barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,874
Tanzania Airport Authority ni "JIPU TAMBAZI" tumkumbushe JPM atembeleee huko TAA makao Makuu na pale JNIA(Julius Nyerere Int'nal Airport).Huo mgahawa ni wa mchina,ni mama wa Kichina ambaye anaelezwa kuwa ana "mahusiano" na mmoja wa vigogo wa TAA.Eneo ulipojengwa Mgahawa ni eneo la maandishi ya "NO PARKING" na lilifaa kuwa moja ya "escape" ya tishio la moto au shambulio la ghafla la "ugaidi" lakini kapewa Mchina na kwa mkataba wa miaka mitano.Hakuna watu wa Mazingira wala wa Civil Engineering waliohusishwa zaidi ya kuona jengo likiibuka kama uyoga wakati eneo hilo maalumu kwa abiria wanaoondoka na wanaosafari.JPM au Mbarawa fika uombe mkataba wa huo mgahawa "fake"
Zaidi ya hapo tembelea eneo la "International Departure" kule juu,watu wamegawiana vibanda vya biashara mpaka wanakaba "lounge",kila mtu akija na "kimemo" basi anapewa eneo na kujenga "kaduka" kake,imekuwa sasa sio "Lounge" ila ni soko kama K'koo,hakuna utaratibu kama viwanja vingine unakuta "Duty Free Shops" zinazoeleweka
Hapo TAA kuna malalamiko na majipu mengi sana,Juzi Waziri Masauni kaishia "kutumbua" majipu ya askari polisi na askari wa Zimamoto wanaoiba mafuta ya ndege na kuuza mtaani,lkn kwanini mmeacha Management ya TAA ambayo imesababisha uwanja huo na mamlaka hiyo kuoza??Ukiacha huo uongozi mpya wa kiwanja uliowekwa wakati wa Utawala wa JPM wa JNIA na TAA-HQ...chinu ya hao wapya kuna uwozo mwingi sana,kama hautarekebishwa basi hata hao waliowekwa wapya hawataweza kuleta "changes" za aina yoyote.
Kuna malalamiko ya Mkurugenzi wa Rasimali Watu,huyo anasemwa kuweka watu wake kiundugu wa kugawa vyeo na madaraka kwa "watu wake",kapachika ndugu yake Meneja Security wakati kuna wengine wengi tu wenye vigezo lkn anapiga chini,wakati anabania wengine kwenda kusoma au kusomeshwa na mamlaka kama ambavyo wamejiwekea ktk utaratibu wa "Human Resource Training and Development",huyo ndugu yake alimpeleka shule India kwa pesa ya mamlaka na kurudi "kumtundika" cheo.Kitengo kingine kaweka hawala yake na kabla ya mkwara wa JPM jamaa alikuwa anampa safari za nje sizizo na mbele wala nyuma.Mbarawa huko TAA mbona hutembelei utumbue haya majipu??Hii tunakupa ni kama "Hints" tu,lkn tumia Usalama wa Taifa walio hapo Kiwanjani wakupe uozo wa hapo,wasipokupa sisi tutakufikishia tu.
Jengo la VIP Lounge ni "Jipu" jingine la TAA,pale kila wanaopita VIP wanalipa kwa dola,waliowekwa kupokea pesa za watumiaji wa VIP kwa cash na hundi ni watoto wa "Vigogo" wa TAA,tembelea upewe mapato na matumizi ya VIP,watoto wao wamekula hela ya mapato ya VIP na bado wapo kazini.Hela imeliwa ila sbb waliokula ni watoto wao issue inazimwa kimyakimya,tembelea hapo na upewe majina ya waliofanya kama wakusanyaji mapato VIP utajionea majina ya watoto wao ndio utaamini.VIP ulikuwa ni mradi wa watu na wamekula sana pesa pale bila risiti
Kuna ile kampuni ya "PORTERS",ule ni mradi wa watu pale JNIA,kila "Porter" anatakiwa kukusanya kiasi cha pesa na kumpatia "Supervisor" kwa siku,na pesa ile ina mlolongo wa watu kugawana.Jiridhishe kuwa kampuni ya "Porter" huwa inashinda "tender" kiharali au ni mradi wa watu wa TAA,uhakika ni kuwa utapata jibu na kujua "Jipu" lilipo.Wale Porter ndio wanatumika kupitisha mizigo ya magendo kwa wafanyabiashara wasio waaaminifu.Mtu akishuka na mzigo anauwacha na porter anaubeba huku akila sahani moja na mtu wa custom na wale Polisi,ule ni mtandao mkubwa wa kukwepa kodi na kupitisha mizigo kimagendo.Kama watu wenu wa usalama wapo makini watwapa ripoti hii,maana sisi wapita njia tu tunajuwa hii michezo vipi vyombo vya usalama??
Uhamiaji ndio kama kawaida,wanapitisha raia wa kigeni kwa rushwa wakati hawana hata "Invatation letter",ndege ya Ethiopia ya usiku ndio inatumika sana maana pale serikali inakuwa "imelala".
Tupia jicho wafanyakazi hewa,wafanyakazi wa muda "temporary workers" ambao wanazidi "parmanent workers".Hawaombi vibali vya ajira ili kuwa na kigezo cha uhaba wa ajira na kuajiri ndugu zao kama wafanyakazi wa muda.Mpaka waliposikia mkwara wa JPM wakawaondoa wachache ambao hawakuwa na "Godfather" na kukatisha ajira zao,sasa HR wa JNIA ana kesi Mahakamani kwa kuwaweka watu kama wafanyakazi wa muda kwa kipindi kirefu halafu wanakuja kuwaondoa kienyeji
Pale TAA/JNIA kuna uwozo mwingi,ili hao Wakurugenzi wapya wa TAA na JNIA wafanye kazi kwa kasi ya serikali yako,lazima majipu chini yao yatumbuliwe,week iliyopita Naibu Waziri Masauni tulimuona akitumbua majipu ya askari polisi na askari wa Zimamoto ambao ni "wezi" wa mafuta ya ndege,lkn akaacha mzizi wa wizi na wezi wakubwa