Rais Magufuli kuibadilisha TANESCO

collezione

JF-Expert Member
Oct 22, 2010
352
178
Na mwandishi wetu.

Promoting private sector will be a permanent solution kwa uchumi wa Tanzania. Kwa vizazi hivi na vijavyo.

MWANZO

Hatuwezi kulilia viwanda vilete ajira. Wakati sector kama umeme na maji, zinaweza kutuletea ajira kubwa. Kuna hoja kubwa na za msingi kuzitumia (exploit) sector hizi ziweze kutengeneza ajira nyingi na za kutosha.

Mpaka sasa Tanesco imeweza kuwafikia sio zaidi ya asilimia 20 ya watanzania wote. Kwa population ya watu milion 50 ina maana Tanesco inahudumia wateja milion 10 tu. Mbali na serikali kutumia hela nyingi kuwekeza Tanesco, sijwahi kusikia hata siku moja Tanesco imefanikiwa kujiendesha yenyewe. Umeme ni kichaka kingine kinachosababisha serikali kukopa fedha nyingi nje kuisaidia Tanesco. Inasababisha hata deni la taifa kuwa kubwa. Mbali na kashfa ambazo haziishi (dowans, Richmond, escrow).

NINI KIFANYIKE

  • Huduma ya Umeme inatakiwa iwe ya ushindani kama ilivyo kwenye masiliano. Serikali iruhusu watu binafsi wawekeze kwenye umeme. Swala la umeme kuiachia Tanesco kuwa monopoly, (ambayo kimsingi imesha prove failure kwa mda mrefu) ni kuziminya fursa nyingi za uchumi.
  • Tuangalie mapinduzi ya technology na mawasiliano yaliyoletwa na makampuni ya simu, baada ya serikali kuacha TTCL monopoly. Tigo, airtel, vodacom, halotel, zantel . Kwa ujumla wao wametoa ajira kwa vijana wangapi Tanzania? Je, leo hii tungekuwa na tigopesa au mpesa kama TTCL ingekuwa bado monopoly?
  • Kwa takwimu za mwezi uliopita Tanzania ni nchi ambayo inaongoza Duniani kwa matumizi ya pesa za simu. Takribani watu milioni 21 kila siku wanafanya money transaction kupitia mitandao ya simu. Tuje kwa Tanesco, hawa jamaa wana wateja wangapi wa kuwahudumia kwa siku? kama wateja wao kwa jumla hawazidi milioni 10?
  • Unagundua kwamba Tanesco has low capacity, and imekalia fursa nyingi za uchumi bila sababu. Tanesco iko busy mjini tu, vijijini uko hakuna kitu wala dalili za umeme.
FAIDA
  • Sector ya umeme na maji ikiachiwa kuwa huru, nina uhakika inaweza kutengeneza ajira zaidi ya watu milioni 10. Ni zaidi ya viwanda tunavyovisubiria.
  • Private sector inaleta ushindani mkubwa kwenye soko, ata bei ya bidhaa hupungua. Umeme utashuka bei tukiruhusu hili.
  • kuna vijiji hapa Tanzania kwa miaka 1000 ijayo havitapata umeme. Hata Kama Prof Muhogo akiwa anakesha mikoni kuzunguka. Lakini utashangaa hivyo vijiji mitandao ya simu imefika, vocha wanapata, na bado pesa wanatoa kwenye simu.
  • Deni la taifa litashuka. Serikali ipunguze pesa kufadhili hili shirika, na hizi pesa zipelekwe kwenye sector muhimu kama polisi, barabara, elimu. Ambayo Mh Raisi amehaidi
TUNACHOPASWA KUJUA
  • Hakuna nchi duniani imeshawahi kuwa mfanyabiashara mzuri. Nchi zilizoendelea duniani zinatumia private sector kuwekeza in their behalf. Wamefanikiwa kutawala dunia kupitia private sectors za nchi zao.
  • Inshort Public sector huwa hazina ubunifu na focus kama ilivyo private sector. Na ndo maana ata ukiongelea rushwa. Zaidi utaikuta kwenye mashirika na ofisi za serikali. why? Because nobody cares. Na hii sio Tanzania tu, duniani kote. Serikalini urasimu hauwezi kuisha ata kama Mh Raisi akiwa mkali mpaka mwisho. Kuruhusu uwekezaji huru, unapunguza kichaka cha urasimu na rushwa kwenye huduma za jamii.
  • mbali na kutoa ajira, itaisaidia serikali punguza mzigo kutoa fedha kila siku kwa biashara ambayo imeshindikana. kwa kutegemea Tanesco na Dawasco Miaka 10 ya Mh Raisi itaisha, lakini bado vijijini hakuna umeme wala Maji.
  • Tunahitaji mashirika ya umeme kutembea kila nyumba kutafuta wateja, sio kama ilivyo sasa unaandika barua ya maombi mwezi mzima, na bado rushwa juu unatoa. Transforma inaharibika, unaambiwa tunapeleka maombi makao makuu usubiri mwezi mmoja. Karne hii kweli biashara inaenda kwa style hii?
  • Tusiogope uwekezaji binafsi, na tusione private sector ni adui. Cha msingi ni kuweka mikakati ya kipamoja na kimaslahi kwa pande zote mbili. Mfano, Malaysia miundo mbinu kama umeme, treni, madaraja yamejengwa na watu binafsi. kwa kushirikiana na private sector nchi nyingi zimepiga hatua haraka. cha msingi ni kuweka mikakati mizuri ambayo kila mtu anafaidika.
conclusion
Kwa mtaji wa population ya watu milion 50, Sector ya umeme na maji, inaweza kutengenzea ajira kubwa kuliko viwanda ambavyo bado tunavifikira.
 
