Rais Magufuli,sema neno moja tu na lugha yetu ipone

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Rais ni mamlaka ya juu kabisa hapa Tanzania. Rais,kikatiba,ni mwenye nguvu kubwa. Rais akisema,nchi husikiliza na kutekeleza. Rais si wa mchezo. Anaweza kusemea chochote,muda wowote na popote.

Umefika wakati wa kutumia Kiswahili. Umefika wakati,kuachana na matumizi ya kiingereza na lugha nyinginezo za kimataifa katika shughuli za kiserikali. Kiswahili kitumike kwenye kuhutubu na kuendesha mikutano. Popote pale. Wakati wote.

Pamoja na kusheheni wasomi na wazungumza kiingereza mahiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam-CKD kimeamua jambo. Baraza la chuo limeamua kuwa mikutano yake yote iwe kwa kiswahili. Vikao vyote. Kiswahili tu. CKD wameonesha njia.

Rais sema. Rais amua. Tuseme na kuandika kwa lugha yetu. Wakalimani wakihitajika watatumika. Muda ni huu. Yatosha sasa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom