Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Hapo kwenye kuzuia watu wasijinyonge Kamanda amezurura aisee. Siriazi kabisa anasema hadharani watahakikisha wanawasaka na wanawakamata watu wanaotaka kujinyonga. Sasa utathibitisha vipi mtu ana mpango wa kujinyonga maana hata anaeenda kujinyonga akifika barabarani anavuka kwa uangalifu asije akagongwa.
 
Unatukana ukiwa umejificha nyuma ya keyboard! Angalie usije ukapotea halafu uanze kusingizia kuwa ni TISS kumbe ni sisi wanaume wa shoka tulioapa kumlinda Rais wetu kipenzi
Inamaana Tz imekuwa kama South africa ya makaburu. Nasikia palikuwa na jengo linaitwa Janvorsters Square sasa hivi ni Jo burg central police. Jamaa walikuwa na kitengo kinaitwa special branch, ilikuwa ukidakwa hauonekani tena. Sasa na wewe unatutisha sasa
 
This is too much! Hakuna speech hata moja asiyomtaja mwanamke. Hata hii alikuwa anatafuta entry point ya kumtaja mwanamke!

Mara sijui mbunge siku hizi unapendeza, mke wa kiongozi mwezie mzuri sana, nenda kaongee na mkeo!! Ukifuatilia kiundani kauli hizi zote zina viashiria vya unyanyapaa!
 
Inamaana Tz imekuwa kama South africa ya makaburu. Nasikia palikuwa na jengo linaitwa Janvorsters Square sasa hivi ni Jo burg central police. Jamaa walikuwa na kitengo kinaitwa special branch, ilikuwa ukidakwa hauonekani tena. Sasa na wewe unatutisha sasa
Hutishwi ukitenda kosa si lazima ushitakiwe? Sasa unaogopa nini kushitakiwa?
 
Ni sawa kabisa,tena itungwe sheria Kali dhidi ya vyombo vya habari vinavyohusika kutoa taarifa za uzushi kama hizi ili Iwe mwisho wa upuuzi huu,mtu amekamatwa let's say na polisi mijitu inasema ametekwa,mtu yuko offline kwa matatizo ya mtandao wanadai ametekwa,hatuwezi kufika kwa kuendekeza upuuzi kama huu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa Kiongozi maana Saanane na Azoli bado wapo offline wakifika maeneo ya network wata-beep mkuu
 
Ripoti za kamati za makinikia ziliaminisha jamii kuwa mikataba ya madini iliyoingiwa huko nyuma ziliifanya nchi yetu shamba la bibi. Ripoti hizo zilitangazwa mubashara kwenye tv ili wananchi wajue hilo.

Viongozi wa dini walipata mialiko kwenda kushuhudia uwasilishaji wa taarifa. Vyombo vya habari vilitekeleza wajibu wao kuhabarisha na kuelimisha umma kuhusu awamu hizo zinazotuhumiwa kuuza nchi.

Siku chache baada ya hapo vyombo vya habari vikapigwa marufuku kuandika uhusika wa marais wastaafu na mikataba ya madini! Vivyo hivyo hili la TISS. Inaelekea baadhi ya waajiriwa wa chombo hiki wametumika kwa njia isiyo rasmi kufanya uhalifu na kuwaumiza raia. Sasa chombo kizima kinatuhumiwa kuhusika na utekaji.

Tuhuma zimekuwa nyingi kiasi cha rais kutoa neno. Bahati mbaya sana rais hakujiandaa kutoa neno; neno limemponyoka tu. Angekuwa amejiandaa angeonyesha kwanza kuguswa na matukio ya watu kutekwa na wengine kupotea kabisa.
 
Hapo sawa kabisa maana vyombo vyetu vinachafuliwa hovyo
Mbona ni polisi wenyewe ndio hutwambia wananchi kwamba wasiojulikana ndio wamefanya uhalifu? Utasikia kamanda akisema " Amepigwa risasi na watu wasiojulikana". Sasa kwa nini lawama tupewe sisi tunaopewa tu taarifa kwamba wasiojulikana wamefanya yao?
 
tatizo la nchi siyo chadema.

tatizo ni viwanda alivyoahidi magufuli na hajajenga hata kimoja.

go back to your senses and stop blaming chadema for your failures.
Sidhani kama umenielewa mkuu.

macson
 
Back
Top Bottom