Kichwa cha habari yako badilisha kimejaa uongo.
Ubinafsishaji dunia nzima haufanyiki kwenye kila kitu.Maji ni bidhaa nyeti na adimu huwezi kuibinafsisha.Biashara ya maji ipo lakini ni ile kama ya maji ya kilimanjaro,Uhai nk ya kufunga kwenye chupa lakini huwezi binafsisha watu wamiliki mito na maziwa na waamue hayo maji wanayasambazaje.

Umeme pia ni swala nyeti huwezi kukabidhi bepari apewe bwawa la kidatu azalishe umeme asambaze nchi nzima kwa pesa yake .Siku mkimtibua anazima switch umeme unakatika nchi nzima anagoma kuwasha hadi msalimu amri kwenye matakwa yake.Kiusalama ni hatari Umeme ni eneo nyeti.Lakini kuuza majenereta ruksa au kujiwekea umeme unaotumia upepo sio maporomolko ya maji au mito mbona inaruhusiwa.Ndio maana hata IPTL wanaotumia mitambo (majenerator makubwa) kuzalisha umeme WAPO
 
Mkubwa hakuna kitu nyeti duniani kwenye swala la uchumi kwa sasa. Nchi zote unazijua wewe kama India, Malaysia, Australia, Singapore, Marekani, Japan etc. kuna watu binafsi ambao wanazalisha umeme na kusambaza umeme. Na nchi hizi hizi ndo wakuja kutubabaisha na misaada.

Kati ya umeme na mawasiliano (simu ) kipi kina unyeti? Mbona leo tigo, airtel wanatoa huduma za watu kuwasiliana ata nje ya Tanzania na bado usalama upo? Kwanini uhofu usalama wa taifa wakati nchi ina sheria binafsi za kiusalama?
Usiwe na chuki na wafanyabiashara, cha msingi ni kuweka kanuni na taratibu mwanzo wa kufanya biashara.

Mugabe yeye anayekataza kampuni za simu kumilikiwa na private sector kwa ajili ya usalama. Je, nchi yake ikoje kiuchumi na ki technologia? je wanatufikia sisi? Na kiusalama wanatuzidi?

Tunaapoongelea private sector sio lazima aje mzungu, humu ndani kuna wafanya biashara wakubwa wakiwezeshwa wanaweza wakafanya. India kuna mtu anaitwa Ratani Tata, au Ambani, hawa kila mmoja anafanya biashara ya umeme zaidi ya MW 10,000. wana supply miji mikubwa kama Mumbai, Delhi. Na huyo ni mtu mmoja. wakati sisi Tanzania tukiongeza MW 500 tunajisifia tumepiga hatua.

Faida za private sector nimeainisha hapo juu. innovation ikiwa moja wapo
 
Jamani Mimi naomba ushauri nimelipia umeme miezi minne iliopita na sijapata hadi Leo ukiwauliza sababu haziishi sasa waugwana nipeni njia itakayo nisaidia Mimi kupata umeme pasipo rushwa
 
Tusirukie vitu bila kujua athari zake kubwa kwa wateja. Hayo mataifa makubwa mengi sasa hivi yamegundua kwamba walifanya makosa makubwa sana kubinafsisha huduma muhimu za maji na umeme.

Privatisation of energy industry was a mistake, Ed Miliband suggests

Na mwandishi wetu.

Promoting private sector will be a permanent solution kwa uchumi wa Tanzania. Kwa vizazi hivi na vijavyo.

MWANZO

Hatuwezi kulilia viwanda vilete ajira. Wakati sector kama umeme na maji, zinaweza kutuletea ajira kubwa. Kuna hoja kubwa na za msingi kuzitumia (exploit) sector hizi ziweze kutengeneza ajira nyingi na za kutosha.

Mpaka sasa Tanesco imeweza kuwafikia sio zaidi ya asilimia 20 ya watanzania wote. Kwa population ya watu milion 50 ina maana Tanesco inahudumia wateja milion 10 tu. Mbali na serikali kutumia hela nyingi kuwekeza Tanesco, sijwahi kusikia hata siku moja Tanesco imefanikiwa kujiendesha yenyewe. Umeme ni kichaka kingine kinachosababisha serikali kukopa fedha nyingi nje kuisaidia Tanesco. Inasababisha hata deni la taifa kuwa kubwa. Mbali na kashfa ambazo haziishi (dowans, Richmond, escrow).

NINI KIFANYIKE

  • Huduma ya Umeme inatakiwa iwe ya ushindani kama ilivyo kwenye masiliano. Serikali iruhusu watu binafsi wawekeze kwenye umeme. Swala la umeme kuiachia Tanesco kuwa monopoly, (ambayo kimsingi imesha prove failure kwa mda mrefu) ni kuziminya fursa nyingi za uchumi.
  • Tuangalie mapinduzi ya technology na mawasiliano yaliyoletwa na makampuni ya simu, baada ya serikali kuacha TTCL monopoly. Tigo, airtel, vodacom, halotel, zantel . Kwa ujumla wao wametoa ajira kwa vijana wangapi Tanzania? Je, leo hii tungekuwa na tigopesa au mpesa kama TTCL ingekuwa bado monopoly?
  • Kwa takwimu za mwezi uliopita Tanzania ni nchi ambayo inaongoza Duniani kwa matumizi ya pesa za simu. Takribani watu milioni 21 kila siku wanafanya money transaction kupitia mitandao ya simu. Tuje kwa Tanesco, hawa jamaa wana wateja wangapi wa kuwahudumia kwa siku? kama wateja wao kwa jumla hawazidi milioni 10?
  • Unagundua kwamba Tanesco has low capacity, and imekalia fursa nyingi za uchumi bila sababu. Tanesco iko busy mjini tu, vijijini uko hakuna kitu wala dalili za umeme.
FAIDA
  • Sector ya umeme na maji ikiachiwa kuwa huru, nina uhakika inaweza kutengeneza ajira zaidi ya watu milioni 10. Ni zaidi ya viwanda tunavyovisubiria.
  • Private sector inaleta ushindani mkubwa kwenye soko, ata bei ya bidhaa hupungua. Umeme utashuka bei tukiruhusu hili.
  • kuna vijiji hapa Tanzania kwa miaka 1000 ijayo havitapata umeme. Hata Kama Prof Muhogo akiwa anakesha mikoni kuzunguka. Lakini utashangaa hivyo vijiji mitandao ya simu imefika, vocha wanapata, na bado pesa wanatoa kwenye simu.
  • Deni la taifa litashuka. Serikali ipunguze pesa kufadhili hili shirika, na hizi pesa zipelekwe kwenye sector muhimu kama polisi, barabara, elimu. Ambayo Mh Raisi amehaidi
TUNACHOPASWA KUJUA
  • Hakuna nchi duniani imeshawahi kuwa mfanyabiashara mzuri. Nchi zilizoendelea duniani zinatumia private sector kuwekeza in their behalf. Wamefanikiwa kutawala dunia kupitia private sectors za nchi zao.
  • Inshort Public sector huwa hazina ubunifu na focus kama ilivyo private sector. Na ndo maana ata ukiongelea rushwa. Zaidi utaikuta kwenye mashirika na ofisi za serikali. why? Because nobody cares. Na hii sio Tanzania tu, duniani kote. Serikalini urasimu hauwezi kuisha ata kama Mh Raisi akiwa mkali mpaka mwisho. Kuruhusu uwekezaji huru, unapunguza kichaka cha urasimu na rushwa kwenye huduma za jamii.
  • mbali na kutoa ajira, itaisaidia serikali punguza mzigo kutoa fedha kila siku kwa biashara ambayo imeshindikana. kwa kutegemea Tanesco na Dawasco Miaka 10 ya Mh Raisi itaisha, lakini bado vijijini hakuna umeme wala Maji.
  • Tunahitaji mashirika ya umeme kutembea kila nyumba kutafuta wateja, sio kama ilivyo sasa unaandika barua ya maombi mwezi mzima, na bado rushwa juu unatoa. Transforma inaharibika, unaambiwa tunapeleka maombi makao makuu usubiri mwezi mmoja. Karne hii kweli biashara inaenda kwa style hii?
  • Tusiogope uwekezaji binafsi, na tusione private sector ni adui. Cha msingi ni kuweka mikakati ya kipamoja na kimaslahi kwa pande zote mbili. Mfano, Malaysia miundo mbinu kama umeme, treni, madaraja yamejengwa na watu binafsi. kwa kushirikiana na private sector nchi nyingi zimepiga hatua haraka. cha msingi ni kuweka mikakati mizuri ambayo kila mtu anafaidika.
conclusion
Kwa mtaji wa population ya watu milion 50, Sector ya umeme na maji, inaweza kutengenzea ajira kubwa kuliko viwanda ambavyo bado tunavifikira.
 
