Mfiaukweli
JF-Expert Member
- Aug 30, 2018
- 5,636
- 8,774
Sijawahi kuwa mpambe wa Rais, CCM au Serikali. Kati ya mambo yaliyonikera na yanayoendelea kunikera katika awamu hii ni hawa Wasiojulikana. Hawa kazi yao ni kuteka, kutesa, kuua, kuwaonea na kuwatengenezea watu kesi bandia na kupoteza watu. Huu ni unyama wa hali ya juu usiostahili kuwepo katika jamii iliyostarabika na inayotambua maana ya utu wa mwanadamu. Hawa wanaturudisha kwenye primitivity. Hawa wameleta chuki kubwa miongoni mwa raia na raia dhidi ya Serikali.
Jana tumeambiwa ndege yetu imekamatwa kule South Afrika kwa amri ya mahakama. Mitandaoni kwa maoni ya wengi inaonesha kuna wengi waliofurahishwa na tukio hilo!
Mara kadhaa nimetumia ndege za ATCL ndani na nje ya nchi. Kuna mema mengi kuiona ndege ya Tanzania nje ya nchi, nawe unaenda kupanda ndege ya nchi yako, tena ndege iliyo nzuri. Unapanda na kwenda moja kwa moja nchini kwako, siyo safari yako ni kwenda Dar, lakini kwanza unazungushwa mpaka Addis Ababa au Nairobi. Unapopanda ndege ya nchi yako, na unaenda moja jwa mojga nchini kwako, unaokoa muda, unatengeneza soko la ajira na bidhaa kwa wananchi wenzako, unatangaza taifa lako na kuna ile proud ya nchi yako pia.
Siwasemei wengine, lakini mimi ni miongoni mwa wanaoamini kuwa uamuzi wa kuwa na shirika la ndege lenye ndege na linalotoa usafiri wa anga wa uhakika, ulikuwa ni uamuzi mzuri. Mimi ni kati ya wanaoamini kuwa uamuzi wa kuwa na shirika la reli lenye train za kisasa ni uamuzi sahihi. Mimi naamini tunahitaji usafiri wa majini ulio salama na wa uhakika. Tunahitaji umeme wa kutosha na wa uhakika. Hivi vitu ni vyetu Watanzania wote, siyo vya serikali, Rais au CCM pekee yao. Vinatumia hela yetu sote lakini ili vitendeke ni lazima Wananchi wote tunatakiwa kuwa na ownership ili tuvipende, tuvitunze, tuviboreshe, na tuvihuzunikie vinapokubwa na mikasa.
Kwenye ndege, reli, meli, umeme, nidhamu serikalini, matumizi ya fedha za umma, maamuzi ya haraka, n.k; naipongeza Serikali, nampongeza Rais na nawapongeza Wananchi wote.
Huyu Rais ni binadamu, aweza kufanya makosa, na wakati mwingine ni wakati anapodhamiria kufanya mema. Hilo linapotokea, tusitazame tu yale makosa bali tuitazame ile dhamira yake njema.
Yawezekana kutokana na mambo ya hovyo yanayofanywa na wasiojulikana, yakatufanya kuichukia awamu hii kwa kila jambo hata tukashindwa kuyaona yaliyo mema.
Lakini kwa hakika, kuna mambo ambayo Rais anayasimamia na yanafanyika, ni mambo sahihi. Tunaweza kumlaumu kwa baadhi ya mambo lakini kuna mambo ya msingi kwa Taifa letu anayoyasimamia, tunaweza kuyapuuza leo lakini kuna siku, huenda akiondoka madarakani au atakapoondoka Duniani, tutamkumbuka. Katika yale mema ambayo Rais anayafanya, Mungubayape baraka ili yakapate kuleta faida kwa Taifa letu. Na yale ya wasiojulikana na wasiojulikana, wakapate laana kuu wote wenye kuyatenda na kuyapanga.
Maadui wakubwa wa Taifa letu, kwa serikali, kwa CCM na kwetu wananchi wote, ni hawa Wanaojiita wasiojulikana. Hawa ndio wanaoondoa upendo miongoni mwa wananchi na wananchi walio wengi dhidi ya serikali na watawala.
Hawa wanajua Mbowe, Msigwa, Heche, Mdee, kila siku wanajua wamekula nini, wamelala na kuamka saa ngapi, wameongea na nani na muda gani, wamevaa nini, n.k. lakini hawana uwezo wa kujua ATCL imeshtakiwa, hawana uwezo wa kujua ndege itashikiliwa, hawana uwezo wa kujua korosho hazitauzika, hawana uwezo wa kujua mahindi yakizuiwa kuuzwa nje yatakosa soko, n.k. Hii inatupa ujumbe kuwa, hawa Wasiojulikana wanachokijua ni uovu na siyo kulisaidia Taifa kwa mambo ya msingi kama usalama wa kiuchumi.
Hivi kweli ATCL imeshindwa kuwa na makubaliano ya ulipaji wa madeni yake mpaka kufikia hatua ya kuchukuliwa ndege yetu? Pamoja na yote, ndege yetu kushikiliwa ndani ya nchi rafiki inasikitisha sana! Hawa akina Kabudi hawana diplomasia ya biashara na uchumi? Au wanachojua ni zile diplomasia za miaka ya 60 tu za hata mtu akijikwaa kwenye gogo aliloliwekwa mwenyewe anasema, 'unaona njama za mabeberu na wakoloni!'.
Hii inadhihirisha wazi ukweli ambao wengi wamekuwa wanausema, Rais hana watu sahihi kwa majukumu ya kitaifa. Mara nyingi watu wanaofanya kazi kubwa ya kumsifu boss wao ni wale wenye mapungifu makubwa kiuwezo na ni watu wasiojiamini.
Poleni Watanzania kwa hii aibu ya kidogo chetu kutaka kunyang'anywa.
Niliponunua kigari changu kwa mara ya kwanza nilisifiwa kuwa nimefanya jambo la maendeleo. Kuna rafiki zangu wawili walinicheka lakini kwa sababu tofauti. Mmoja alinicheka kwa kununua "gari la kike" - gari nililonunua ilikuwa Toyota Starlet yeye akiwa amenunua Toyota Crown. Rafiki wa pili alinicheka kwa kuwekeza kwenye kitu kitakachonipunguzia kipato badala ya kuniongezea, na nilinunua hilo gari kutokana na pesa ya mkopo (personal loan).
Miaka miwili baadae niliwaelewa rafiki zangu hawa wote wawili; lakini kwa experience tofauti. Alieniambia nimejipunguzia kipato alikuwa sahihi MNO, yule mwenye Toyota Crown alijikuta anakosa hata wa kumuuzia hilo gari lake la kiume (Toyota Crown ni 6 cylinder na zinakunywa mafuta balaa).
Hayo "mema" ya Magufuli ni kununua Toyota Crown kwa kuchukua personal loan huku mahitaji yake ya mafuta yanakula 70% ya pato lako kabla hujakatwa marejesho ya mkopo. Miradi yake yote kabisa haina immediate returns, na tuna mahitaji mengi MUHIMU zaidi kuliko hizo "Toyota Crowns" zake.
My two cents worth of opinion.