maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Ni nadra sana kwa aina ya viongozi tulionao barani Afrika kumpata kiongozi akiyatamka maneno mazito kama haya mbele ya wasaidizi wake wa ngazi za juu na hata kuthubutu kuwaambia mawaziri wake kuwa kama kuna waliozoea chai chai, posho posho na safari za ovyo ovyo wampishe.
Kikubwa na kinachotutia moyo wananchi ni ile hulka yake kuonyesha kutotania kwa jambo lolote serious analoongea. Kwa mfano katika hili ilionekana dhahiri kwamba anachokisema kinatoka ndani ya dhamira ya moyo wake, hasemi kutufurahisha.
Tulizoea huko nyuma kumwona Rais akishindwa kumkemea hata waziri, naibu waziri ama hata DC aliyemteua yeye mwenyewe kwa visingizio vya kijinga.
Watanzania tuendelee kumwombea Rais wetu tusiwe na shaka atatuvusha, hatutapigishwa tena maktaimu kama ilivyokuwa miaka 10 iliyopita.