Nakuunga mkono, ila serekali isiruhusu kiholela. Mikataba iwekwe kuwa serekali na haswa usalama wa taifa uwe na say zaidi kwenye kila mwekezaji. Asiweze kuuzima kwa vyovyote vile na serekali pia isimsumbue bila sababu.
Wauzalishe umeme, wausambaze wenyewe kwa njia yao, wawatafute wateja wao wenyewe. Mbona kampuni za simu zina wateja (Maofisi ya serekali) na watu binafsi? Mbona wanalipana bila usumbufu?? Mfano mzuri ni LUKU. Unatumia kiasi chako tu hivyo Tanesco hawakufuati. Ofisi nyingi za serekali hutumia LUKU na hawadaiwi na Tanesco.
Waletwe wawekezaji
 
Suala la Tanesco ku-monopoly soko la umeme ni la kijinga sana. Bila ushindani na kupewa ruzuku ni shida. Japokuwa mimi naona Serikali ingejikita vilivyo katika kuzalisha umeme lakini msambazaji awe mwingine na hata mkusanya mapato iwe ni kampuni nyingine. Si kama ilivyo Tanesco inazalisha, inasambaza na kuuza. Hapana. Tukifagawa hili eneo la usambazaji waje mult-companies wasambaze hapo ndo ushindani utakuwa mkubwa na mlaji kama wewe hapo juu unayeomba kuunganishwa miezi 4 ungeshaunganishwa maana kama huyu angekuzingua ungeenda kwa yule. Naunga mkono hoja 90%.
 
Critique of Electricity Privatisation

Mkubwa hakuna kitu nyeti duniani kwenye swala la uchumi kwa sasa. Nchi zote unazijua wewe kama India, Malaysia, Australia, Singapore, Marekani, Japan etc. kuna watu binafsi ambao wanazalisha umeme na kusambaza umeme. Na nchi hizi hizi ndo wakuja kutubabaisha na misaada.

Kati ya umeme na mawasiliano (simu ) kipi kina unyeti? Mbona leo tigo, airtel wanatoa huduma za watu kuwasiliana ata nje ya Tanzania na bado usalama upo? Kwanini uhofu usalama wa taifa wakati nchi ina sheria binafsi za kiusalama?
Usiwe na chuki na wafanyabiashara, cha msingi ni kuweka kanuni na taratibu mwanzo wa kufanya biashara.

