dolomon
JF-Expert Member
- Jun 5, 2018
- 595
- 1,214
Kumekuwa na amshaamsha nyingi sana kwenye vyombo vya habari za kumsifia rais wetu mpendwa kuwa yeye ni bonge la rais haijawahi tokea tangu enzi za baba yetu wa taifa. Kauli hizi zinasemwa sana hasa na wanacha wa CCM hasa wa kizazi cha zama za uhuru na kidogo wale wa miaka ya 70, huku wale wa miaka ya 80 kama mimi wanasema tu ili angalau wapate chochote kile ama ajira au teuzi,maana huyu dingii kajikita kidogo kuwainua vijana viroporopo na wenye uthubutu wa kutukana na kudhalilisha watu kwa ajili ya chama.
Sasa,mimi naungana na wote wanao mpongeza,kwa kweli kuna vitu vikubwa kafanya orodha yake ni ndefu, nikianza kuvieleza hapa nitakesha,wengi wetu tunavijua na hakuna anayepinga.
Kama wahenga wasemavyo, ndege mjanja hunaswa na tundu bovu,au mdharau mwiba huota tende..ni kweli kabisa kuwa mwiba ni mdogo sana,kwa sie tuliowahi kuchunga,mwiba ukikuchoma na kuvunjikia sharti uuchomoe muda huohuo, ukizama ndani zaidi hakikisha unapaka mafuta ya kondoo na uchome na moto kuuvuta usogee juu,usipofanya hivyo uvimbisha maguu utakuwa mkubwa kama matende,kisha utabebwa na mishipa ya damu usafirishwe hadi kwenye moyo kisha uuchome moyo na halafu unazima ghafla na unakufa.
Sasa, rais wangu huyu mpendwa anayetuchunga ana miiba mingi miguuni,imemchoma,bahati mbaya sana anaipuuzia kwa kiburi cha kusifiwa kwamba yeye ni mchungaji mzuri eti anashibisha ng'ombe anajidanganya! Tena anajidanganya kweli kweli....Naomba niitaje miiba michache ambayo imo miguuni ni ishaanza kukuza matende. Suala la ajira,amekuwa akiajiri kwa kustukiza,watu wachache tu wengio wao ni makada...hilo tunalijua vizuri tu, sasa mwak huu katangaza kuajiri walimu 12,000 wakati huu wa uchaguzi,eti anadhani ni karata dume,wanachi wamebadilika sana, sio wajinga kama unavyodhani.
Pili,mwiba wa kutopandisha madaraja na kuongeza mishahara...kwa kigezo tunajenga miundo mbinu. Huu ni mwiba mbaya..tena upo deep kwenye muscles.Wafanyakazi wanmchekea tu,lakini wanalao rohoni. Hivi anajua kuwa wafanyakazi wamekuwa masikini kweli tangu huyu bwana achukue ofisi,mishahara imesimama,maisha yamezidi kuwa magumu kwa wafanyakazi,hawakopesheki tena na kuna ndoa za wafanyakazi zimekufa,watu wameacha shule,wengine wana stress za kujiuwa. Siku za meo mosi anaongea vitu vya kitoto kabisaaaa huyu mzee mbona atajuta...wait and see.
Miiba mingine ni ile ya vyombo vyake vya dola,uonevu kwa watu,wanabambikiwa kesi,watu wanajifanya kama hawaoni tu,mingine utaongezea na wewe.
Asilewe sifa wajumbe tunamsubiria tu huku,akumbuke waliompitisha ni CCM, huku kitaa mara hii atashangaa zinapigwa za hasira,tutaona hao ma DED, Ma DC na polisi kama watambeba tena. Na uzuri wafanyakazi ndio wanasimamia uchaguzi. Octoba kuna mtu ataimba haleluya.
Ongezea kama kuna mwiba mwingine unaujua.