Rais Magufuli, kwanini Nape na sio Bashe?

Rais Magufuli, kwanini Nape na sio Bashe?

Michezo itenganishwe na mambo mengine isichanganywe na habari , yaani kulipaswa kuwepo na wizara ya michezo tu Kama ulivyo wizara ya Fedha au maji , yaani awepo waziri aliyecheza michezo mpenda michezo, Katibu Mkuu awe mwanamichezo bajeti ya wizara ya michezo iwe ya kitosha inayokidhi gharama za kusafirisha Timu kwenda mashindano ya kimataifa nk, Kwa sasa michezo imedorola Kwa sababu mawaziri si wanamichezo pia wapo busy na kufungia Radio, magazeti na mambo mengine huku waziri akiwa Hana mzuka na michezo kabsa, Ni vyema wizara ya michezo iwe peke yake hizo habari zipelekwe kwingine huko wizara ya sayansi na tekinologia.
Naunga mkono hoja
Tungekuwa na wizara mbili
1: Wizara ya Utamaduni na Michezo
2: Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Habari
 
Tutakapofikia wakati wa kuongoza nchi kwa matakwa ya wananchi, basi nchi itafikia maendeleo makubwa sana kwa wakati mfupi sana.

Lakini tusikate tamaa ipo siku neema yan kweli itaifunukia nchi yetu na wananchi watakuwa ndiyo wanaoamua aina ya viongozi wanaowataka na sio kwa mayakwa ya mtu mmoja.

Mwarobaini wa yote hayo ni katiba itakayopatika kwa kuzingatia maoni ya hao wananchi.

WANANCHI AMKENI PAZENI SAUTI KWA UMOJA WENU.
 
Moja ya vitu vinavyomfanya Bashe awe huru kusema kila anachosadiki na kinachosadikiwa na wazalendo wa hii nchi kua no sahihi na kinapaswa kusemwa na raia yeyote mwenye kuitakia hii nchi mema,ni ndugu Bashe(Mb).Hii yawezekana no kwasababu hana tamaa ya pesa na njaa ambayo wabunge na viongozi wengi hasa walioko CCM asilia(achana na akina Lyatonga Mrema,John Momose Cheyo et al).Kwa muda wote amekua ni mtu wa kuikosoa serikali pale inapofanya mambo yanayoonekana kwa namna moja au nyingine kua hayafai kwa mustakabali wa taifa letu.Hayo anayofanya ndugu Bashe ni vigumu sana kupendekezwa na baadhi ya watu walioko kwenye mfumo unaoratibu upatikanaji wa watu wanaotakiwa kuteuliwa na mkuu wa nchi.Watu wengi wanaofanya kinyume na akifanyacho Bashe wengi wao hupendekezwa kushika nyadhifa mbalimbali has a zinazohusiana na teuzi.
 
Back
Top Bottom