Rais Magufuli pitia upya mkataba wa KQ na Tanzania

Wanavyo laumu na kubeza hiyo mikataba utadhani ilipitishwa na chama cha upinzani
Inamaana miaka yote mitano alikuwa anafanya nini? Kwenye mikutano hakwenda hivyo alikuwa na muda wa kutosha kabisa
 
Mkuu upo sahihi sana, lkn sidhani kama kuwabeza viongozi waliopita sidhani kama upo sahihi.

Kumbuka hao viongozi walikuwa ni viongozi wetu kama tulio nao sasa hivi na kingine kikubwa ni kuwa wote wanakitumikia ccm.
Hapo ndo namkubaligi Magufuli. Hawa Wakenya wapuuzi sana. Wanadhani Tanzania ya sasa ni ile ya Mzee Mwinyi. Wakae wakijua wakimwaga ugali saa tatu asubuhi sisi huku saa tatu na dakika tano tunamwaga mboga na meza tunavunja kila mtu alale njaa.

Wajinga sana na ikiwezekana hivi vigari vyao vinavyobeba vitunguu na mahindi vipigwe pini hukohuko mpakani. Kwani stail yetu ya kuishi na corona kishkaji inawaumiza nini? Sisi tumeimudu wao waendelee kuhesabiana wagonjwa tu.
 
Hahaha Magufuli huwa mnamnanga lkn linapokuja swala la kazi na utendaji ninyi wenyewe ndani ya nafsi zenu mnajua kabisa kwamba ndiye pekee anayeweza kutenda na kutekeleza kwa vitendo kupigania maslahi ya Tanzania yetu, hao wengine ni wasanii tu, ...

Chagua Magufuli kwa Afya na Ustawi wa Taifa letu, Magu tena 2020/35!
Umeanza.
 
Chagua Tundu Lissu kwa maendeleo ya taifa letu la Tanzania ili ufurahie uhuru wako kulingana na matakwa ya katiba.
Hahaha Magufuli huwa mnamnanga lkn linapokuja swala la kazi na utendaji ninyi wenyewe ndani ya nafsi zenu mnajua kabisa kwamba ndiye pekee anayeweza kutenda na kutekeleza kwa vitendo kupigania maslahi ya Tanzania yetu, hao wengine ni wasanii tu, ...

Chagua Magufuli kwa Afya na Ustawi wa Taifa letu, Magu tena 2020/35!
 
Kawashauri wapuuzi wenzako
Linapokuja swala la kitaifa inabidi tuweke tofauti zetu pembeni. Uzalendo ni pamoja na kukosa pale unapoona serikalu inaenda sivyo na kuunga mkono pale wanapofanya vizuri na sio kupinga bila sababu au kuunga mkono upuuzi.

Inabidi kenya walete ndega kama ilivyokubaliwa
 
Nadhani badala ya kuhangaika na wakenya,tungeelekeza nguvu zetu kuaddress ujinga unaowakabili watanzania ili waweze kucompete,haya mengine we are just wasting our time
Hilo ndiyo suluhisho sahihi
 
Lkn watanzania hao hao wenye mawazo tofauti na nyinyi kisiasa wanatandikwa virungu na wengine kuburuzwa mahakamani mnashangilia!

Mnapo pata matatizo ndiyo mnaona umuhimu wa taifa kuwa kitu kimoja?

Badilikeni basi maana mnaonekana mnapenda kusaidiwa wakati wa shida ili muwaone hata wapinzani nao ni watanzania na wanastahili haki kwenye nchi yao.
Huo ndiyo ukweli were suppose to be proud TANZANIA ni yetu wenyewe
 
Wewe ni Mpuuzi

Kumewasaidia nini hao Wakenya kwa kuangalia Katiba yao...!!!!

Chief
Hali ya Wakenya ni mbaya kuliko maelezo.
Wanaofaidi Nchi ni hao Wasomi wao unaowasifia......

Kuna wakati,ukitaka kufanya jambo muhimu,ni lazima upasue Mlima

Haijalishi.......
"SiSI" kwa sababu watanzania wote ni waoga. Haiwezekan katiba mara kibao inavurugwa na sisi wananchi tumekaa tu kimya. Kenya huo upuuz haupo. Sisi hadi mahakama inaingiliwa lakin tupo kimya kama mtungi wa maji. Mtu mmoja anaongoza nchi kama familia yake tupo tuu. Alaf unataka niseme ni mm na sio sisi.
 
Issue ya kupitia mkataba wala haipaswi kufika kwa Rais. Kama terms kwa mfano zinasema KQ wafanye trips 14 kwa week then wao wanakuja mara 20, kuna mtu junior kabisa kwenye airports zetu anapaswa kuraise hili na likafanyiwa kazi kwa level za chini.

Ni bahati mbaya sana tumefika mahali hata kujenga vyoo vya stand au kukarabati gari mpaka Rais wa Nchi afike kutoa maelekezo
 
Mnavyo tupiga virungu na kutumwagia maji ya washa washa mnakuwa hamjui kuwa kama taifa tunahitaji umoja?
Subiri tumalize kazi ya kuitetea Tanzania kwanza ndio uje na hizi hoja zako.

Tanzania ni zaidi ya kila kitu na kila mtu.
 
Back
Top Bottom