Rais Magufuli na ufufuaji wa viwanda vilivyokufa

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,429
Rais Magufuli anataka viwanda ambavyo vilikuwa vya serikali vikabinafsishwa na kisha vimekufa , vitaifishwe na vifufuliwe jambo ambalo bila shaka lina nia njema.

Aidha, pamoja na nia hiyo njema, ni vyema wanaohusika kwenye zoezi hilo kujiuliza yafuatayo ili jambo hilo jema liweze kufanikiwa.

1. Ni lazima wajiulize ni sababu zipi zilifanya viwanda hivyo vibinafsishwe, na kwa nini walipewa hao waliopewa.

2. Inafaa wafanye utafiti kama sababu zilizotumika kuvibinafsisha bado zipo ama laaa!

3. Wanatakiwa wafanye utafiti pia kujua kuwa ni sababu zipi zilizopelekea waliomilikishwa viwanda hivyo kushindwa kuviendesha hata vikafa na kuwa magofu na kujiuliza kama sababu hizo hazipo tena kwa sasa na kama zipo, ni kwa namna gani zitashughulikiwa ili sasa viwanda hivyo viweze kusimama.


4. Inafaa kutafakari pia kuwa baada ya kutaifisha viwanda hivyo, serikali ndio itakayo viendesha au watapewa wawekezaji wengine, na kama itaendesha serikali, ni vyema kufanya utafiti wa namna ambavyo serikali inaweza kuviendesha kwa ufanisi, na kama ni wawekezaji, ni vizuri kujiridhisha kama kuna wawekezaji wako interested kuwekeza kwenye maeneo husika na ni kwa vipi wao wanaweza kuwa na uwekezaji endelevu tofauti na wawekezaji wa hapo awali.

Mwisho, niwatakie kila la heri wote watakaosaidia kufufua viwanda vilivyokufa wakiongozwa na Mh. Rais.


usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
Asubiri kurudishiwa magofu na akiita wengine hakuna anaejitokeza hata mmoja.......nani atupe pesa zake kwa uchumi upi? Na ushindani huu balaaa sanaa!!! Hakunaa......akilazimisha mashirika umma anarudia kitu kile kile.....afufue na pesa zake za mwendokasi aone.......atafukuza woote hakuna kiwanda!! Akimaliza kiwanda arudishe nyumba za serikali!
 
Na kuongezea kwa Bwana Bethlehem..viwanda vingi vilitegemea mali ghafi ya mazao ya biashara ambayo kwa sasa ni machache au kama hakuna. Nadhani tunahitaji viwanda ila hatujui viwanda gani vinahitajika. Wazo la viwanda zuri sana sanaa lakini tinahitaji muda mwingine tena kutafiti uwekezaji wake. Bila kilimo hakuna maendeleo ya viwanda. Mh. angepigia debe kwanza kilimo ndio viwanda vijengwe/vifufuliwe au tusubirie awamu ingine. Tukitumia mhemko hapa kwa viwanda kwa siasa zetu nadhani tutakwama. Nachukulia mfano wa Kilimo Kwanza ulivyokwama awamu ya NNE.
 
Back
Top Bottom