Mugabe yeye anayekataza kampuni za simu kumilikiwa na private sector kwa ajili ya usalama. Je, nchi yake ikoje kiuchumi na ki technologia? je wanatufikia sisi? Na kiusalama wanatuzidi?

Tunaapoongelea private sector sio lazima aje mzungu, humu ndani kuna wafanya biashara wakubwa wakiwezeshwa wanaweza wakafanya. India kuna mtu anaitwa Ratani Tata, au Ambani, hawa kila mmoja anafanya biashara ya umeme zaidi ya MW 10,000. wana supply miji mikubwa kama Mumbai, Delhi. Na huyo ni mtu mmoja. wakati sisi Tanzania tukiongeza MW 500 tunajisifia tumepiga hatua.

Faida za private sector nimeainisha hapo juu. innovation ikiwa moja wapo
 
Na mwandishi wetu.

Promoting private sector will be a permanent solution kwa uchumi wa Tanzania. Kwa vizazi hivi na vijavyo.

MWANZO

Hatuwezi kulilia viwanda vilete ajira. Wakati sector kama umeme na maji, zinaweza kutuletea ajira kubwa. Kuna hoja kubwa na za msingi kuzitumia (exploit) sector hizi ziweze kutengeneza ajira nyingi na za kutosha.

Mpaka sasa Tanesco imeweza kuwafikia sio zaidi ya asilimia 20 ya watanzania wote. Kwa population ya watu milion 50 ina maana Tanesco inahudumia wateja milion 10 tu. Mbali na serikali kutumia hela nyingi kuwekeza Tanesco, sijwahi kusikia hata siku moja Tanesco imefanikiwa kujiendesha yenyewe. Umeme ni kichaka kingine kinachosababisha serikali kukopa fedha nyingi nje kuisaidia Tanesco. Inasababisha hata deni la taifa kuwa kubwa. Mbali na kashfa ambazo haziishi (dowans, Richmond, escrow).

NINI KIFANYIKE

  • Huduma ya Umeme inatakiwa iwe ya ushindani kama ilivyo kwenye masiliano. Serikali iruhusu watu binafsi wawekeze kwenye umeme. Swala la umeme kuiachia Tanesco kuwa monopoly, (ambayo kimsingi imesha prove failure kwa mda mrefu) ni kuziminya fursa nyingi za uchumi.
  • Tuangalie mapinduzi ya technology na mawasiliano yaliyoletwa na makampuni ya simu, baada ya serikali kuacha TTCL monopoly. Tigo, airtel, vodacom, halotel, zantel . Kwa ujumla wao wametoa ajira kwa vijana wangapi Tanzania? Je, leo hii tungekuwa na tigopesa au mpesa kama TTCL ingekuwa bado monopoly?
  • Kwa takwimu za mwezi uliopita Tanzania ni nchi ambayo inaongoza Duniani kwa matumizi ya pesa za simu. Takribani watu milioni 21 kila siku wanafanya money transaction kupitia mitandao ya simu. Tuje kwa Tanesco, hawa jamaa wana wateja wangapi wa kuwahudumia kwa siku? kama wateja wao kwa jumla hawazidi milioni 10?
  • Unagundua kwamba Tanesco has low capacity, and imekalia fursa nyingi za uchumi bila sababu. Tanesco iko busy mjini tu, vijijini uko hakuna kitu wala dalili za umeme.
FAIDA
  • Sector ya umeme na maji ikiachiwa kuwa huru, nina uhakika inaweza kutengeneza ajira zaidi ya watu milioni 10. Ni zaidi ya viwanda tunavyovisubiria.
  • Private sector inaleta ushindani mkubwa kwenye soko, ata bei ya bidhaa hupungua. Umeme utashuka bei tukiruhusu hili.
  • kuna vijiji hapa Tanzania kwa miaka 1000 ijayo havitapata umeme. Hata Kama Prof Muhogo akiwa anakesha mikoni kuzunguka. Lakini utashangaa hivyo vijiji mitandao ya simu imefika, vocha wanapata, na bado pesa wanatoa kwenye simu.
  • Deni la taifa litashuka. Serikali ipunguze pesa kufadhili hili shirika, na hizi pesa zipelekwe kwenye sector muhimu kama polisi, barabara, elimu. Ambayo Mh Raisi amehaidi
TUNACHOPASWA KUJUA
  • Hakuna nchi duniani imeshawahi kuwa mfanyabiashara mzuri. Nchi zilizoendelea duniani zinatumia private sector kuwekeza in their behalf. Wamefanikiwa kutawala dunia kupitia private sectors za nchi zao.
  • Inshort Public sector huwa hazina ubunifu na focus kama ilivyo private sector. Na ndo maana ata ukiongelea rushwa. Zaidi utaikuta kwenye mashirika na ofisi za serikali. why? Because nobody cares. Na hii sio Tanzania tu, duniani kote. Serikalini urasimu hauwezi kuisha ata kama Mh Raisi akiwa mkali mpaka mwisho. Kuruhusu uwekezaji huru, unapunguza kichaka cha urasimu na rushwa kwenye huduma za jamii.
  • mbali na kutoa ajira, itaisaidia serikali punguza mzigo kutoa fedha kila siku kwa biashara ambayo imeshindikana. kwa kutegemea Tanesco na Dawasco Miaka 10 ya Mh Raisi itaisha, lakini bado vijijini hakuna umeme wala Maji.
  • Tunahitaji mashirika ya umeme kutembea kila nyumba kutafuta wateja, sio kama ilivyo sasa unaandika barua ya maombi mwezi mzima, na bado rushwa juu unatoa. Transforma inaharibika, unaambiwa tunapeleka maombi makao makuu usubiri mwezi mmoja. Karne hii kweli biashara inaenda kwa style hii?
  • Tusiogope uwekezaji binafsi, na tusione private sector ni adui. Cha msingi ni kuweka mikakati ya kipamoja na kimaslahi kwa pande zote mbili. Mfano, Malaysia miundo mbinu kama umeme, treni, madaraja yamejengwa na watu binafsi. kwa kushirikiana na private sector nchi nyingi zimepiga hatua haraka. cha msingi ni kuweka mikakati mizuri ambayo kila mtu anafaidika.
conclusion
Kwa mtaji wa population ya watu milion 50, Sector ya umeme na maji, inaweza kutengenzea ajira kubwa kuliko viwanda ambavyo bado tunavifikira.
Wewe ni miongoni mwa wasomi Taifa linaowategemea hongera kwa uchambuzi mahiri Serikali ikiufuata utakumbukwa daima
 
