Rais Magufuli - Mema Yake Hayaonekani?

Rais Magufuli - Mema Yake Hayaonekani?

Sijawahi kuwa mpambe wa Rais, CCM au Serikali. Kati ya mambo yaliyonikera na yanayoendelea kunikera katika awamu hii ni hawa Wasiojulikana. Hawa kazi yao ni kuteka, kutesa, kuua, kuwaonea na kuwatengenezea watu kesi bandia na kupoteza watu. Huu ni unyama wa hali ya juu usiostahili kuwepo katika jamii iliyostarabika na inayotambua maana ya utu wa mwanadamu. Hawa wanaturudisha kwenye primitivity. Hawa wameleta chuki kubwa miongoni mwa raia na raia dhidi ya Serikali.

Jana tumeambiwa ndege yetu imekamatwa kule South Afrika kwa amri ya mahakama. Mitandaoni kwa maoni ya wengi inaonesha kuna wengi waliofurahishwa na tukio hilo!

Mara kadhaa nimetumia ndege za ATCL ndani na nje ya nchi. Kuna mema mengi kuiona ndege ya Tanzania nje ya nchi, nawe unaenda kupanda ndege ya nchi yako, tena ndege iliyo nzuri. Unapanda na kwenda moja kwa moja nchini kwako, siyo safari yako ni kwenda Dar, lakini kwanza unazungushwa mpaka Addis Ababa au Nairobi. Unapopanda ndege ya nchi yako, na unaenda moja jwa mojga nchini kwako, unaokoa muda, unatengeneza soko la ajira na bidhaa kwa wananchi wenzako, unatangaza taifa lako na kuna ile proud ya nchi yako pia.

Siwasemei wengine, lakini mimi ni miongoni mwa wanaoamini kuwa uamuzi wa kuwa na shirika la ndege lenye ndege na linalotoa usafiri wa anga wa uhakika, ulikuwa ni uamuzi mzuri. Mimi ni kati ya wanaoamini kuwa uamuzi wa kuwa na shirika la reli lenye train za kisasa ni uamuzi sahihi. Mimi naamini tunahitaji usafiri wa majini ulio salama na wa uhakika. Tunahitaji umeme wa kutosha na wa uhakika. Hivi vitu ni vyetu Watanzania wote, siyo vya serikali, Rais au CCM pekee yao. Vinatumia hela yetu sote lakini ili vitendeke ni lazima Wananchi wote tunatakiwa kuwa na ownership ili tuvipende, tuvitunze, tuviboreshe, na tuvihuzunikie vinapokubwa na mikasa.

Kwenye ndege, reli, meli, umeme, nidhamu serikalini, matumizi ya fedha za umma, maamuzi ya haraka, n.k; naipongeza Serikali, nampongeza Rais na nawapongeza Wananchi wote.

Huyu Rais ni binadamu, aweza kufanya makosa, na wakati mwingine ni wakati anapodhamiria kufanya mema. Hilo linapotokea, tusitazame tu yale makosa bali tuitazame ile dhamira yake njema.

Yawezekana kutokana na mambo ya hovyo yanayofanywa na wasiojulikana, yakatufanya kuichukia awamu hii kwa kila jambo hata tukashindwa kuyaona yaliyo mema.

Lakini kwa hakika, kuna mambo ambayo Rais anayasimamia na yanafanyika, ni mambo sahihi. Tunaweza kumlaumu kwa baadhi ya mambo lakini kuna mambo ya msingi kwa Taifa letu anayoyasimamia, tunaweza kuyapuuza leo lakini kuna siku, huenda akiondoka madarakani au atakapoondoka Duniani, tutamkumbuka. Katika yale mema ambayo Rais anayafanya, Mungubayape baraka ili yakapate kuleta faida kwa Taifa letu. Na yale ya wasiojulikana na wasiojulikana, wakapate laana kuu wote wenye kuyatenda na kuyapanga.

Maadui wakubwa wa Taifa letu, kwa serikali, kwa CCM na kwetu wananchi wote, ni hawa Wanaojiita wasiojulikana. Hawa ndio wanaoondoa upendo miongoni mwa wananchi na wananchi walio wengi dhidi ya serikali na watawala.

Hawa wanajua Mbowe, Msigwa, Heche, Mdee, kila siku wanajua wamekula nini, wamelala na kuamka saa ngapi, wameongea na nani na muda gani, wamevaa nini, n.k. lakini hawana uwezo wa kujua ATCL imeshtakiwa, hawana uwezo wa kujua ndege itashikiliwa, hawana uwezo wa kujua korosho hazitauzika, hawana uwezo wa kujua mahindi yakizuiwa kuuzwa nje yatakosa soko, n.k. Hii inatupa ujumbe kuwa, hawa Wasiojulikana wanachokijua ni uovu na siyo kulisaidia Taifa kwa mambo ya msingi kama usalama wa kiuchumi.

Hivi kweli ATCL imeshindwa kuwa na makubaliano ya ulipaji wa madeni yake mpaka kufikia hatua ya kuchukuliwa ndege yetu? Pamoja na yote, ndege yetu kushikiliwa ndani ya nchi rafiki inasikitisha sana! Hawa akina Kabudi hawana diplomasia ya biashara na uchumi? Au wanachojua ni zile diplomasia za miaka ya 60 tu za hata mtu akijikwaa kwenye gogo aliloliwekwa mwenyewe anasema, 'unaona njama za mabeberu na wakoloni!'.

Hii inadhihirisha wazi ukweli ambao wengi wamekuwa wanausema, Rais hana watu sahihi kwa majukumu ya kitaifa. Mara nyingi watu wanaofanya kazi kubwa ya kumsifu boss wao ni wale wenye mapungifu makubwa kiuwezo na ni watu wasiojiamini.

Poleni Watanzania kwa hii aibu ya kidogo chetu kutaka kunyang'anywa.
mwambie kabudi akwambie mema yake maana " alimtoa jalalani"

pia angalia TBC utaona mema yake.
 
Mkuu na kuheshimu sana Umejijengea heshima hapa jf kwamuda mrefu sana waga nafatilia sana comments zako sijui umechomolewa betri au umepatwa na nini anyway mkuu awamu hii sio wasiojulika pekee hawa jamaa wameua uchumi makusudi mazima kwaubishi biashara zimefungwa Sekita binafi ziko juu ya mawe kwakisingizio cha wapiga dili watu uswahili maisha ni magumu sana kupita awamu zote zilizopita Kazi hakuna Kodi ziko juu sana kila kukicha magari ya matangazo ya kodi tena kodi zenyewe zakero tupu kila kona usumbufu watu tunaishi kama wakimbi ndani ya nchi yetu kila kundi kwenye jaimii limebatizwa kwa moto wafanya biashara wakulima wafanyakazi wastaafu ukienda kwenye taasisi za umma ndio usisema ni mateso sana mkuu swala la kupanda ndege moja kwamoja bila kwenda Kenya au Ethiopia au Rwanda mbona Fastjet walilimaliza tatizo ilo tena kwa garama ndogo ya nauli ukilinganisha na ATCL.
Nashukuru kwa kuheshimu michango yangu. Sijachomolewa betri na wala sifikirii kuchomolewa. Siyo mpambe na wala sitakuja kuwa mpambe wa mtu. Nafurahia na kushukuru uhuru niliopewa na Mungu. Naweza kuwa sawa au nikaosea lakini siyo kwa sababu ya kumtukuza mtu. Pekee ninayemuenzi na kumtukuzu ni Mungu pekee yake maana yeye ukuu wake hauhojiwi na binafamu yeyote - ndivyo tulivyofundishwa na tukayashika.

Nilichoeleza ni mambo yale mazuri yaliyofanywa, hata kama yangekuwa ni machache, kama ni mazuri tuyakunali.

Yale ya hovyo nayo tuyaseme pia. Nimeweka mfano wa baya kabisa kwa upande wangu ninaliona, hili la kuteka watu, kutesa, kuua na kuwapoteza. Matendo haya yanaweza kufanywa na shetani au wakala wake tu na siyo binadamu mwenye roho ya Mungu.

Kwenye uchumi wa jumla, na hasa kodi niliwahi kuweka hata makala kadhaa kuliongelea hilo. Adui mkubwa wa uwekezaji ni kodi zisizolipika, kodi zisizowezesha mitaji kuongezeka. Hakuna nchi hata moja Duniani ambayo ilikuwa maskini halafu iliendelea kwa kwa haraka kwa kuwa na kodi nyingi au kodi kubwa. Nchi ambayo iliwahi kubadilika kabisa toka kuwa maskini mpaka kuwa tajiri kwa kipindi kifupi cha miaka 15 ni Dubai, walifanya hivyo kwa kuondoa au kupunguza kodi.

Haikuwa dhamira yangu kuyaelezea yasiyo sahihi yote, zaidi nililenga mambo machache niliyoyaona ni mema lakini hayaonekane kutokana na mabaya yaliyopo. Je, tuyakatae yote, hata mazuri, hata kama yakiwa machache kwa sababu ya yale mabaya mengi?

Utekaji watu - HAPANA
Ninaamini kama mtu akiulizwa, ni aheri nini, usafiri kwenye train ya kisasa, ndugu/rafiki/jirani apotee AU uwe unasafiri kwa pikipiki lakini jamaa zako wawe hai, kila mwenye akili atasema aheri nitembee hata kwa baiskeli lakini niendelee kuwa na jamaa zangu. Tunataka train nzuri lakini uzuri huo hauna maana kama ndugu zetu au mimi mwenyewe sitakuwepo kwa sababu nimenyakuliwa na wasiojulikana.

MADC kuweka watu ndani hovyo - HAPANA
Mimi nimewahi kushuhudia kijana anawekwa ndani kwa sababu amemuuliza swali ambalo DC hakutaka. Sheria ile ni ya hovyo na wala kwa sasa haihitajiki. Nadhani walioiweka sheria ile waliamini kila DC atakuwa na akili timamu na hekima.

TRA kutumika kuwakomoa maadui wa kisiasa - HAPANA
Kuna mambo ya wazi yasiyotaka uthibitisho, katika maeneo kadhaa na kwa nyakati kadhaa, TRA imetumika kama nyundo dhidi ya wapinzani wa CCM. Hiyo ni primitivity.

Teuzi za kikanda - HAPANA
Watu hawataki kuliongelea sana hili lakini tusipolikemea, madhara yake ni makubwa. Watu wenye uwezo wapo nchi nzima, wala siyo kanda moja. Watu wakiwa na madhaifu hujiegemeza kwenye ukanda, ukabila au dini. Viongozi wanastahili kutetewa kwa weledi wao na wala siyo kwa ukanda, ukabila au udini

Wapinzani kufanywa siyo raia wa nchi yetu - HAPANA
Leo kauli hiyo hiyo ikitolewa na kiongozi wa CCM inakuwa sawa, ikitolewa na kiongozi wa CHADEMA, ni kama uhaini.

Hata haya niliyoyaandika, ambayo ni mabaya yaliyoota mizizi awamu hii, siyo pekee lakini tunayataja kwa kuzingatia lengo lililokusudiwa.

Pamoja na hayo yote, bado naamini kuna miradi inayofanywa awamu hii, ikimalizika kwa ufanisi, vizazi vingi vijavyo, vitakiri ulikuwa ni uamuzi sahihi bila kujali mchakato miradi hoyo iliyopitia.
 
Niliponunua kigari changu kwa mara ya kwanza nilisifiwa kuwa nimefanya jambo la maendeleo. Kuna rafiki zangu wawili walinicheka lakini kwa sababu tofauti. Mmoja alinicheka kwa kununua "gari la kike" - gari nililonunua ilikuwa Toyota Starlet yeye akiwa amenunua Toyota Crown. Rafiki wa pili alinicheka kwa kuwekeza kwenye kitu kitakachonipunguzia kipato badala ya kuniongezea, na nilinunua hilo gari kutokana na pesa ya mkopo (personal loan).
Miaka miwili baadae niliwaelewa rafiki zangu hawa wote wawili; lakini kwa experience tofauti. Alieniambia nimejipunguzia kipato alikuwa sahihi MNO, yule mwenye Toyota Crown alijikuta anakosa hata wa kumuuzia hilo gari lake la kiume (Toyota Crown ni 6 cylinder na zinakunywa mafuta balaa).

Hayo "mema" ya Magufuli ni kununua Toyota Crown kwa kuchukua personal loan huku mahitaji yake ya mafuta yanakula 70% ya pato lako kabla hujakatwa marejesho ya mkopo. Miradi yake yote kabisa haina immediate returns, na tuna mahitaji mengi MUHIMU zaidi kuliko hizo "Toyota Crowns" zake.
My two cents worth of opinion.
Good argument.

Mimi pia niliwahi kusema kuwa miradi hii yote mikubwa kuifanya kwa wakati mmoja haukuwa uamuzi sahihi. Dhamira ilikuwa njema lakini namna ya utekelezaji haikuwa sahihi kwa vile inahamisha hela nyingi kwa muda mfupi.

Sasa ndege zimekwishanunuliwa, zimetumia pesa yetu walipa kodi. Hela yetu hii utafurahi ipotee kwa vile utekelezaji wa mradi ulifanyika vibaya? Ufufuaji wa shirika la ndege ilikuwa ni sehemu pia ya dhamira ya CHADEMA kama ingeshinda. Kwa hiyo uamuzi wa ufufuaji wa shirika la ndege ulikuwa sahihi, labda tofauti ni namna ambavyo ingefanyika. Na hata hizo namna nyingine hatuna uhakika kama zingekuwa sahihi.

