Rais Magufuli, ongoza nchi hii mpaka tutakapopata wapinzani makini

Gluk

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,856
2,953
Habari zenu wanajukwaa. Wakati tukiendelea kuomboleza kifo cha mpendwa wetu Ruge naomba nichukue nafasi hii kueleza hili.

Kitendo cha Lowasa kujiunga CHADEMA na kupewa nafasi ya kugombea urais sikukiunga mkono, na si Lowasa pekee ila pia kitendo cha mtu anayetoka chama fulani na kujiunga na CHADEMA kupewa nafasi ya kugombea nafasi ya ubunge na kuwanyima fursa waliomwaga jasho na damu kukipigania chama pia sikikubali.

Wenyewe mtakuwa mashahidi kuwa kuna watu wengi tuliwaamini na kuwakaribisha CHADEMA ila wakasaliti chama mifano ni mingi sana.

Ni ajabu sana kumuacha mtu aliyekipigania chama na kumsimamisha mgeni tena aliyekataliwa na upande fulani kana kwamba chama hakina watu wenye sifa za kugombea.

Kwa upinzani huu ninaouona kwa sasa sioni upinzani wa kuiondoa CCM madarakani labda vizazi vingine ila sio hawa viongozi tulio nao maana hawajaonyesha nia ya kutaka kushika dola.

Nahitimisha kwa kusema kwamba mh rais ndugu JOHN JOSEPH POMBE MAGUFURI ongoza nchi na ikiwezekana 2020 ufanyike uchaguzi wa wabunge pekee ili tusipoteze pesa za walipa kodi bure, ili pindi upinzani ukiimarika nchini na wapinzani tukawa tiyari kuchukua nchi ndo ufanyike uchaguzi wa urais.
Asanteni sana


MAENDELEO HAYANA CHAMA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom