Rais Magufuli na Uhuru wa Tanzania

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
MAGUFULI NA UHURU WA TANZANIA, MAADUI WA NCHI NI NANI?

Na, Robert Heriel.

Leo ni kumbukizi ya sherehe ya uhuru wa nchi yetu ambapo hapo awali ilifahamika kama Tanganyika kabla ya kuungana na Zanzibar mnamo mwaka 1964.

Hii ni kusema Tanganyika ilipata uhuru wake siku na mwezi kama wa leo mnamo mwaka 1961. Hapo ikatangazwa rasmi kuwa nchi yetu ni huru na haipo chini ya dola la Malkia Elizabeth wa Uingireza.

Ni miaka 58 sasa tokea tupate uhuru. Jitihada mbalimbali zimefanyika kuhakikisha nchi yetu inaenda sawa. Hatuwezi puuzia hatua tuliyofikia.

Lakini pia hatuwezi lemaa wala kulala kwa hatua tuliyofikia. Ni hakika tumejitahidi sana. Lakini haitufanyi kujivuna wala kujisifu kwa hatua hii.

Kila hatua kwetu ni muhimu na kuthaminiwa. Kila mmoja kwa nafasi yake ameweza kuonyesha umuhimu wa mchango wake katika taifa hili. Kila mchango ni muhimu.

Hatuwezi kuwa huru bila maadui. Wala hatuwezi kuwa watumwa pasipo marafiki. Tunatambua uwepo maadui zetu ambao wamekuwa wakizorotesha ustawi wa taifa hili. Lakini sio vyema kupambana na maadui wasiohalisi. Huko sio tuu kupoteza muda Bali pia ni kupoteza nguvu na mapambano. Wengi waliopambana na maadui bandia walishindwa. Sisemi kuwa Magufuli utashindwa Bali najaribu kukushtua kuwa uwe mwangalifu usije ukashindwa katika vita yako. Maadui hatari ni Wale wasiopiga kelele. Kwani Simba mwenda pole ndiye mla nyama.

Tunatambua jitihada za mahasimi wetu waliotuzunguka kila pande kuvuruga umoja na amani ya nchi yetu. Hata hivyo jambo moja muhimi ni kuwa, Tunafurahia tunapokabiliana na adui zetu. Ni sehemu ya kuijenga Historia ya nchi yetu.

Nchi yetu imejipatia heshima za kidunia kutokana na namna tulivyokabiliana na adui zetu. Hatuwezi kusahau mchango wa adui wetu kutufanya tuheshimike mbele ya dunia mara baada ya kuwachakaza vibaya.

Tungewezaje kujua nguvu zetu pasipo na adui. Adui wametufanya tuwe bora zaidi. Tutawamaliza lakini hatutawamaliza wote kabisa.

Tunajua wazi. Bila ya adui hatuwezi kuwa taifa kubwa, imara lenye heshima. Adui ni muhimu ikiwa atatumiwa kwa akili.

Hata hivyo tunaweza kukosa adui halisi. Lakini hilo halitufanyi tushindwe kuweka hata adui bandia. Adui tutamtengeneza ili nchi yetu tuweze kuonyesha ubora wetu.

Tunafahamu kupitia kupambana na adui ndio tunajenga Legacy katika jamii zetu. Bila ya kumuondoa Adui hatuwezi kuweka Historia yenye maana kwa kizazi cha taifa hili.

Adui ni adui hata kama haonekani. Adui ni adui hata kama ni bandia. Jambo kuu hapa ni kuleta uhuru halisi hata kama umepatikana kwenye adui bandia.

Leo ni kumbukizi muhimu kwa kizazi cha Watanzania ambao hapo awali waliitwa Watanganyika. Ni baada ya kumuondoa Adui Mkoloni.

Tunamkumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kuweza kukamilisha zoezi lile la kutupa uhuru bandia naam ndio Uhuru wa bendera.

Adui alikuwa halisi lakini Uhuru ulikuwa bandia. Naam ndio uhuru wa bendera. Wataalamu wanasema uhuru wa Kisiasa.

Hata hivyo Hatuwezi puuzia uhuru wa bandia ikiwa Mwl. Nyerere alidhamiria kuleta uhuru halisi. Hata hivyo Nyerere ambaye kwangu nina mtambua kama Mwanafalsafa wa kwanza katika taifa hili ninayemheshimu kwa kazi zake za mdomo na maandishi.