Ukweli ni kwamba ndege zimekwishanunuliwa. Ni hela yetu imetumika. Ni sisi tunaozipanda. Na siku hizi hata kupata nafasi ni kazi. Ina maana ni huduma tunayoihitaji. Je, tuzichukie kwa vile tu kuna mabaya mengine yanayotuumiza?
 
Ndani ya miaka 58 ya uhai wa taifa letu yametokea mengi sana. Na kama nchi haupo uwezekano wa kutomdai mtu wa nje au kutodaiwa na mtu wa nje.

No man is an ireland, kama sio leo au kesho utajikuta unao uhitaji wa ushirikiano aidha wa kibiashara au kisiasa na taasisi za kimataifa.

Ni uzi wenye kejeli inayohusianisha wasiojulikana na masuala ya kibiashara. Sarcastic Thread.
Jicho lako umelielekeza upande mmoja tu. Negative side.
 
Nadhani mema huwa yanazidiwa na mabaya,mfano unaweza kukaa na mtu kwako miaka 10,ila siku moja tu akilala njaa inafuta yote mema uliyomtendea
 
Good argument.

Mimi pia niliwahi kusema kuwa miradi hii yote mikubwa kuifanya kwa wakati mmoja haukuwa uamuzi sahihi. Dhamira ilikuwa njema lakini namna ya utekelezaji haikuwa sahihi kwa vile inahamisha hela nyingi kwa muda mfupi.

Sasa ndege zimekwishanunuliwa, zimetumia pesa yetu walipa kodi. Hela yetu hii utafurahi ipotee kwa vile utekelezaji wa mradi ulifanyika vibaya? Ufufuaji wa shirika la ndege ilikuwa ni sehemu pia ya dhamira ya CHADEMA kama ingeshinda. Kwa hiyo uamuzi wa ufufuaji wa shirika la ndege ulikuwa sahihi, labda tofauti ni namna ambavyo ingefanyika. Na hata hizo namna nyingine hatuna uhakika kama zingekuwa sahihi.

Ukweli ni kwamba ndege zimekwishanunuliwa. Ni hela yetu imetumika. Ni sisi tunaozipanda. Na siku hizi hata kupata nafasi ni kazi. Ina maana ni huduma tunayoihitaji. Je, tuzichukie kwa vile tu kuna mabaya mengine yanayotuumiza?

Tatizo ni kuwa bado ni hela ya walipa kodi ndio inaendesha ATCL, hai-generate fedha za kujiendesha yenyewe.
 
Nachoelewa ni Kwamba Toka uchaguzi Mkuu 2015 uishe SIO CCM WALA UPINZANI ULIOTAKA KUISHI KAMA WATANZANIA. Kila upande uliendelea na unaendelea kuishi kama wako kwenye Kampeni za Uchaguzi. Kabla hata ya hiki mnachokiona kukandamiza UPINZANI, Hakuna siku upinzan Uliwahi msifu au kupongeza Kazi yoyote aliyofanya Magufuli. Na hakuna siku Wapenzi wa Magufuli waliwahi ponda au kosoa mapungufu yake.Wanasema for every action there is an equal and opposite reaction.Nguvu inayotumika kumpinga Magufuli toka kaingia madarakan ni kubwa mno na hii lazima iende sambamba na nguvu kubwa katika kumsifia au kupongeza. Nachokiona Ni kwa upinzan kutoelewa hiyo kanuni,Ukisema Magufuli anasifiwa sana lzm uangalie na nguvu inayotumika kumponda iko vipi?Kama nilivyosema hapo hawali, Siasa ya 2015 kuja juu tofauti na 2015 kushuka chini. Na hii inachangiwa na MABADILIKO makubwa katika nyanja za technology ambayo yamepelekea wananchi wengi kufuatilia siasa kwa karibu mno Elimu ya uraia ya mtu mmoja mmoja.

Mfano before awamu hii ufuatiliaji wa mambo ya SIASA ulikua mdogo sana,Jambo lolote la kisiasa likitokea ni wachache sana walikua wanadeal nalo na utaona wengi sana kila linalofanyika awamu hii wanakuambia hatujawahi ona awamu zilizopita. Wakusifia wanaona kuna kipya sana na wakuponda wanaona hivyo hivyo. Ni wachache sana wanaweza kuchambua Tofauti ya utawala huu na uliopita kwa FACTS ZAIDI na sio HISIA. Kamfano kadogo,Siku jpm alifanyia mkutano na wanaccm wenzie ikulu.Kuna watu walikuja juu na matusi kibao wakionesha ni ushamba na jambo hili ni geni sana. Lkn je jambo hili ni geni?So utaona kuna kundi ambalo kazi yao ni kupinga kila kitu na kuna kundi kazi yao ni kusifia kila kitu. Na kwa mazingira haya ndio tunaona kundi lingine ambalo upo wewe unahisi Sifa za Magufuli zimezidi kipimo bila kujua hizo sifa zinatokana na juhudi kubwa za kupinga kila kitu.

