Rais Magufuli kutua Bukoba kesho Jumapili, kuhutubia wananchi Jumatatu

abagabo

Senior Member
Jun 4, 2014
155
168
Wana jamvi, muda huu nipo ndani ya manispaa ya Bukoba. Kuna matangazo yanapitishwa kwenye mitaa ya mji huu yakihusisha ujio WA Magufuli mjini hapa kesho, na kuhutubia Jumatatu kuanzia saa tano hadi saa saba.
=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli anatarajia kuwasili Bukoba Kesho Januari mosi mwaka 2017 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili akitokea mkoani Geita.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo DISEMBA 31 MWAKA 2016 na mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jeneral Mstaafu Salum Kijuu imebainisha kuwa Rais Magufuli atatembelea maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi na baada ya hapo atahutubia mkutano wa hadhara utakaofanyika mjini Bukoba.

Hii itakuwa ni ziara yake ya kwanza kuifanya mkoani Kagera tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Wana jamvi, muda juu nipo ndani ya manispaa ya bukoba. Luna matangazo yanapitishwa kwenye mitaa ya mji huu yakihusisha ujio WA magufuri mjini hapa kesho, na kuhutubia jumatatu kuanzia SAA tano hadi SAA saba.
hapo chacha - tuwaone nshomile!
 
Wahaya kaeni majumbani kwenu.
Watatoka tuu na wengine tutawaleta na malori toka Chato, Shinyanga na Mwanza. Pia Diamond, Christian Bella na Saida Karoli tunaweza kuwapandisha jukwaani ili kuwapa burudani la nguvu kupunguza machungu.
Na pia Lwakatare tunaweza kumuweka ndani kama kuna dalili za watu kutojitokeza kwani atakuwa yeye ndio kawashawishi.
"Sisi" sio wa mchezo mchezo.
 
Umeeleweka vizuri. Kwaheri nshomile! Ngoja tuone nshomile-
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom