SONGOKA
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 1,841
- 1,843
Duniani kuna michezo ya aina nyingi sana, na kwa kulitambua hili wenzetu wamewekeza pesa nyingi katika michezo kwa sababu huko ndo ajira kwa vijana zinaweza kupatikana kwa wingi.
Rais Magufuli hajui kama POOL ni mchezo kama ilivyo football, basket ball na kadharika na ili uwe mchezaji nguli lazima ufanye mazoezi ya kutosha, na kupata muda wa kutosha kujinoa.
Lakini rais Magufuli hajui kama kuna chama duniani cha mchezo wa pool kinachoitwa World Pool and Billiards Association kinachosimamia michezo ya pool duniani na kuandaa mashindano ya dunia.
Rais Magufuli hajui kuwa Africa ina chama pia cha mchezo huo kinachoitwa, All African Pool Association na kina nchi wajumbe 14 Tanzania ikiwemo, nchi ambayo anaiongoza.
Rais Magufuli hajui kuwa katika mashindano ya pool ya dunia mshindi hulipwa dola 300,000 ambayo ni Tsh 600,000,000 ya kitanzania, lakini washindi wa stage mbalimbali pia hulipwa kuanzia dola 10,000 hadi 100,000. na mashindano haya hufanyika kila mwaka
Lakini kuna mashindano mengi tu ya kikanda na kibara ambayo pia huingiza pesa nyingi tu kwa wachezaji, mbali na ufadhili mbalimbali wa makampuni ya michezo. Lakini pia hapa Tanzania kuna mashindano ya kitaifa na yanadhaminiwa na SAFARI LAGER na kupitia haya mashindano vijana wamekuwa wakipata kipato cha kujikimu.
Nilitegemea kwa takwimu hizi chache, Rais angewahamasisha wakuu wa mikoa kuanzisha club zinazotambulika za pool ili kuwawezesha hawa vijana kupata fursa hizi badala yake anaamua kuua vipaji.
Alichofanya Magufuli ni sawa na kusema hamna vijana kucheza mpira wakati wa kazi, nilitegemea BMT wamuandikie barua kumuelimisha, nao wamekaa kimyaaa.
Katika dunia nzima ni Tanzania tu ndo tunapiga marufuku michezo, huku mataifa mengine yakibuni kila aina ya mchezo ili kutengeneza ajira.