Mkuu hiki unachokiona hakiji from nowhere, asilimia kubwa kinasababishwa na Makundi Hayo mawili yaani WAFIA CHAMA NA WAFIA UPINZANI.
Nakubaliana nawe 100%.

Ukweli ni kuwa kama tutamsema vibaya Rais kwa kila jambo, jema na baya, hata yeye hawezi kujua abadilike wapi maana lolote alifanyalo ni baya. Ataamua kufanya chochote kwa sababu anajua atalaumiwa tu.

Mazuri tuyakiri. Mabaya aliyoyafanya kwa dhamira njema, tuyatambue. Na yale tunayoyaona ni mabaya tuyaseme, tulalamike na kuyakataa. Kuyakataa yote siyo sahihi, na itamwondolea Rais moyo wa usikivu.
 
Magufuli na Tanzania ni kama mwaume anaemtunza mkewe, tatizo lake moja tu, anakunywa pombe. mwanaume anaemtamani mwanamke wa huyu jamaa atajikita kwenye huo udhaifu wa jamaa kunywa pombe, ataelezea ubaya wote wa kunywa pombe mpaka mwanamke aanze kusononeka na kuanza kumtilia mashaka huyo jamaa. Siku mwanamke atakapohamia kwa huyu mwanaume mpya ndo ataanza kuona madhaifu ya huyo mwanaume mpya, pengine na kujutia kabisa kwanini aliachana na mnywa pombe ambae alikua anamhudumia kila kitu.

hii ndio trick inayotumiwa na CHADEMA. nakumbusha, mimi sina chama chochote, natoa tu maoni yangu kuhusu hawa watu wawili wanaogombania tonge moja.
Unaonaje ukatekwa wewe au tukupoteze ili maendeleo yawepo.
 
Nashukuru kwa kuheshimu michango yangu. Sijachomolewa betri na wala sifikirii kuchomolewa. Siyo mpambe na wala sitakuja kuwa mpambe wa mtu. Nafurahia na kushukuru uhuru niliopewa na Mungu. Naweza kuwa sawa au nikaosea lakini siyo kwa sababu ya kumtukuza mtu. Pekee ninayemuenzi na kumtukuzu ni Mungu pekee yake maana yeye ukuu wake hauhojiwi na binafamu yeyote - ndivyo tulivyofundishwa na tukayashika.

Nilichoeleza ni mambo yale mazuri yaliyofanywa, hata kama yangekuwa ni machache, kama ni mazuri tuyakunali.

Yale ya hovyo nayo tuyaseme pia. Nimeweka mfano wa baya kabisa kwa upande wangu ninaliona, hili la kuteka watu, kutesa, kuua na kuwapoteza. Matendo haya yanaweza kufanywa na shetani au wakala wake tu na siyo binadamu mwenye roho ya Mungu.

Kwenye uchumi wa jumla, na hasa kodi niliwahi kuweka hata makala kadhaa kuliongelea hilo. Adui mkubwa wa uwekezaji ni kodi zisizolipika, kodi zisizowezesha mitaji kuongezeka. Hakuna nchi hata moja Duniani ambayo ilikuwa maskini halafu iliendelea kwa kwa haraka kwa kuwa na kodi nyingi au kodi kubwa. Nchi ambayo iliwahi kubadilika kabisa toka kuwa maskini mpaka kuwa tajiri kwa kipindi kifupi cha miaka 15 ni Dubai, walifanya hivyo kwa kuondoa au kupunguza kodi.

Haikuwa dhamira yangu kuyaelezea yasiyo sahihi yote, zaidi nililenga mambo machache niliyoyaona ni mema lakini hayaonekane kutokana na mabaya yaliyopo. Je, tuyakatae yote, hata mazuri, hata kama yakiwa machache kwa sababu ya yale mabaya mengi?

Utekaji watu - HAPANA
Ninaamini kama mtu akiulizwa, ni aheri nini, usafiri kwenye train ya kisasa, ndugu/rafiki/jirani apotee AU uwe unasafiri kwa pikipiki lakini jamaa zako wawe hai, kila mwenye akili atasema aheri nitembee hata kwa baiskeli lakini niendelee kuwa na jamaa zangu. Tunataka train nzuri lakini uzuri huo hauna maana kama ndugu zetu au mimi mwenyewe sitakuwepo kwa sababu nimenyakuliwa na wasiojulikana.