Kichwa cha habari yako badilisha kimejaa uongo.
Ubinafsishaji dunia nzima haufanyiki kwenye kila kitu.Maji ni bidhaa nyeti na adimu huwezi kuibinafsisha.Biashara ya maji ipo lakini ni ile kama ya maji ya kilimanjaro,Uhai nk ya kufunga kwenye chupa lakini huwezi binafsisha watu wamiliki mito na maziwa na waamue hayo maji wanayasambazaje.

Umeme pia ni swala nyeti huwezi kukabidhi bepari apewe bwawa la kidatu azalishe umeme asambaze nchi nzima kwa pesa yake .Siku mkimtibua anazima switch umeme unakatika nchi nzima anagoma kuwasha hadi msalimu amri kwenye matakwa yake.Kiusalama ni hatari Umeme ni eneo nyeti.Lakini kuuza majenereta ruksa au kujiwekea umeme unaotumia upepo sio maporomolko ya maji au mito mbona inaruhusiwa.Ndio maana hata IPTL wanaotumia mitambo (majenerator makubwa) kuzalisha umeme WAPO
Bora umewahi kumweleza. Kuhusu maji umemaliza

Kwa nyongeza kuhusu umeme.

Je umewahi sikia kampuni binafsi linalotaka kusambaza umeme kwa wataje wanaoiibia tanesco? Wawekezaji wote hukimbilia kuzalisha na kuiuzia tanesco ipambane na wateja ambao wapo walio wezi na wasiolipa bili jwa wakati. Hakuna mwekezaji anayetaka kuuza umeme wa rejarea kwa wateja kama ilivyo kwenye makampuni ya simu.

Je umepitia reform process inayoendelea tanesco kabla ya kuandika haya. Ni vyema tukawa na tabia ya kufanya uchunguzi kabla ya kuandika. Hii reform itajibu baadhi ya hoja zako.

