Rais Magufuli, kwa hili la COVID-19 hujengi Taifa bali unajenga chuki na hasira kwa wananchi

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,219
Mh Rais samani I know una nguvu zote na Mamlaka ila hiki unakifanya kubeza njia za kisayansi na kupingana na watu wa afya wazi kweli unalitesa Taifa na kamwe hulijengi.

Hivi kweli una apa nakujivuna as if huwoni nini kimeikumba dunia kweli basi hata kama niukweli basi kuna mambo bora usiseme.. Watu wanazika ndugu jamaa na marafiki sasa watu wa afya wanashauri wewe kila ukisimama unarusha mawe hivi kweli unafikiri hii ni dalili nzuri ktk utawala wako?

Basi heshim kidogo madaktar wanao pata tabu ni wananch wako watu wanaongea vibaya sana huku kitaa una creat hasira na uchungu hasa kwa watu wamesha poteza ndugu kwa covid 19.

Hivi unafikiri Watanzania tunajisikiaje? Basi funga hosp zote hili liwe taifa la watu wamitishamba dawa za jadi aka tiba mbadala. Mkuu covid anayeyuka at 56c joto la binadam 36-37c huko kujifukiza nihatari sana wengi wamekufa je unaweza jifukiza up to 56c? Nahapandio wengi wanapasemea?

Nafasi yako kubwa sana unatisha watu sana kiasi unafanya watu wote kwenye secta ya afya kushindwa tekeleza wajibu wao vyema. Wakiogopa tumbuliwa. Be on side ya Raia; je, tumwamini nani? Unatukosesha iman na sekta ya afya unaleta chuki kati ya raia na sekta ya afya. Unasababisha majibu ya covid 19 yatolewe fake ili wakufurahishe yes watakufarisha ila nataka kusema even you and your team hamtokuwa salama n hapo ndipo mtakumbuka ushauri mlikwisha ambiwa.

Viongoz wastaafu marais naomba mumshauri Mh Rais watu hatumuelewi kwani alienda somea udaktar wabinadam mbona yeye dokta, mkemia, eng nk kulikoni nini kaz ya taasisi ya Rais? Je anajuwa madhara ya muda mrefu kwakuwa kila mahali?

Mh sema ukweli mega projects umezianzisha zinakomba hazina yote ukifunga nchi tumekwisha na huwo ndio ukweli mchungu. Pili covid 19 kwa wa Tz imetukuta kipindi kibaya sana tayari uchumi ulikuwa kwenye kilima.. Tatu waache watu wa afya atekeleze kaz zao. Usiwarushie mawe na vijembe.
 
Sauti inakwaruza kwaruza Tune Vizuri Lumumba FC.

Kwa taarifa nilizo nazo ambazp nilipewa na mdau mkubwa yaani Daktari Bingwa wa Afya ambaye amespecialize ktk utabibu wa magonjwa ya mapafu( pulmonologist) amekiri kwamba ktk miaka yake kumi ya intensive practice kwenye field yake hapa Bongo kwenye moja ya hospitali kubwa nchini, hajawahi kuona kasi ya vifo na vya homa kali ya mapafu kama ilivyo kuanzia january 2020 hadi sasa. Anakiri kuwa vifo ni vingi kiasi cha kushindwa kuhandle kwwnye ICUs na HDUs.

Na kwamba ikiwa hakuna covidi-19 kama ambavyo serikali ya wanyonge na wanyongaji inavyodai basi kuna homa nyingine ya mapafu ambayo sio corona lakini ipo.

Kwa ndugu na marafiki ambao wameshauguliwa na ndugu zao na hata kupoyeza maisha wakisikiliza hotuba za JPM si tu watamchukia bali watamwombea hata laana.
 
Aliyekuambia Covid hakuna nani!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
GPM hajaka taa dawa matibabu ya kidaktari utakuwa umwmwelewa vibaya na isotoshe miti shamba nayo ni mawazo yake kama alternative(njia mbadala) sasa naisi amny way refers hotun zake utaelewa ana maanisha nn.

pujo
 
Nafasi yako kubwa sana unatisha watu sana kiasi unafanya watu wote kwenye secta ya afya kushindwa tekeleza wajibu wao vyema. Wakiogopa tumbuliwa. Be on side ya Raia; je, tumwamini nani? Unatukosesha iman na sekta ya afya unaleta chuki kati ya raia na sekta ya afya. Unasababisha majibu ya covid 19 yatolewe fake ili wakufurahishe yes watakufarisha ila nataka kusema even you and your team hamtokuwa salama n hapo ndipo m
Thread yako imejaa maneno ya kufikirika na hisia binafsi ukijifanya kusemea walio wengi
Kujifukiza hata kama hakuui wadudu wote,lakin kunasaidia kuwapunguza nguvu na.kuqadhibi,ukishapiga kwa siku 3 tu,kwishney
Nyie mnaopiga makelele tukichungulia chini ya vitanda vyenu lazima tutakuta masufuria ya nyungu tena yale meusii kwa masizi,halafu mnakuja huku kuwachanganya watu
 
Mkuu TumainiEl, sitaki kamwe kukusuta kwa yaliyopita, ngoja tugange yaliyopo na yajayo.