MADC kuweka watu ndani hovyo - HAPANA
Mimi nimewahi kushuhudia kijana anawekwa ndani kwa sababu amemuuliza swali ambalo DC hakutaka. Sheria ile ni ya hovyo na wala kwa sasa haihitajiki. Nadhani walioiweka sheria ile waliamini kila DC atakuwa na akili timamu na hekima.

TRA kutumika kuwakomoa maadui wa kisiasa - HAPANA
Kuna mambo ya wazi yasiyotaka uthibitisho, katika maeneo kadhaa na kwa nyakati kadhaa, TRA imetumika kama nyundo dhidi ya wapinzani wa CCM. Hiyo ni primitivity.

Teuzi za kikanda - HAPANA
Watu hawataki kuliongelea sana hili lakini tusipolikemea, madhara yake ni makubwa. Watu wenye uwezo wapo nchi nzima, wala siyo kanda moja. Watu wakiwa na madhaifu hujiegemeza kwenye ukanda, ukabila au dini. Viongozi wanastahili kutetewa kwa weledi wao na wala siyo kwa ukanda, ukabila au udini

Wapinzani kufanywa siyo raia wa nchi yetu - HAPANA
Leo kauli hiyo hiyo ikitolewa na kiongozi wa CCM inakuwa sawa, ikitolewa na kiongozi wa CHADEMA, ni kama uhaini.

Hata haya niliyoyaandika, ambayo ni mabaya yaliyoota mizizi awamu hii, siyo pekee lakini tunayataja kwa kuzingatia lengo lililokusudiwa.

Pamoja na hayo yote, bado naamini kuna miradi inayofanywa awamu hii, ikimalizika kwa ufanisi, vizazi vingi vijavyo, vitakiri ulikuwa ni uamuzi sahihi bila kujali mchakato miradi hoyo iliyopitia.
Tatizo analikuza mhusika kwa kutokemea maovu yanayotokea chini ya wateule wake kwa hali yiyote ile lazima achukiwe, utakumbuka yupo mkuu wa wilaya aliwacharaza walimu bakora nadhani kesho yake rais alimfukuza kazi lakni leo hii akifanya kitendo kama hicho kesho yake anapandishwa cheo.
 
Umeongea vyema... ila mema na mabaya yote ni majukumu...

Yanapotendeka mema acheni wananchi wasifie bila kulazimishwa, na yanapotekea mabaya waacheni wananchi wahoji bila lawamana au kuwaona sii wazalendo...

Maji yashamwagika, tuyazoe hivyo hivyo hata kwa tambala la deki...

Cc: mahondaw
 
Maadui wakubwa wa Taifa letu, kwa serikali, kwa CCM na kwetu wananchi wote, ni hawa Wanaojiita wasiojulikana. Hawa ndio wanaoondoa upendo miongoni mwa wananchi na wananchi walio wengi dhidi ya serikali na watawala.
Umehangaika sana mkuu Bams na mada yako hii na kuizungusha zungusha bure.
Hao wasiojulikana hawana utawala wao wenyewe wa kujiamria kufanya wanayoyataka wao.

Na umezungumzia "mambo ya msingi" anayoyafanya Rais ambayo watu watamkumbuka sana kuyafanya.. Haya mandege, mabarabara, mareli, madaraja, maumeme, sote tunayapenda sana na kuyafurahia na tungejivunia sana nayo. Lakini hayo sio "mambo ya msingi" kama ulivyopenda kuyaita.

Heshima ya ubinaadam yeyote ni jambo la msingi popote duniani. Unapomnyima heshima binaadam huyo hata umpe mavitu kiasi gani, ubinaadam wake utakuwa sio kamili.
Usimnyanyase mtu, eti kwa kutafuta njia za kumfurahisha kwa kumpa vitu vizuri. Haki ya kila mTanzania sio ya kuombwa.
WaTanzania tunajivunia umoja na ushikamano wetu, mtu akija na kutaka kutufarakanya eti kwa sabau anatujengea vitu vizuri na ananunua mandege ya kutuleta nyumbani, hili haliwezi kamwe kuwa jambo la msingi.

Rais amedhani kungali mapema katika ngwe yake kwamba watu watatiwa uoga na kunyamaza kwa kufanya vitisho mbalimbali, ikiwemo kuwekwa mahabusu wapinzani na kutunga sheria za kikandamizi. Inaonekana dhahiri kwamba haya aliyafanya maksudi ili watu wanyamaze na afanye lolote analopenda kufanya yeye bila kuhojiwa.

Kwa maoni yangu hapa ndipo alipojiharibia mwenyewe, kwa sababu kutokana na mavitu mengi uliyoyaorodhesha, wananchi wengi wangekuwa upande wake kama pasingekuwepo hayo ya "Msingi zaidi" aliyoyaharibu.

Jambo tu la kulinda raslimali za taifa letu ili zitunufaishe sisi ingetosha kabisa kumjengea heshima kuu hata bila ya kufanya hayo mavitu. Lakini kuwa na hulka za chuki, visasi zidi ya watu usiokubaliana nao mawazo, hii inaondoa sifa aliyostahili kuwa nayo.
 
Mabaya yakizidi mema hata kama yale mema machache ni mazuri kiasi gani maana yake huondoshwa na yale mabaya yaliyokithiri.
Baya moja au mawili tu, na hasa yakiwa yanayokiuka mambo ya "Msingi" kama Haki, Heshima,Utu yanafuta "Mema" hata yakiwa milioni moja, kama hayo ya madege na miundombinu.
 
Sijawahi kuwa mpambe wa Rais, CCM au Serikali.
Pole ndugu yangu, kila kitu kina mwanzo. Wako wengi kama wewe waliokutangulia, hawakuwahi kuwa wapambe wa Rais, CCM au serikali ila when things got tough, their toughness couldn't withstand the test na kwa sasa wao in wapambe wakubwa wa Rais, CCM an serikali. Walikuwepo kabla yako na watakuwepo baada yako...wapo waliozawadiwa na wapo wanaosubiria kuzawadiwa na orodha in ndefu. Karibu, join the team!
Kati ya mambo yaliyonikera na yanayoendelea kunikera katika awamu hii ni hawa Wasiojulikana.
Hata huko kukerwa na yanayoendelea katika awamu hii kama ya Wasiojulikana yana mwanzo na mwisho. Wapo waliokerwa labda hata kukuzidi wewe ila when things got tough, their toughness couldn't withstand the test na sasa hawakerwi tena. Walikuwepo kabla yako na watakuwepo baada yako...wapo waliozawadiwa na wapo wanaosubiria kuzawadiwa na orodha in ndefu. Karibu, join the team!

Bams
labda na mimi niko njiani...siku yangu ya kuwasaliti raia wema wa taifa hili wanaodai utawala wa haki unaozingatia sheria na unaoheshimu Katiba haiko mbali! Labda when things get tough, my toughness won't withstand the test na bila shaka nitaunga mkono kuteswa kwa ndugu zangu, rafiki zangu, jirani zangu na Watanzania wenzangu, kwa kudai tu haki ya kuishi salama kama Katiba yetu inavyoelekeza. May be I too will join the team!

Who knows! Maybe my shadow knows best! But the truth still remains that when the going gets tough, only the tough keep going. Kwa nafsi yangu, utu, haki na uhuru ndizo zinatutofautisha na viumbe vingine duniani na kwa binadamu ndizo nguzo kuu za maisha kama ulivyo msingi wa nyumba. Bahati nzuri hizi zimeorodheshwa kwenye Katiba na hivyo Katiba ikishakiukwa, maendeleo yoyote yale hayana maana!
 
Wewe jiunge, lakini mawazo huru ya wananchi yaheshimiwe. Wasiojulikana hatuwahitaji. Police wafanye kazi zao kuwakamata wahalifu
 
Sijawahi kuwa mpambe wa Rais, CCM au Serikali. Kati ya mambo yaliyonikera na yanayoendelea kunikera katika awamu hii ni hawa Wasiojulikana. Hawa kazi yao ni kuteka, kutesa, kuua, kuwaonea na kuwatengenezea watu kesi bandia na kupoteza watu. Huu ni unyama wa hali ya juu usiostahili kuwepo katika jamii iliyostarabika na inayotambua maana ya utu wa mwanadamu. Hawa wanaturudisha kwenye primitivity. Hawa wameleta chuki kubwa miongoni mwa raia na raia dhidi ya Serikali.

Jana tumeambiwa ndege yetu imekamatwa kule South Afrika kwa amri ya mahakama. Mitandaoni kwa maoni ya wengi inaonesha kuna wengi waliofurahishwa na tukio hilo!

Mara kadhaa nimetumia ndege za ATCL ndani na nje ya nchi. Kuna mema mengi kuiona ndege ya Tanzania nje ya nchi, nawe unaenda kupanda ndege ya nchi yako, tena ndege iliyo nzuri. Unapanda na kwenda moja kwa moja nchini kwako, siyo safari yako ni kwenda Dar, lakini kwanza unazungushwa mpaka Addis Ababa au Nairobi. Unapopanda ndege ya nchi yako, na unaenda moja jwa mojga nchini kwako, unaokoa muda, unatengeneza soko la ajira na bidhaa kwa wananchi wenzako, unatangaza taifa lako na kuna ile proud ya nchi yako pia.

