Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,646
- 2,911
Hoja dhaifu. Nchi nyingi kuna kampuni binafsi za uzalishaji na usambazaji wa umeme. Nchi kama Japan umeme wote unazalishwa na kasambazwa au na kampuni binafsi au kampuni binafsi zenye ubia na serikali.Kichwa cha habari yako badilisha kimejaa uongo.
Ubinafsishaji dunia nzima haufanyiki kwenye kila kitu.Maji ni bidhaa nyeti na adimu huwezi kuibinafsisha.Biashara ya maji ipo lakini ni ile kama ya maji ya kilimanjaro,Uhai nk ya kufunga kwenye chupa lakini huwezi binafsisha watu wamiliki mito na maziwa na waamue hayo maji wanayasambazaje.
Umeme pia ni swala nyeti huwezi kukabidhi bepari apewe bwawa la kidatu azalishe umeme asambaze nchi nzima kwa pesa yake .Siku mkimtibua anazima switch umeme unakatika nchi nzima anagoma kuwasha hadi msalimu amri kwenye matakwa yake.Kiusalama ni hatari Umeme ni eneo nyeti.Lakini kuuza majenereta ruksa au kujiwekea umeme unaotumia upepo sio maporomolko ya maji au mito mbona inaruhusiwa.Ndio maana hata IPTL wanaotumia mitambo (majenerator makubwa) kuzalisha umeme WAPO
Haya mambo ya kila wakati kusema kwaajili ya usalama wa nchi ndiyo yanalirudisha nyuma Taifa letu. Zamani hata ukitaka kujua JWTZ ina askari wangapi, utaambiwa hutakiwi kujua kwa sababu ya usalama wa nchi. Leo hii taarifa za majeshi ya nchi mbalimbali unazipata mpaka kwenye mitandao.
Zamani hata huduma za simu tuliaminishwa haiwezekani kutolewa na kampuni kwa sababu ya usalama wa nchi. Leo zinatolewa. Ni usalama gani wa nchi uliotokea?
Tuondokane na mawazo mgando.