Rais Magufuli ni Nyerere na Nkrumah mpya

Rais Magufuli ni Nyerere na Nkrumah mpya

hugochavez

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2013
Posts
1,907
Reaction score
1,009


Aeleza ukweli kwamba Africa ina rasilimali za kutosha kujitegemea. Akemea ufisadi kwa vitendo na kusema ndio sababu kubwa ya umaskini wa Africa. Asema katika kipindi chake atahakikisha Tanzania inapiga hatua na inaondokana utegemezi kutoka kwa wafadhili. msikilize hapo juu.
 
Aeleza ukweli kwamba Africa ina rasilimali za kutosha kujitegemea. Akemea ufisadi kwa vitendo na kusema ndio sababu kubwa ya umaskini wa Africa. Asema katika kipindi chake atahakikisha Tanzania inapiga hatua na inaondokana utegemezi kutoka kwa wafadhili. msikilize hapo Chini kwenye video clip.

Arudishe fedha za wastaafu
 
Rais Magufuli ameyasema hayo kwa hisia na kueleza kuwa umaskini wa Afrika unasababishwa na migogoro inayotengenezwa na Nchi wafadhili na hivyo jawabu pekee ni kungana kwa pamoja na kupiga vita aina zote za ubeberu. pia ameeleza kuwa Bara la Afrika lina rasilimali zote muhimu ikiwamo madini, ardhi safi na yenye rutuba na vivutio kibao lakini imeshindwa kunufaika navyo. Amesema rasilimali zetu zimewanufaisha zaidi mataifa ya nje badala ya Afrika yenyewe.
Mawazo na fikra za Magufuli zinaendana na zile za wapigania uhuru wa Nchi za Afrika akiwemo Samora michael, Nkrumah, Nyerere na wengineo wengi bila kumsahau Kanal Muammar Gadafi aliyedhulumiwa uhai wake kutokana na misimamo yake ya kutaka kuikomboa Afrika kutoka kwny dimbwi la umaskini. Tazama video
 
Nyerere alifahamu vyema kuongea kiingereza, ila huyu anakwepa sana makongamano na marais wenzie kwa kuhofia kuvuruga lugha ya malikia. CCM ni janga la kitaifa
kuabudu kiingereza ni ukoloni wa kifikra. badilika. tukuza vyako. china inaongea kichina na wamefanikiwa
 
Raslimali bila ujuzi na elimu ni kazi bure.
Venezuela wana mafuta mengi sana lakini leo theluthi ya raia wake wamekimbia nchi yao kutokana na umaskini uliokithiri.
Raslimali za Tanzania zinatusaidia nini wakati bajeti ni trillion 33 makusanyo ya TRA ni wastani wa trillion 17.5?
 
Sasa anayesainisha mikataba ya kuwaruhusu hao wanyonyaji ni nani kwani
 
Africa kamwe haiwezi ungana,sababu kuu ni tuna tamaduni tofauti,tunaongea lugha tofauti,viongozi walafi.
 
Back
Top Bottom