Siwasemei wengine, lakini mimi ni miongoni mwa wanaoamini kuwa uamuzi wa kuwa na shirika la ndege lenye ndege na linalotoa usafiri wa anga wa uhakika, ulikuwa ni uamuzi mzuri. Mimi ni kati ya wanaoamini kuwa uamuzi wa kuwa na shirika la reli lenye train za kisasa ni uamuzi sahihi. Mimi naamini tunahitaji usafiri wa majini ulio salama na wa uhakika. Tunahitaji umeme wa kutosha na wa uhakika. Hivi vitu ni vyetu Watanzania wote, siyo vya serikali, Rais au CCM pekee yao. Vinatumia hela yetu sote lakini ili vitendeke ni lazima Wananchi wote tunatakiwa kuwa na ownership ili tuvipende, tuvitunze, tuviboreshe, na tuvihuzunikie vinapokubwa na mikasa.

Kwenye ndege, reli, meli, umeme, nidhamu serikalini, matumizi ya fedha za umma, maamuzi ya haraka, n.k; naipongeza Serikali, nampongeza Rais na nawapongeza Wananchi wote.

Huyu Rais ni binadamu, aweza kufanya makosa, na wakati mwingine ni wakati anapodhamiria kufanya mema. Hilo linapotokea, tusitazame tu yale makosa bali tuitazame ile dhamira yake njema.

Yawezekana kutokana na mambo ya hovyo yanayofanywa na wasiojulikana, yakatufanya kuichukia awamu hii kwa kila jambo hata tukashindwa kuyaona yaliyo mema.

Lakini kwa hakika, kuna mambo ambayo Rais anayasimamia na yanafanyika, ni mambo sahihi. Tunaweza kumlaumu kwa baadhi ya mambo lakini kuna mambo ya msingi kwa Taifa letu anayoyasimamia, tunaweza kuyapuuza leo lakini kuna siku, huenda akiondoka madarakani au atakapoondoka Duniani, tutamkumbuka. Katika yale mema ambayo Rais anayafanya, Mungubayape baraka ili yakapate kuleta faida kwa Taifa letu. Na yale ya wasiojulikana na wasiojulikana, wakapate laana kuu wote wenye kuyatenda na kuyapanga.

Maadui wakubwa wa Taifa letu, kwa serikali, kwa CCM na kwetu wananchi wote, ni hawa Wanaojiita wasiojulikana. Hawa ndio wanaoondoa upendo miongoni mwa wananchi na wananchi walio wengi dhidi ya serikali na watawala.

Hawa wanajua Mbowe, Msigwa, Heche, Mdee, kila siku wanajua wamekula nini, wamelala na kuamka saa ngapi, wameongea na nani na muda gani, wamevaa nini, n.k. lakini hawana uwezo wa kujua ATCL imeshtakiwa, hawana uwezo wa kujua ndege itashikiliwa, hawana uwezo wa kujua korosho hazitauzika, hawana uwezo wa kujua mahindi yakizuiwa kuuzwa nje yatakosa soko, n.k. Hii inatupa ujumbe kuwa, hawa Wasiojulikana wanachokijua ni uovu na siyo kulisaidia Taifa kwa mambo ya msingi kama usalama wa kiuchumi.

Hivi kweli ATCL imeshindwa kuwa na makubaliano ya ulipaji wa madeni yake mpaka kufikia hatua ya kuchukuliwa ndege yetu? Pamoja na yote, ndege yetu kushikiliwa ndani ya nchi rafiki inasikitisha sana! Hawa akina Kabudi hawana diplomasia ya biashara na uchumi? Au wanachojua ni zile diplomasia za miaka ya 60 tu za hata mtu akijikwaa kwenye gogo aliloliwekwa mwenyewe anasema, 'unaona njama za mabeberu na wakoloni!'.

Hii inadhihirisha wazi ukweli ambao wengi wamekuwa wanausema, Rais hana watu sahihi kwa majukumu ya kitaifa. Mara nyingi watu wanaofanya kazi kubwa ya kumsifu boss wao ni wale wenye mapungifu makubwa kiuwezo na ni watu wasiojiamini.

Poleni Watanzania kwa hii aibu ya kidogo chetu kutaka kunyang'anywa.

Tenda mambo Mazuri 1000 ukafanya moja baya huaribu sifa ya Mazuri yote.Wasiojulikana kama wana nguvu kuliko dola je wanafugwa na nani?Kila MTU amebeba shina za maanguko yake mwenyewe
 
Back
Top Bottom