Rais Magufuli; Mawaziri na Makatibu Wakuu wasiotii ratiba ya kuhamia Dodoma Feb 2017 Watumbuliwe tu

Mr Emmy

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,219
550
Kupanga ni kuchagua tumeshaamua na tumeshapanga kama Serikali na kama Chama Tawala tunahamia Dodoma yeyote anaekwamisha mpango huu lazima atumbuliwe tu. Ratiba ya Serikali kuhamia Dodoma inaonesha ifikapo Feb 2017 Mawaziri na Makatibu wakuu wa wizara zote wanatakiwa kuwa Dodoma ili kutekeleza kwa vitendo Mpango ulioasisiwa na Baba wa Taifa na kuongezewa kasi na Kaka wa Taifa JPM.
 
itapangwa deadline nyingine. hii ya february ni deadline ya 6 so far
 
Kupanga ni kuchagua tumeshaamua na tumeshapanga kama Serikali na kama Chama Tawala tunahamia Dodoma yeyote anaekwamisha mpango huu lazima atumbuliwe tu. Ratiba ya Serikali kuhamia Dodoma inaonesha ifikapo Feb 2017 Mawaziri na Makatibu wakuu wa wizara zote wanatakiwa kuwa Dodoma ili kutekeleza kwa vitendo Mpango ulioasisiwa na Baba wa Taifa na kuongezewa kasi na Kaka wa Taifa JPM.
Kuhamia Dodoma kuna Financial Implication kubwa sana siyo kitu cha kukurupuka tu, Hivi unajua kumhamisha mtumishi mmoja kumtoa Dar kwenda Dodoma ni bei gani? Hivi unajua kujenga mazingira/Miundombinu yatakayobeba Wizara na Taasisi zake zote ni bei gani? Hivi unajua trend ya mapato ya Serikali kwa mwezi yamekaaje? Hivi unajua Wage bill ya nchi yetu inachukua asilimia ngapi ya mapato yote? Hivi unajua Serikali imekusanya jumla Shillingi ngapi mwezi uliopita na zimetumikaje? Hivi unajua Deni la Taifa kwasasa limefikia kiasi gani? Hivi unajua Serikali ikihamisha watumishi wake kwenda Dodoma kwa kuwakopa hii itakua na implication gani kwenye deni la Taifa?

Mimi naamini kwamba Serikali kwasasa haina uwezo wa Kuhamia Dodoma ndani ya miaka mitano, unless labda tuamue kuwaonea watumishi wa umma, na tuamue kukata matumizi kibao muhimu kwa nchi ili kuwekeza kila kitu kuhakikisha Safari ya Dodoma inafanikiwa
 
Kitu cha ajabu ni kwamba hili unalozungumzia lilikuwa linaonekana toka mwanzo, lakini wakubwa wakadharau takwimu na kudhani watahamia fasta fasta. Sisi wengine tuliona toka mwanzo kuwa haiwezekan. Ndo maana yale maigizo ya PM kuhamia Dodoma tulisema tumpe mwezi-matokeo yake hata wiki mbili hakumaliza!

Ni lazima tuwe na mipango realistic, na tuepuke matamko. Chanzo cha matamko ni one-man show. Serikali ifanye kazi kama team. Kosa lao ni kutamka kuhamia Dodoma halafu ndo wakaanza kupiga hesabu za kuhamia. Kumbe walitakiwa waanze na hesabu.
 
Back
Top Bottom