wazazi.
Exactly
 
dunia nzima utumishi wa umma una maslahi kidogo kuliko sekta binafsi, uzalendo ni kwa kila mwananchi awe ameajiriwa, kajiajiri au hana ajira. tatzizo ni pale unapofananisha committment za mwajiri na uzalendo wakati ni vitu tofauti. it is a two way traffic. serikali inalazimika kama mwajiri kuwa committed kwa watumishi wake kwa kuwapatia rasilimali fedha na watu kwa kiwango kinachostahiki ili kuongeza tija. huwezi kudai kuliko unachotoa. ni mara ngapi uongozi wa serikali unaahidi bado hautekelezi kwa watumishi wa umma! weka suala la mishahara mbali, kila mara fedha na vifaa vinachelewa, vinakuja kidogo au haviji kabisa. huo ndio mzizi wa hoja yangu.

private sector mwajiri akimuahidi mwajiriwa wake anatimiza kwasababu anajua asipofanya hivyo faida itashuka au atapata hasara which is contrary to government leadership. JAZWA UJAZWE

Mkuu nashukuru sana kwa kulitazama hili kimapama zaidi, Ulichoandika kimeonyesha ukomavu wako katika kujadiliana..

Bosi wa hawa wafanyakazi ni Serikali, na Bosi mkubwa sana ni Rais. Bosi wao ambaye ni serikali kupitia Rais ametuambia hawa waajiriwa wameonyesha ufanisi duni kwa maana ya Lowa productivity, ukimbuke Rais ana vyanzo vyake vya taarifa na pia ana taasisi zake zinazofanya uchunguzi na kumpa taarifa...

Wafanyakazi wa umma ni jukumu lao sasa nao kupitia vyama vyao kumpinga Rais na kuwaonyesha wananchi kama kilichosemwa na mkuu ni uongo wa mchana na kiwango cha ufanisi wao ni a,b, c, na wanakwama pia maeneo mengine kwa kuwa bosi wao Serikali ameshindwa kuwapa vitendea kazi, Hili wanatakiwa walifanye wazi na watanzania wooote tusikie lakini wakikaa kimya na kulia huko vichocholoni basi kauli ya mkuu itaonekana sahihi tu..
 
Utafika lini uzalishaji na hii ni nchi watu wanahitaji wajikimu kimaisha na uchumi, hii si familiya ya MTU mmoja ya kusema Leo sitoi huku wala kile. Jaman TUJITAMBUE
 
Faida itaongezeka wapi wakati madeni nayo yanazidi kutuumiza? Bombadier, Konoike nk, hiyo faida itatoka wapi? msituchanganye bana!
 
'To every action there is an equal and opposite reaction'

Rais Dr Magufuli tafadhali sikiliza kilio cha watumishi wa umma kuhusu masilahi yao ambayo yako kisheria.

Huwezi kupata maziwa mengi na bora kutoka kwa ng'ombe ambaye hapewi chakula vizuri na mmiliki wake.

Huwezi kupata mayai kutoka kwa kuku wa mayai kama huwapi chakula bora cha kuzalisha mayai

Wizara na idara ya utumishi jitahidi kuhakikisha maslahi ya watumishi yanapatikana kwa wakati ili watumishi watulie kiakili na kuongeza uzalishaji na kuboresha huduma za jamii kama elimu, afya nk.

Watumishi wa umma kwa sasa wanatumia akili na muda kutafuta kipato cha ziada ili kuweza kumudu hali ya maisha ktk familia yake, hivyo inapunguza uzalishaji na hata kiwango cha utoaji wa huduma kinapungua.

Na ikichanganya na gap la wafanyakazi waliofukuzwa kwa vyeti feki ndiyo shida inakuwa kubwa zaidi.
 
Hivi wale mliosupport kuwa watumishi wasiongezewe na sahivi Ze Mchongoko amekanusha mko upande upo na nyie mnakanusha?
 
Na kama hawataki kujiongeza waache hiyo kazi waje huku kwetu mtaani alafu waone baada ya miezi miwili kama hatukutani nao wana maroba wanaokota makopo.
Hii inaitwa roho mbaya.wakiongezewa mshahara wewe unapungukiwa na nini na je kwa miaka ambayo watumishi hawajaongezewa mshahara umepata unafuu gani? Umepata ajira? Au eameajiliwa wangapi?
 
Mheshimiwa Rais ameyaongea hayo katika mkutano mkuu was 33 wa ALAT jijini Dar es Salaam.

Kwa hiyo wafanyakazi jipeni moyo, msubiri mpaka uchumi utakapokua japo haijulikani ni lini uchumi utakua.
(sio


Maswali magumu:
MBUKENI
=>Uchumi/ uzalishaji unatakiwa ufikie kiwango gani ili mishahara iongezwe?

=>Ni nchi gani yenye uchumi mkubwa na ikajiona ina uchumi mkubwa kisha kuridhika?

=>Je, ahadi alizo ahidi zilikiwa za uwongo kuwa akiwaondoa watumishi hewa na wenye vyeti feki ataongeza mishahara?

Inawezekana mheshimiwa Rais ana lengo jema ila siku zote UONGO NA UKWELI VYOTE VIWILI HAVIWEZI KUTOKA KWENYE KINYWA KIMOJA, NA IKITOKEA NI WAZI HATA UKWELI ULIOTOLEWA UNATAKIWA UTILIWE MASHAKA.



KUMBUKENI kuwa kupandishiwa mishahara sio lazima.. MUHUMU mshahara wako tuliokubaliana wakati nakuajiri....kama uchumi sio poa NUKULIPA mshahara wako TULIOKUBALIAN ...KAMA uchumi huko poa naweza kukupandishia mshahara NA SIO LAZIMA
 
Back
Top Bottom