Rais Magufuli, ni wakati muafaka "Ikulu" irudishwe kwa wenyewe, Waislam

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,894
109,227
Mheshimiwa Rais Magufuli, Asalaam Alaikum (Salama na Amani iwe juu yako).

Tunafahamu kuwa wewe ni Rais wa wanyonge na ni mpenda haki usiyependa yeyote adhulumiwe.

Sisi Waislam, mkoloni Mjerumani alitudhulumu majengo yetu mengi hapo jijini Dar Es Salaam, jina ambalo limetokana na jengo ambalo sasa linaitwa "Ikulu". Majengo hayo ni pamoja na jengo la Dar us Salaam ambalo ndilo ikulu ya sasa, hospitali inayojulikana kama "Ocean Road" pamoja majengo ambayo yalibadilishwa na kufanywa makanisa katika ufukwe wa Bahari ya Hindi ulio jijini Dar Es Salaam.

Kwa kuwa sasa unahamia rasmi Dodoma basi tunaomba haki itendeke na jengo hilo au majengo na viwanja vinavyozunguka majengo hayo yarudishwe kwa wenyewe ili haki itendeke.

Naomba ujisikilizie mwenyewe ushahidi huu hapa, nauweka chini, wa mali hizo kuwa si za wengine bali za Waislam waliodhulumiwa.

Pia tunaomba mali hizo zisikikabidhiwe Bakwata kwani wana koo za waliojenga na wenye kumiliki ardhi hizo, kabla hazijadhulumiwa, wapo hai na wakabidhiwe wao haki zao.

Natumai kilio na ombi hili la kutafuta haki zilizodhulumiwa kitakufikia nawe utatenda haki ya msingi ya kurudisha mali za waliodhulumiwa.

Ahsante.

 
Tuache udini kila mtu akianza kudai alichonyang'anywa uko nyuma 75% ya vitu vya serikali vitarudishwa kwa wenye navyo. mashule ya wakiristo, hospital vingapi vilitaifishwa kipindi kile?

Tufanye siasa lakini uko tunakoelekea siko!

Makonda tu aliwapa pesa zake za msikiti kama sikosei mjenge Makao Makuu ya Bakwata.

Hata ukirudishiwa utapata faida gani na Majengo? jamani dini zisitufanye tuwe na chuki na serikali tulete hoja zenye tija kwa umma bila kujari dini.

Basi tukitoka hapo tutasema waislam wasitumie reli maana ilijengwa na Mjerumani jamani?

Kuna Watoto waislam wanasoma kwenye shule zilikuwa za mission mpaka leo zinamilikiwa na serikali so serikali izirudishe kwa kanisa?

Hakuna kitu nachukia kama udini, ukabila na uchama.
 
Mbona wanadhulumu pensheni za wastaafu, mishahara na nyingeza za mishahara ya wafanyakazi, wanateka wananchi, wanaua, wamewashilikia mashehe magerezani bila hatia, nk.

FaizaFoxy zipo dhulma nyingi sana zinazofanywa na awamu hii, wewe umeona msikiti tu?

Wameshindwa kuacha dhulma hata za kawaida kabisa eti waje waachie msikiti?

Pole sana
 
Warudishiwe Waislamu au Waarabu? Kwa maana nafikiri kuna tofauti hapo, kati ya Uislamu na Uarabu, isitoshe kama ni hivyo Waarabu pia hapa siyo kwao, warudishe pia ardhi ya mtu mweusi.

Mambo mengine ni kuacha tu, mkiamua kufukunyua hakuna mwisho.
Misikiti na taasisi za elimu za Kiislam huwa ni za Waislam. Kajifunze maana ya "waqf".
 
Kuzungumzia Mambo ya dini kwenye Dunia ya sasa inaonyesha jinsi Gani mwafrika alivyo duni kifkra

Mabeberu wangekuwa wanawaza km mwafrika dunia isingeendelea kabisa

Unataka ikulu leo,kesho utasema Tunataka bahari ni ya waislamu

Kesho wacatholic watasema Tunataka shule zetu

Tuache mawazo ya kijima
 
Back
Top Bottom