Rais Magufuli, kwanini Nape na sio Bashe?

Rais Magufuli, kwanini Nape na sio Bashe?

Azim Sokoine

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2014
Posts
1,488
Reaction score
2,760
Amani iwe juu yenu wakuu,

Nimejaribu kama kuweka comparison juu ya vijana hawa wawili wa CCM.
Ninajiuliza ni kigezo gani rais alichotumia kumchagua Nape kuwa Waziri kamili na kumuacha Bashe bado natafakari. Ikumbukwe Rais Magufuli alichelewa kutangaza baraza lake la mawaziri kwa madai anataka achague watu makini wa kufanya naye, kazi CCM inawabunge zaidi ya 200 hivyo Rais Magufuli alikuwa anachekecha mwenyewe kupata watu makini atakaofanya nao kazi.

Kuna kijana makini huyu ambaye anaitw Hussein Bashe ni moja kati ya mwanasiasa kijana ambaye yuko very smart, kwenye kujenga hoja ubunifu siwezi maliza sifa zake ila kiukweli kwenye masuala ya uongozi amekamilika kwa kweli japo inaweza isiwe 100% the way anavyochangia bungeni na kujenga hoja yupo vizuri CCM inabidi wamwangalie sana, anaweza kuwa hazina kwenye chama chao mbeleni.

Ninachojiuliza hivi kwanini Rais Magufuli hakumuona Bashe na kumuona Nape? wakati ukiwapima watu wawili hawa naona kama Bashe na Nape kuna utofauti mkubwa sana kiuwezo nawaza tu
 
Kama mtu unasahau kuwa anayeteua mawaziri ni rais basi huyo anatakiwa akapimwe! Rais ndiye anayeteua mawaziri, ukitaka Bashe awe waziri basi wewe kuwa rais! Je kuhoji mamlaka halali yaliyotolewa na katibakuna madhara gani kisheria?
 
Aliachwa Kwa kuwa yeye si mnafiki kama wengine
 
Amani iwe juu yenu wakuu,
Kuna kijana makini huyu ambaye anaitwa Hussein Bashe ni moja kati ya mwanasiasa kijana ambaye yuko very smart, kiuwezo nawaza tu

Hussein Bashe ni moja kati ya mwanasiasa kijana ambaye yuko very smart, kwenye kujenga hoja,,,,
Ndugu yangu Azim, hapo penye nyekundu kwa Kiswahili FASAHA husemwa:
Hussein Bashe ni kati ya WANASIASA VIJANA ambao.....
 
Angepita Eddo basi Bashe alikuwa kasha ukwaa uwaziri
 
Michezo itenganishwe na mambo mengine isichanganywe na habari , yaani kulipaswa kuwepo na wizara ya michezo tu Kama ulivyo wizara ya Fedha au maji , yaani awepo waziri aliyecheza michezo mpenda michezo, Katibu Mkuu awe mwanamichezo bajeti ya wizara ya michezo iwe ya kitosha inayokidhi gharama za kusafirisha Timu kwenda mashindano ya kimataifa nk, Kwa sasa michezo imedorola Kwa sababu mawaziri si wanamichezo pia wapo busy na kufungia Radio, magazeti na mambo mengine huku waziri akiwa Hana mzuka na michezo kabsa, Ni vyema wizara ya michezo iwe peke yake hizo habari zipelekwe kwingine huko wizara ya sayansi na tekinologia.
 
Acha kumlinganisha nape na vitu vya kawaida huyo unaemtaja labda akawe waziri Somalia
 
Back
Top Bottom