Rais Magufuli na Lissu wakutanishwe

Rais Magufuli na Lissu wakutanishwe

pureman2

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
1,491
Reaction score
2,563
Tunaweza kukataa na kupinga Ila dalili zote ziko bayana Taifa limemegeka kisiasa, kihisia, kimitazamo, na kivitendo.

Kuna roho ya ubinafsi na majivuno inazidi kusimika mizizi katika taifa hili. Kuna wanojiona ni bora na wanastahili vyote, na wengine wanajiona kuchukiwa, kutotambulika, kutokuwa na haki hata ya kuheshimiwa mitazamo yao.

Kilichotufikisha hapa hakijaanza leo wala jana. Tunachokishuudia ni matokeo ya roho iliyopaliliwa na kunyeshewa maji kwa muda Sasa. Na kadri tunavyochelewa kuchukua hatua hali itakua mbaya Sana.

Siasa zetu zimekua chanzo Cha utengano huu. Sio kwetu tu siasa imekua chanzo Cha anguko la umoja wa kitaifa bali duniani kote siasa ugawa watu. Hili utokea kwa kuwa siasa pasina shaka ni ulaji na mamlaka. Wahenga husema palipo na ulaji hapakosi fitina, Ila ni wajibu wetu kuonyesha ustaarabu na utu.

Wazee wako kimya, watumishi wa Mungu tayari wamekubali ku take side na kuendeleza mpasuko huu. Wasomi wamekubali kubaki neutral. Wengine wamechagua kuwa kimyaa kabisaa ili kuzipa amani fake familia zao na kujihakikishia mkate mezani. Kifupi njaa na uchu wa madaraka umefubaza kalamu zao na kuamua kuisariti Taifa hili.

Nani anaweza kututoa kwenye janga hili?

Bila kupepesa macho JPM na LISSU wanaweza kulisahidia Taifa hili.

JPM- unazo nyenzo, unawajibika kikatiba, unawajibika kisiasa, na unawajibika kiimani kuongoza juhudi za kulijenga taifa hili na kuziba mpasuko. Kuchukua wajibu huu sio udhaifu na kujishusha Ila ni kuonyesha njia na kuwajibika. Utakumbukwa zaidi ukilifanikisha ili kuliko kuamua kukaa kimyaa. Heri wapatanishi maana wataitwa wana wa Mungu.

LISSU- Kama mwanasiasa unawajibika kikatiba kuilinda amani ya taifa hili. Unawajibika kiimani kusamehe na kuachilia. Unawajibika kiraia kutii na kukubali kunyenyekea mamlaka. Utakumbukwa zaidi kwa kuongoza maridhiano ya kitaifa kuliko kufanikisha mashindano.

Kwa wanaowazunguka wawili hawa, mnao wajibu wa kutuliza majeraha, kuponya nafsi zao, na kusisitiza malidhiano, na sio kuwajaza sifa, hasira na viburi.

Msione kwa kuwa mnafaidika leo kwa kushabikia umwamba huu mkaona haya ndo maisha. Hakika hiyo itakua dhambi kubwa sana mbele za Mungu na Jamii ya Watanzania.

Tunapenda kuona umoja na mshikamano wa taifa hili kuliko uhasama na maumivu tunayoyashuudia leo katika kona nyingi za taifa hili.

Mwisho wa waraka huu, nitoe rai kwa wanajeshi wanobeba silaha kwa jina la Tanzania kamwe mtusaidie kurejesha tumaini na heshima ya taifa hili. Tulisifiwa na mataifa mengi duniani coz jeshi letu liliheshimu uhai wa raia zake , na liliwalinda kwa adui awaye yote. Ila leo ni haibu kuona raia zetu wanauawa na wanajeshi wetu na maafisa usalama. Tafadhari mjizuie, mtangulize weledi na utu na muwalinde raia wa taifa hili bila upendeleo.

Nashusha kalamu yangu chini. Nimetimiza wajibu wangu na ninaomba record iwekwe bayana.

Heri mpatanishi maana ataitwa mwana wa Mungu.

Ainone:

1: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jonh Pombe Magufuli

2: Mh. Tundu Antipas Lissu

3: Marais wastaafu

4: Wakuu wa majeshi ya Tanzania

5: Viongozi wa vyama vya siasa

6: Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Rais akutanishwe na kibaraka wa mabeberu ili iweje? Acheni kumtafutia promo za kitoto hapa. Amekimbia, amejipanga kuichafua nchi yetu kwa kutumiwa na mabeberu wanotaka kuja kuchuma. Hana uzalendo wowote kwa nchi yetu. Yeye aishi huko huko, hatumhitaji.
Tutaijenga upya CHADEMA aliyoibomoa. Let him go to hell
 
Rais akutanishwe na kibaraka wa mabeberu ili iweje? Acheni kumtafutia promo za kitoto hapa. Amekimbia, amejipanga kuichafua nchi yetu kwa kutumiwa na mabeberu wanotaka kuja kuchuma. Hana uzalendo wowote kwa nchi yetu. Yeye aishi huko huko, hatumhitaji.
Tutaijenga upya chadema aliyoibomoa. Let him go to hell
Kauli kama hizi ndio mafuta ya taa katika utambi unaofuka moshi. Natamani kuona Kauli za kujenga na sio kubeza.
 
Lissu hapana kabisa huyo nia yake ovu ni dhahiri mbele ya macho ya kila mmoja ni bora Mbowe ana uzalendo fulani sema amepigwa pin sababu amekuwa mlezi wa vibaraka na mawakala wa shetani huku Lissu na genge lake la kina Robert Amsterdam wakina ndio vinara
 
Wewe unaijua CHADEMA kweli?
Rais akutanishwe na kibaraka wa mabeberu ili iweje? Acheni kumtafutia promo za kitoto hapa. Amekimbia, amejipanga kuichafua nchi yetu kwa kutumiwa na mabeberu wanotaka kuja kuchuma. Hana uzalendo wowote kwa nchi yetu. Yeye aishi huko huko, hatumhitaji.
Tutaijenga upya chadema aliyoibomoa. Let him go to hell
 
Kauli Kama hizi ndio mafuta ya taa katika utambi unaofuka moshi. Natamani kuona Kauli za kujenga na sio kubeza
Ningeelewa kana mtu angependekeza Rais akutane na viongozi wa vyama vya upinzani walioko nyumbani, Mbowe, Zitto, nk; lakini siyo Lissu. Yeye aachwe atimize nia yake aliyonayo kwa taifa let, then tutaona kama atatia mguu Tanzania tena.
 
1605472675583.gif

Baada ya kula kiapo, Urais unaanza kupata joto.
 
Tuijenge nchi yetu, Uchaguzi umepita Watanzania wamefanya uamuzi hakuna sababu ya kupendekeza kutaka kwenda kinyume na Watanzania! Chapa kazi Kwa masilahi ya taifa letu uone Kama wazungu hawatatuogopa!
 
Mkuu, umenena vyema.

Kuna watu wana mtindo wa mbuni wa kuzika vichwa kwenye mchanga na kudai hakuna shida yoyote, lkn kweli ni kuwa shida ipo.

Huyo anayedaiwa hafai, anaweza kuwa na wafuasi wengi na ndo sabb uchaguzi haukuachwa kuwa huru na haki.

Mmoja anaweza kuwa na mamlaka yote lkn akakosa wingi wa watu.. Mwingine akawa na watu wengi bila mamlaka.

Hekima kubwa inahitajika kutatua huo mkwamo
 
Lisu hapana kabisa huyo nia yake ovu ni dhahiri mbele ya macho ya kila mmoja ni bora mbowe ana uzalendo fulani sema amepigwa pin sababu amekuwa mlezi wa vibaraka na mawakala wa shetani huku Lisu na genge lake la kina Robert Amsterdam wakina ndio vinara
Acha kuhukumu. Tulisaidie taifa kuwa na mshikamano . Sote ni ndugu
 
Ningeelewa kana mtu angependekeza Rais akutane na viongozi wa vyama vya upinzani walioko nyumbani, Mbowe, Zitto, nk; lakini siyo lissu. Yeye aachwe atimize nia yake aliyonayo kwa taifa let, then tutaona kama atatia mguu Tanzania tena.
Punguza chuki. Hakuna ushahidi Kama mtu huyu amekua adui kwa Tanzania kwa uzani huo unaousisitiza. Hatua zote za malidhiano zitabarikiwa na wapenda amani.
 
Tuijenge nchi yetu, Uchaguzi umepita Watanzania wamefanya uamuzi hakuna sababu ya kupendekeza kutaka kwenda kinyume na Watanzania! Chapa kazi Kwa masilahi ya taifa letu uone Kama wazungu hawatatuogopa!
Tunatamani kuona taifa linalochapa kazi huku likiwa na mshikamano. Juhudi zifanyike kuziba nyufa zote. Sio sifa wewe kufurahi huku mwezako ana nung'unika.
 
Back
Top Bottom