Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,874
RAIS MAGUFULI KUWEKA JIWE LA MSINGI MAGOMENI KOTA KESHO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajia kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa nyumba za kisasa eneo la Magomeni Kota Kinondoni hapo kesho jumamosi tarehe 15 April, 2017.
Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi katika eneo hilo mradi ambao unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu ukiwalenga wakazi wa iliyokuwa Magomeni Kota.
Huu ni utekelezaji wa ahadi ya Mh. Rais ya kuwajengea nyumba za kisasa ambazo wakazi hao wataishi kwa miaka zaidi ya minne bure kufidia kadhia waliyopata baada ya makazi yao kubomolewa.
Wananchi wote mnaombwa kujitokeza kwa wingi kesho kuanzia saa 3 asubuhi kumlaki Rais wetu mpendwa.