Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Return Of Undertaker,
....................
Nadhani kuna haja ya jeshi letu la Polisi kuwa pro-active,kwa maana kufanya mambo mbele ya muda ili kuweza kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kwa ustadi mkubwa.

Hakupaswa Raisi kutamka kuwa wale wanaozusha watu kupotea wakamatwe ili waisaidie polisi kutoa taarifa,hii ilikua ni kazi ya jeshi la polisi kupima na kuwakamata wahusika wote.Ikiwezekana kuchukua wale wote waliowahi kutoa taarifa hizo hata kama wahusika wamekwishapatikana ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Yapo matukio mengi ya kijinai na kihaini ambayo yamekua yakitangazwa na kikundi kidogo cha wahuni katika mitandao,walishawahi mzushia raisi kifo,walishawahi mzushia CAG mstaafu Profesa Asad kuwa ametekwa,walishawahi kuzusha waandishi wa habari na watu maarufu wametekwa na pengine kuzigusa taasisi za usalama.

Hizi taarifa za kuchafua vyombo vya usalama zinafanywa na kikundi cha watu sio zaidi ya 14,wakiwemo watoto wa viongozi wastaafu,viongozi wa kisiasa na wachache wanaoishi ughaibuni.

Jeshi la Polisi lichukue hatua!
 
Kuna hii tabia ya gari za polisi kutembea bila ya number plates, au plate numbers za kigeni hasa UK, ni tabia ya kupingwa kwa nguvu zote.
 
Mfano ni CAG bwashee mrangi......hapo Ufipa mkishirikiana na Zitto mkazusha kapotea kumbe anakula tende huko Kisarawe!
Mfano mwingine ni Zakaria!Chapa risasi mpaka watu wanagugumia kwa maumivu na sauti zikiwatoka,sisi ni TISS!!!!Shubaamitikenge
 
Well said my beloved president, sasa watakoma watakaoendelea kuhusianisha kupotea kwa watu na vyombo vya usalama!. Maana hadi inakera, usalama gani ambao wana kazi ya kuteka watu wao kila siku!!. Yaani badala ya kuwalinda wawateke, kweli!?
Hata mimi nawashangaa hao TISS,Zakaria asingejihami sasa hivi angekuwa hajulikani alipo!!Kazi ya kukamata watuhumiwa ni kazi ya polisi na si TISS kwa mujibu wa katiba ya JMT!Sasa ni vema raia wakajihami kwa kumiliki silaha na kuwa standby muda wote kama alivyofanya Zakaria!
 
..Mwanaharakati Mdude Nyagali amefungua kesi dhidi ya maofisa wa polisi waliomteka na kumtesa.

..Mdude ameweza kuwatambua maofisa hao kwa majina na force number zao.

..Pia alipeleka malalamiko yake Tume ya haki za binaadamu, lakini tume hiyo imekuwa ikikwepa kufanyia kazi malalamiko ya Mdude.
Sasa hizi sarakasi zote bado jiwe hataki watu wahoji?
 
Back
Top Bottom