Weston Songoro
JF-Expert Member
- Feb 17, 2014
- 2,793
- 1,083
Masaa kadhaa yaliyopita tumepata taarifa za kutenguliwa kwa Mkurugenzi wa TIC kwa sababu hakuwahi kuchukua mshahara wake tangu mwaka 2013. Baadaye nimesoma bandiko moja ambalo linaonesha ni UTETEZI wa Bi JULIETH RUGEIYAMU KAIRUKI ambalo linalalamika kuwa Rais Magufuli kapotoshwa na wasaidizi wake.
Binafsi sikubaliani kabisa na utetezi huo ambao kimsingi hauna hata chembe ya ukweli. Labda hoja ya maana niliyoiona kwenye utetezi huo ni huyo mama kususia mshahara huo kwa madai kuwa hautoshelezi.
Nami nachukua fursa hii kumlaumu sana Kikwete kwani kwa kipindi chote huyu mama akiwa Mkurugenzi wa TIC, alimruhusu kujilipa POSHO ya zaidi ya shilingi milioni 25 kwa mwezi kwa madai kuwa anafidia mshahara mnono aliokuwa analipwa huko South Afrika ijapokuwa ukweli halisi wa mshahara aliokuwa analipwa huko ni Dola za Kimarekani 9,260 na si 15,000 kama alivyodai Bi. Julieth.
Kitendo cha Rais Mstaafu Kikwete kumruhusu huyu mama kujilipa fedha hizo kilimjengea kiburi na kujiona kuwa yeye si wa kawaida. Akawahadaa watu wa chini yake kuwa hachukui mshahara na kwamba anafanya kazi kwa kujitolea wakati anakomba mamilioni ya TIC. Hakika inaniuma sana.
Nina uhakika kama TAKUKURU na vyombo vingine vya dola watafanya uchunguzi wa kina, watabaini madudu mengi sana ya huyu mama. Nimewadokeza hili la kujilipa posho ya Milioni 25 kwa mwezi lakini naamini kuwa yapo madudu mengi sana aliyofanya huyu mama.
Hapo sijagusia safari za mara kwa mara alizokuwa anafanya SA kwa gharama ya serikali huku tija ya safari hiyo ikiwa haionekani na haijulikani alikuwa anaenda kufanya nini huko.