Mwisho umesema wenzetu wameendelea kwa kutokuwa na mashirika ya umma. Hebu fafanua maana ni kichekesho. Nchi ipi ya ulaya magharibi haina shirika la umma la maji na umeme?
Ufaransa hawajauza mashirika yao na hata reli na treni ni za umma. Shitika lao la umma la simu linafanya vizuri kuliko ya watu binafsi.
Ethiopia wana mashirika ya umma kuanzia ndege simu nk. yanafanya vizuri.

Pia hii ya wateja milioni kumi bora ukaweka chanzo chake.

Tujiulize hapa kwetu kwa nini hayafanyi kazi kwa ufanisi na tushauri kuliko kuwa na mawazo ya kubinafsisha kila kitu. Hatujafikia hatua hiyo ya ubepari kiuchumi na kijamii.
 
  • mkuu hapa sijaongelea kuuzwa wala kubinafsisha. kwani Mh Mkapa aliporuhusu Mobitel na Tri-tel kutoa huduma za mawasiliano aliuza TTCL? cha kwanza alitambua serikali haikuwa na capacity ya kuwekeza kwenye mawasiliano, kulinganisha na kasi technologia inavyobadilika. Aliruhusu soko huria. Je, leo hii kuna mtu anatamani kuwekewa mkonge wa TTCL tena? ofisi zenyewe za serikali sasa hivi wanatumia vodacom, tigo na airtel, na sio TTCL.
  • Ethiopia ndugu yangu haitukuti kwenye mapinduzi ya mawasiliano, achana na money transaction ambazo Tanzania tunaongoza duniani. Beleive me kwa Africa, Tanzania kwenye mawasiliano ya simu tuko mbali sana. Nchi yetu mpaka vijijini watu wanamiliki simu. Nakukuhakikishia kwenye mawasiliano tuko vizuri (ni kwamba tu sisi waTanzania hatujikubali)
  • Ethiopia mgao wa umeme upo kama kwetu. In fact wana poor standard of living, usione tu ndege zao zinaruka kila kona.
  • Tunaporuhusu wawekezaji binafsi sio lazima wawe wazungu. Mtu kama Bakhresa au Mengi, au MO, akiwezeshwa sidhani kama anaweza kushindwa kusambaza umeme at least kwa mikoa 3. kwa capacity ya Tanasco haiwezi kuhimili mikoa yote ya Tanzania. ingepunguziwa idadi ya coverage na wengine wakasambaza sehemu zingine. Imagine transforma inaharibika Tukuyu unaambiwa mpaka waripoti makao makuu ndo walete. Hivi Karne hii kuna mambo ya time wastege like this?
  • Kumbuka nchi zetu maskini tuna matatizo na challenges nyingi. Barabara bado hazitoshi, walimu wanadai fidia zao, polisi mishahara bado midogo etc. Hizi pesa tunazoendelea kufadhili Tanesco kwenye biashara ambayo hailipi. Si ni bora tuache wajiendeshe wenyewe kama ilivyo TTCL.
  • kupanga ni kuchagua, na uzuri ata Mh Raisi analitambua swala la private sector kuwekeza kwenye uchumi. Alipofungua Daraja la Kigamboni aligusia. Kwamba China kuna Madaraja yamejengwa na private sector, na watu wanatozwa pale wanapopita kwenye daraja husika.
  • Sasa kama Nchi kubwa kama China inaona kwamba serikali haiwezi kufanya kila kitu. inatoa uhuru kwa watu binafsi kuwekeza kwenye Uchumi. Sisi Tanzania kwanini tunataka kila kitu kiongozwe na serikali? mwisho wa siku serikali inazidiwa kwenye mahitaji ya msingi tunaishia kukopa fedha au kuomba misaada ili kuendesha nchi.
 
  • mkuu hapa sijaongelea kuuzwa wala kubinafsisha. kwani Mh Mkapa aliporuhusu Mobitel na Tri-tel kutoa huduma za mawasiliano aliuza TTCL? cha kwanza alitambua serikali haikuwa na capacity ya kuwekeza kwenye mawasiliano, kulinganisha na kasi technologia inavyobadilika. Aliruhusu soko huria. Je, leo hii kuna mtu anatamani kuwekewa mkonge wa TTCL tena? ofisi zenyewe za serikali sasa hivi wanatumia vodacom, tigo na airtel, na sio TTCL.
  • Ethiopia ndugu yangu haitukuti kwenye mapinduzi ya mawasiliano, achana na money transaction ambazo Tanzania tunaongoza duniani. Beleive me kwa Africa, Tanzania kwenye mawasiliano ya simu tuko mbali sana. Nchi yetu mpaka vijijini watu wanamiliki simu. Nakukuhakikishia kwenye mawasiliano tuko vizuri (ni kwamba tu sisi waTanzania hatujikubali)
  • Ethiopia mgao wa umeme upo kama kwetu. In fact wana poor standard of living, usione tu ndege zao zinaruka kila kona.
  • Tunaporuhusu wawekezaji binafsi sio lazima wawe wazungu. Mtu kama Bakhresa au Mengi, au MO, akiwezeshwa sidhani kama anaweza kushindwa kusambaza umeme at least kwa mikoa 3. kwa capacity ya Tanasco haiwezi kuhimili mikoa yote ya Tanzania. ingepunguziwa idadi ya coverage na wengine wakasambaza sehemu zingine. Imagine transforma inaharibika Tukuyu unaambiwa mpaka waripoti makao makuu ndo walete. Hivi Karne hii kuna mambo ya time wastege like this?
  • Kumbuka nchi zetu maskini tuna matatizo na challenges nyingi. Barabara bado hazitoshi, walimu wanadai fidia zao, polisi mishahara bado midogo etc. Hizi pesa tunazoendelea kuwekeza Tanesco kwenye biashara ambayo hailipi. Si ni bora tuache wajiendeshe wenyewe kama ilivyo TTCL.
  • kupanga ni kuchagua, na uzuri ata Mh Raisi analitambua swala la private sector kuwekeza kwenye uchumi. Alipofungua Daraja la Kigamboni aligusia. Kwamba China kuna Madaraja yamejengwa na private sector, na watu wanatozwa pale wanapopita kwenye daraja husika.
  • Sasa kama Nchi kubwa kama China inaona kwamba serikali haiwezi kufanya kila kitu. inatoa uhuru kwa watu binafsi kuwekeza kwenye Uchumi. Sisi Tanzania kwanini tunataka kila kitu kiongozwe na serikali? mwisho wa siku serikali inazidiwa kwenye mahitaji ya msingi tunaishia kukopa fedha au kuomba misaada ili kuendesha nchi.
Ndiyo maana nikakuuliza kama unaelewa REFORMS zinazoendelea huko TANESCO. Ukiijua hutaleta hoja hii hapa. Yote unayoongelea yamejibiwa huko.
 
Umeme ukiwa private sector itakua vizuri ila itakua kama vile mitandao ya simu watu wataanza unit 1 = 50Tshs baada ya muda watu wanakuka na tariff 1 unit = 1500tshs labda ije halotel ya kwenye umeme...
 
Kwa Wiki nne Jumamosi na jumapili kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni wamekuwa wakitukatia umeme full day nini maana yake hata hamu ya kushinda home inakosekana sports zinakuwa ni za kuhadithiwa inakuwa haina maana kulipia ving'amuzi kwani week days hutizami week end umeme hamna matengenezo ya aina gani haya... yaani last sunday ndio tumeachiwa lilikuwa jambo la kushangaza sana... Tanesco iuzwe tu...
 
Ndiyo maana nikakuuliza kama unaelewa REFORMS zinazoendelea huko TANESCO. Ukiijua hutaleta hoja hii hapa. Yote unayoongelea yamejibiwa huko.
Ni aibu Bakhresa anataka MW10, tanesco inalala mpaka Mh Raisi aje atie mkwara. Tanesco haifanyi biashara, wao kukufungia umeme wanaona kama wanakufanyia favour flan.

Sasa hizo reform ziko wapi?
Kwa karne hii biashara ya kubembelezwa utawezaje kutengeneza pesa?

kama hupigani kuongeza wateja, biashara haiwezi ku-survive. Mwisho wa siku utashindwa kujiendesha.

Mh Raisi kama anataka nchi ya viwanda, lazima umeme uwe kibiashara na kwa ushindani. Sio mteja kusumbuliwa na Tanesco. Kuwe na option ya kupata huduma za umeme. Kwa kufanya hivyo bei ya umeme itashuka na kutakuwa na madiliko makubwa kiuchumi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom