Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,076
- 136,498
Ni mara kadhaa sasa nimemsikia mtukufu rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, akiwa anazungumzia suala la amani, akiitolea mfano nchi ya Libya kipindi cha Gadafi.
Kwamba mambo huko Libya yalikuwa safi tu. Vijana waliokuwa wanaoa walipewa hela, nyumba, na mengineyo.
Inawezekana kweli walikuwa wanapewa hivyo vitu lakini je, walikuwa wako huru kiasi gani?
Gadafi alikuwa dikteta. Tena dikteta mkubwa tu aliyeng'ang'ania madaraka kwa muda mrefu sana hadi walipomfurumsha.
Mtukufu rais Magufuli naye watu wengi wameshaanza kumwona kuwa ni dikteta. Hataki watu wafanye siasa kwenye maeneo yasiyo yao.
Tumeshaona na kusikia watu wakikamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa makosa ya kumtukana/ kusema maneno mabaya dhidi yake.
Tumeona vyombo vya habari vikifungiwa kwa sababu zisizo na mashiko.
Sasa haya mambo ya yeye kuisifia Libya ya Gadafi mimi yananitatiza.
Nabaki najiuliza maswali tu. Ina maana yeye Magufuli alikuwa anamwona Gadafi kuwa ni kiongozi bora aliyeweza kutunza amani huko Libya hadi awe anaisifia sifia hivyo?
Kama Gadafi ndo mmoja wa viongozi ambao Magufuli anawaona kama mfano mzuri wa utunzaji wa amani, watu wakimwona na yeye dikteta watakuwa wanakosea kweli?
Ndo mambo ya ndege wafananao hayo au..?