Yeye mwenyewe aliwahi kusema adui wa taifa hili ni Maradhi, Ujinga na Umasikini. Hao ni maadui halisi wa taifa. Japo hawaonekani lakini tunawaona kupitia maisha ya Watanzania.

Haya niachane na Nyerere. Hata hivyo hayupo. Tuliyenaye ni Rais Magufuli.

Rais Magufuli anapaswa kujua taifa hili bado halipo huru. Najua anajua.

Adui ni muhimu sana. Kupitia adui ndio tunapata maendeleo. Lakini ili umfukuze adui kwenye nchi yako basi lazima ujue pakumpeleka.

Labda sieleweki. Lakini najitahidi kufanya nieleweke.

Adui lazima tujue pakumpeleka kabla hatujaanza kukabiliana naye. Bila kujali aina ya adui.

Adui wa taifa labda tuchukulie mtu msaliti ambaye anaungana na taifa jingine kutupiga katika taifa letu.
Lakini nafahamu kuwa Magufuli anaweza kuwa anajiweka katika vita na maadui bandia huku akiacha maadui Halisi. Hata hivyo Mimi ni kijana Mdogo tuu siwezi jitia ninaakili kuliko Rais, huenda anawafahamu lakini ninayohaki pia ya Kueleza Jambo hili ili kama atasahau akumbuke.

Msaliti WA nchi anayeimbwa kila siku na Magufuli. Huyu baada ya kumtambua sehemu muhimu ya kumpeleka ni kuzimu. Lakini kabla ya kufanya hivyo tunaowajibu wa kumuonya na kuangalia rekodi yake ya nyuma. Isijekuwa amelaghaiwa.

Kama atakubali kosa na kuomba toba basi tunaweza msamehe. Lakini akikaidi. Mahali pekee salama panapo mfaa ni kuzimu. Hii inafanyika mahali pote duniani na kwenye falme za kiroho.

Adui namba mbili ni adui wasioonekana kama MARADHI, UMASIKINI NA UJINGA. Wengine ni KIFO, NJAA N.k.

Adui wa aina hii ili tuwe huru nao ni lazima tujue pa kuwapeleka. Bahari nzuri adui hawa huwezifanya mazungumzo nao kwa sababu hawaonekani kaa macho lakini wapo.

Nchi yetu haipo huru kwa sababu haijui ni wapi pakuwapeleka adui haqa watu. Sijaeleweka najua.

Ipo hivi; Huwezi ufukuza umasikini bila kujua wapi unaupeleka. Umasikini ni adui anayehitaji hifadhi. Maradhi ni adui anayehitaji hifadhi. Halikadhalika na Ujinga.

Taifa makini ni lile linalojua kukabiliana na Adui zake na kujua wapi watawapeleka. Lazima kabla hujapigana na adui yako basi sharti ujue kaburi lake litakuwa wapi. Hii ni kusema kuwa Unachimba kaburi la adui. Ati bado sijaeleweka. Subiri utaelewa tuu.

Watu wenye akili wote wanajua na watakubaliana na mimi kuwa. Umasikini, ujinga na maradhi ambao ni maadui hawataisha dunia mpaka kiama. Hata Yesu alikwisha sema Masikini hawataisha mpaka kurudi kwake. Na watakuwa wengi dunia ingalipo.

Kama taifa halijui pakupeleka umasikini wake litawafanya Raia wake kuwa masikini Lipende lisipende.

Kama Taifa halijui ni wapi litapeleka adui maradhi na Ujinga basi litawafanya Raia wake kuwa wajinga na wenye magonjwa ya hapa na pale.

Wazungu walihangaika na kupambana na Maadui zao. Hata hivi leo wanaendelea kufanya hivyo. Lakini kama nitaulizwa ni mbinu ipi ya akili ambayo wazungu watasifiwa kwa kuwa nchi zilizoendela basi ningejibu nikiwa nime-Relax kuwa; WAZUNGU WALIJUA PAKUWAPELEKA ADUI ZAO.

Wazungu walijua umasikini, maradhi na Ujinga ni adui wabaya kuwahi kutokea. Walichokifanya ni kuwasukumiza maadui hao katika nchi za watu wengine.

Hapo ndipo wakawaleta adui hao huku Afrika ikiwemo nchi yetu ya Tanzania. Sasa naona unaanza kunielewa.

Ni kupitia Kutupa ujinga wa elimu zao ndipo wanapozika ujinga wao. Ni kupitia misaada yao ambayo wanajitia wanatusaidia kuondoa umasikini ndipo wanapozika umasikini wao ili sisi tuwategemee na kuwa watumwa wao.