Kichwa cha Mada yako kinajitosheleza kabisa kwa msomaji, hata bila kusoma uliyoandika ndani.

Ngoja na mimi nizame huko, nione kuna nini ulichoandika.

-------------------

Nimerudi baada ya kukusoma mkuu TumainEl, na ninajiuliza sana.

Hivi akili zote hizi na uwezo mkubwa unaoonekana wazi katika bandiko lako hili; vyote hivi wakati ule ulipokuwa unashangilia mambo ya ajabu sana, ulikuwa umezikabidhi kwa nani?

Kuna watu chungu nzima kwenye jukwaa hili waliokuwa timu yako, hivi kati yao bado kuna wanaoweza kurudi na kuzirudia akili zao za kawaida kama ulivyofanya wewe?

Ngoja nami nisiondoke bila kutoa mchango wa kisayansi aliotoa Magufuli kwa upotoshaji mkubwa kama hajawahi kuingia darasa la sayansi.
Anasema, ule mvuke wa kujifukizia una jto la nyuzi 100 sentigredi!

Kwanza itawezekana vipi? Maji yanayochemka ndiyo yanayoweza kuwa na nyuzi kiasi hicho katika hali ya kawaida. Mvuke unaomfikia mtu anayejifukiza kamwe hauwezi kuwa nyuzi 100 sentigredi!

Mara nyingi itakuwa ni pungufu ya hapo, lakini bado utakuwa ni juu zaidi ya nyuzi 37 sentigredi ambazo ndio kawaida ya mwiliu. Utando wote wa puani na mdomoni vingebabuka vingekutana na joto la aina ile..

Na licha ya hayo yote, coronavirus hakai hapo juu ya utando wa mdomo au puani akisubiri ababuliwe na joto la kujifukiza. Crona yumo ndani ya sel mwilini akiamrisha seli hizo zizalishe kwa wingi corona wengine, huku seli hizo zikiharibiwa.
Sayansi inaeleza kwamba mwili wa binaadam una njia za kujikinga. Joto lililojuu kidogo, litarekebishwa ili mwili upate kulihimiri (homeostasis), kama sio joto kali sana.

Kwa hiyo, hata kama ule mvuke ungeingia hadi ndani ya mwili, ndani kabisa (hata sijui utapenyeza vipi), ujoto ule ungerekebishwa uwe karibu na nyuzi 37 sentigredi. Corona angeendelea kutamba.

Kuwa Rais aliye na Ph.D. katika somo la sayansi, hakimwongezei mhusika ufahamu zaidi wa sayansi kuwazidi waliosomea eneo husika. Hili anakosa kulifahamu na kutaka kuwaaminisha wananchi wasiokuwa na ufahamu wowote na mambo haya kuwa asemalo rais ndilo sahihi. Na yeye kwa bahati mbaya anapenda sana sifa hizi za hovyo kabisa.
 
Sauti inakwaruza kwaruza Tune Vizuri Lumumba FC.

Kwa taarifa nilizo nazo ambazp nilipewa na mdau mkubwa yaani Daktari Bingwa wa Afya ambaye amespecialize ktk utabibu wa magonjwa ya mapafu( pulmonologist) amekiri kwamba ktk miaka yake kumi ya intensive practice kwenye field yake hapa Bongo kwenye moja ya hospitali kubwa nchini, hajawahi kuona kasi ya vifo na vya homa kali ya mapafu kama ilivyo kuanzia january 2020 hadi sasa. Anakiri kuwa vifo ni vingi kiasi cha kushindwa kuhandle kwwnye ICUs na HDUs.

Na kwamba ikiwa hakuna covidi-19 kama ambavyo serikali ya wanyonge na wanyongaji inavyodai basi kuna homa nyingine ya mapafu ambayo sio corona lakini ipo.

Kwa ndugu na marafiki ambao wameshauguliwa na ndugu zao na hata kupoyeza maisha wakisikiliza hotuba za JPM si tu watamchukia bali watamwombea hata laana.
Hizi kumbukumbu zitakuwepo.

Zitatumika kujua kwa usahihi taarifa zote zilizofichwa na serikali iliyopo kwenye madaraka sasa hivi.

Hata iwe ni miaka kumi ijayo, taarifa sahihi za vifo hivi vingi vinavyofichwa vitajulikana tu.

Hapo ndipo watu watakapoona uharifu wanaofanya watu hawa kwa kutumia madaraka vibaya.

Kuna sababu gani za msingi kuficha taarifa hizi? Inawasaidia nini wao!
 
Yupo tayari nchi nzima mfe ili mradi asifate maneno ya wapinzani hahaha! Mnaongozwa na tahira
 
Back
Top Bottom