Rais Magufuli kuwa mgeni rasmi mkutano mkuu wa wakadiriaji majengo Afrika

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa wakadiriaji majenzi Afrika unaotarajiwa kufanyika tarehe 18-19 Agosti, 2016 jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa leo na Rais wa chama cha wakadiriaji majenzi Tanzania (TIQS) Samuel Marwa kuwa Tanzania kwa mara ya kwanza imekuwa mwenyeji katika mkutano huo ukiwa na lengo la kukuza fani ya ukadiriaji majenzi ili mchango wake katika jamii uweze kutambulika.

Amesema mada kuu ya mkutano huo ni kufikia malengo ya maendeleo endelevu na mchango wa huduma za ukadiriaji majenzi hivyo sekta ya ujenzi na hasa miundombinu ni moja ya vipaumbele vilivyoainishwa kama kichocheo cha kuwezesha kufikia malengo ya maendeleo endelevu na kukuza uchumi wa nchi.

“Malengo ya Maendeleo Endelevu yanakusudia kuondoa umaskini na kupambana na udhalimu na kuleta usawa pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kufikia mwaka 2030, hivyo mada hii inaendana na na jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta maendeleo yenye usawa, mafanikio na ustawi wa kila mwananchi”alifafanua Rais huyo.

Aidha, amesema kuwa huduma hizo, zikitumika kwa ukamilifu zitasaidia kupambana na rushwa na uwajibikaji dhaifu kwani huduma hiyo ni nguzo muhimu katika kuchangia ufanisi na udhibiti wa gharama za ujenzi na ukamilishaji kwa muda wa miradi na kupata dhamani ya fedha.

Mbali na hayo Rais huyo ameuomba uongozi wa vyuo tofauti nchini kuanzisha na kuzidi kudahili wanafunzi katika taaluma ya ukadiriaji majenzi ili kutatua changamoto zilizopo.

Nchi zaidi ya 16 za Afrika zilizoko Jumuiya ya Madola pamoja na Angola na Msumbiji zinatarajiwa kushiriki katika mkutano huo.
 
Tutegemee majengo ya NSSF na wenzo kushuka gharama!?
 
Back
Top Bottom