Nani asiyejua Magonjwa makubwa hapa Afrika yanauswahiba na hao hao wazungu.

Labda nijidanganye lakini ukweli nitabaki nao kuwa ni kupitia madawa yao wanayoyatoa bure au kwa gharama waiitayo nafuu ndio wanamzika adui maradhi katika nchi zetu.

Labda sijaeleweka lakini sina uhakika kama sieleweki.

Mimi sitaki kuelezea masuala ya adui kifo ambapo ni kupitia vita Wazungu wanaweza kukosa kwao vita. Wamezika vita kwao na kuzipeleka katika makaburi waliyoyachimba Afrika na nchi za mashariki ya kati.

Siku zote nazungumzia dini ingawaje Mimi ni Mkristo lakini siwezi kuwa mnafiki nikikana kuwa Ukristo na Kaburi la kunifanya nisiwe huru na Utamaduni wa Uafrika wangu ambao kuna dini zetu nyingi.

Magufuli, Kwa heshima yako kama Jemadari na kiongozi uliyepata bahati kuwa kiongozi wakati mimi nikiwa ninaakili angalau za kuchambua mambo.

Nakushauri, Kwa vile najua unashaurika. Nakupa jumbe hii kwa kuwa najua unania ya kulikomboa taifa hili.

Kama unania ya kuuondoa umasikini katika nchi hii. Basi huna budi kutafuta pa kuupeleka. Huwezi ondoa umasikini bila kujua utaupeleka wapi. Kama utafanya hivyo si ajabu ukazidisha umasikini kwa raia wako.

Huwezi ondoa ujinga kwa kutoa elimu ya kikoloni ambayo ni mifupa iliyooza ambayo haiwezi kutumika tena. Haina uhai. Kama mimi nimuongo nisahihishwe hivi leo ikiwa kijana aliyemaliza Shahada yake ya awali katika masuala ya Compyuta kama anaweza hata kutengeneza hiyo kompyuta. Sitaki kuulizia habari za magari au masuala ya madawa. Hapo ndipo ninachoongea kinaweza onekana ni kweli.

Ujinga hautaondolewa na elimu iliyokuwa ni mifupa iliyozikwa katika kaburi la ujinga.

Magufuli, Maradhi hayataisha ikiwa tutaendelea kutumia teknolojia ya adui zetu. Leo UKIMWI, kesho SARATANI, Mtondogoo HOMA YA INI. Hapo ndipo wenye akili wanaelewa kuna mchezo.

Kabla hatujapigana na adui lazima tujue tutamfukuzia wapi. Ahaa!. Sasa tumeelewana.

Zipo nchi tunaweza kuwafukuzia umasikini wakapambane nao huko. Zipo nchi tunaweza zifukuzia maradhi na Ujinga zikapambane nazo huko.

Kama Wakoloni walivyotuletea Adui hao. Sasa tutafute pakuwapelekea.

Hapo ndipo tunaona nafasi ya UJasusi Katika misheni hii muhimu. UJASUSI WA KIDOLA NA KIUCHUMI ndio tunaona umuhimu wake.

Naomba nirudie kuwa; Hatuwezi kuondoa umasikini bila ya kujua pakuupeleka.

Ili mbingu iwe paradiso basi lazima shetani aondolewe na atupwe duniani.

Ili umasikini. Ujinga, na Maradhi viondoke hapa nchini basi sharti tutafute mahali au nchi za kuzipelekea ujinga wetu, maradhi yetu na umasikini wetu.

Bado sijaeleweka Mhe. Rais.

Sitaki kueleza jinsi ambavyo tungeweza kunufaika na vita vinavyoendelea katika nchi zinazotuzunguka. Mtanitajia ikiwa sitataja nchi hizo ambazo kwa haraka ni Kongo, Somalia, Sudani n.k. Nchi zote hizo zingekuwa sehemu salama kwa kutupia umasikini wetu na Ujinga wetu kama sio maradhi.

Hakuna heshima tutakayopata ikiwa hatutatumia nafasi kama hizo. Si ajabu tukaonekana wahuni na wajinga.

Mimi sina kumbukumbu lakini sitasahau juzi juzi jinsi Waafrika Kusini walivyotufanyia huko kwao. Hayo ndiyo matunda yake.

Nitaendelea hasira zikipungua. Sehemu zipo nyingi za kutupia umasikini wetu

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Morogoro
09/12/2019
 
Back
Top Bottom