Rais Magufuli ni Nyerere wa pili

Tangu aondoke Mwalim Julius Kambarage Nyerere watanzania wabaki wanyonge sana.

Misingi aliyoiacha Nyerere ilikosa mtu wa kuiendeleza na kuisimamia ipasavyo.

Zilibaki ngonjera tu. Asante Mungu kutuletea hiki kisu, kifaa cha ukweli Daktari wa falsafa John Pombe Joseph mtoto wa Magufuli. Umevaa viatu vya Nyerere na vimeku fit ipasavyo. Endelea hivyo hivyo.
acha kumfananisha Nyerere na vitu vya ajabu ajabu.Nyerere alikufa na misingi yake. c huyu mkaburu mweusi
 
Misingi ya Nyerere mbona ilikufa na yeye yupo hai?

Kabla ya kung'atuka kwake tulikuwa hata chakula hatuna, kila kitu foleni. Mabarabara hayapitiki. Ukitaka kwenda Mwanza au Kagera ni lazima upitie Kenya kwanza.

Hivi ulikuwepo wakati huo wa foleni za chakula?
Mkuu wapo watu wanamsikia Nyerere kwa propaganda,lakini kwa wale waliomuona Nyerere akiwa raisi,tunapicha nyingine tofauti kabisa.
Mwl hakuwa tiyari kukosolewa wala kushauliwa.
Tanzania ilizama wakati hakiwa raisi.
 
nyerere ni ccm tu na alituachia hili dude ccm lakini at least hakuwa mwizi wa nyumba za serikali,hakuiba kwenye barabara na wala hakunnua kivuko kibovu kwa mabilioni....acha kumfananisha nyerere(pamoja na upuuzi wake) na mambo ya kijinga na ya kipuuzi kupindukia.
 
Tangu aondoke Mwalim Julius Kambarage Nyerere watanzania wabaki wanyonge sana.

Misingi aliyoiacha Nyerere ilikosa mtu wa kuiendeleza na kuisimamia ipasavyo.

Zilibaki ngonjera tu. Asante Mungu kutuletea hiki kisu, kifaa cha ukweli Daktari wa falsafa John Pombe Joseph mtoto wa Magufuli. Umevaa viatu vya Nyerere na vimeku fit ipasavyo. Endelea hivyo hivyo.
Nyerere hajawahi kufanya biashara ikulu. Swali moja tu nakupa na ukijibu najitoa JF na swali lenyewe lipo hivi; ile zabuni ya kununua ndege chakavu za Bomba mapenzi ilitangazwa wapi? Wakati ukifikiria kujibu hili nakupa "home work" ukatafute jibu magogoni kama ifuatavyo; zile zabuni za kujenga barabara ya morocco - mwenge, uwanja wa ndege wa chato, na ofisi ya TRA chato zilitangazwa wapi? Ukishindwa kujibu haya basi kuna siku atajibu huyo unayemfananisha na nyerere
 
Kuweni na subra amalize utawala wake uje uskilizie vioja na vimbwanga tusivyovijua
 
Tangu aondoke Mwalim Julius Kambarage Nyerere watanzania wabaki wanyonge sana.

Misingi aliyoiacha Nyerere ilikosa mtu wa kuiendeleza na kuisimamia ipasavyo.

Zilibaki ngonjera tu. Asante Mungu kutuletea hiki kisu, kifaa cha ukweli Daktari wa falsafa John Pombe Joseph mtoto wa Magufuli. Umevaa viatu vya Nyerere na vimeku fit ipasavyo. Endelea hivyo hivyo.
Acha masihara. Nyerere ni mashine nyingine. JPM hawezi hata kumsogelea!!
 
Tangu aondoke Mwalim Julius Kambarage Nyerere watanzania wabaki wanyonge sana.

Misingi aliyoiacha Nyerere ilikosa mtu wa kuiendeleza na kuisimamia ipasavyo.

Zilibaki ngonjera tu. Asante Mungu kutuletea hiki kisu, kifaa cha ukweli Daktari wa falsafa John Pombe Joseph mtoto wa Magufuli. Umevaa viatu vya Nyerere na vimeku fit ipasavyo. Endelea hivyo hivyo.
Bwege wewe! Tena si Bure utakuwa umetumwa! Nyerere wa hivi?? Lol
 
Huwezi mlinganisha Nyerere na wezi huyu mtu ana historia ya wizi rejea nyumba za serikali alizojenga mwalimu kuvunja katiba na sheria za nchi anatumia fedha ya umma yeye na mpwawe kununua vivuko MV Dar mbovu nakuwasakizia jeshi kukurupuka kwenye maamuzi kusababisha serikali ilipe mbilioni ya samaki kujipendelea kwa majengo uwanja chato majumba chato Nyerere alijengewa na jeshi Magufuli mkabila mbaguzi hana heshima kwa wananchi wake hana level yeyote ya Nyerere
 
Nia ya Mwalimu ni maisha bora ya kijamaa kwa Watanzania. Sema utekelezaji mbovu, hakua na makuu, ufisadi kwake sumu. Nae JPM ana sifa hizo ndio maana anamlinganisha nae. Kila mara anasema kutoka moyono anaipenda Tz, kwa mtu asiyeona juhudi zake ana lake jambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu aondoke Mwalim Julius Kambarage Nyerere watanzania wabaki wanyonge sana.

Misingi aliyoiacha Nyerere ilikosa mtu wa kuiendeleza na kuisimamia ipasavyo.

Zilibaki ngonjera tu. Asante Mungu kutuletea hiki kisu, kifaa cha ukweli Daktari wa falsafa John Pombe Joseph mtoto wa Magufuli. Umevaa viatu vya Nyerere na vimeku fit ipasavyo. Endelea hivyo hivyo.
I know what you mean mkuu.But to me he is not a "Nyerere reincanate," but rather a different and a better being called John Joseph Pombe Magufuli.
 
Misingi ya Nyerere mbona ilikufa na yeye yupo hai?

Kabla ya kung'atuka kwake tulikuwa hata chakula hatuna, kila kitu foleni. Mabarabara hayapitiki. Ukitaka kwenda Mwanza au Kagera ni lazima upitie Kenya kwanza.

Hivi ulikuwepo wakati huo wa foleni za chakula?
.

Kati ya maeneo machache ninayotofautiana na wew dada yangu Faiza ni chuki yako kwa Nyerere,sijui alikukosea kipi.Sishangai sana kwa kuwa pia u mtu wa visasi.Nitakuuliza,hivi Nyerere angekuwa hovyo kiasi hicho wale unaowapenda upeo upande wa elimu mngesogea kiwango alichowasogeza Mwalimu? Ugomvi wa ukabila na udini ungekuwa hafifu kiasi hiki tulicho nacho?

Kama Nyerere alikuwa dhaifu hivyo na JPM ni dhaifu zaidi,kwa tunaoamini kuwa Nyerere alifanya mema mengi licha ya mapungufu yake tunamwona JPM akimsogelea.JPM hafiki hata robo ya uzungumzaji si wa Mwalim tu bali hata wa Mzee Mwinyi,Mkapa wala Jakaya.Hao watatu kwa pamoja hawafikii hata robo ya utendaji wa JPM katika eneo la kudhibiti rushwa,nidhamu ya watumishi na kuheshimu wasio nacho.Peke yake JPM baada ya Nyerere ameweza kuwaambia ngozi nyeupe Tanzania ina wenye nayo nao wakaelewa japo kwa hasira na maumivu makubwa.Nani mwingine kafanya hivyo.

Kama suala ni udini BWM ni mkristo,hatumfumbii midomo kwa kuuza viwanda vyote alivyovikuta,kuuza hata benki iliyokuwa inaendeshwa kwa faida kubwa.Imani zetu kwa nini zitufarakanishe?
 
Back
Top Bottom