Rais Magufuli iboreshe Taasisi ya Usalama wa Taifa

Rais Magufuli iboreshe Taasisi ya Usalama wa Taifa

Status
Not open for further replies.
kwa taarifa yako, hawa hawa unaowasema ndio walio amua kufukua makaburi wakampa
mchongo mkulu wa kaya, kwani wao walikuwa wanjua kila kitu. Asanteni sana kwa kazi yenu ya
Kiweledi wa kiwango cha hali ya juu.
Tatizo kuna nyumbu wengi sana,mambo mengine hayana umuhimu wa kuanzishia nyuzi
 
TISS wanafanya kazi yao vizuri kuliko hata mnavyodhani. Tatizo tulilokuwa nalo ni dhamira ya Kiongozi Mkuu wa Nchi. Tumuunge mkono Rais wetu na tuwe wamoja sisi kama Watanzania, Tanzania mpya inakuja!
Tanzania mpya ya kuua na kukamata wanaokosoa serikali....?
 
TISS wanafanya kazi vizuri sana na taarifa hizi zote zipi mezani kwa wakubwa kwa mujibu wa sheria ya TISS ya mwaka 1996.

Suala la kufanyia kazi taarifa za TISS ni suala kingine kwa issue za kitaifa.Hata mengine ya kikanda na huku chini hakuna shida yanashughulikiwa vizuri tu!!

Viongozi waliopewa dhamana ndiyo shida nchi hii hakuna kingine!! Wanatakiwa kuchunguzwa na kushistakiwa wakibainikiwa kuwa na tuhuma!
 
TISS inapaswa kuboreshwa katika maeneo mengi
Tuwe na shirika la ujasusi wa kiuchumi na maslahi ya nchi
tuwe na shirika la ujasusi kwa masuala ya utawala yaani Core intelligency
tuwe na shirika la ujasusi wa teknolojia ambalo litakuwa huru kwenye kufanya tafiti na kupendekeza njia bora za kushughulikia masuala ya kisayansi na tafiti zake
kuwa na shirika la ujasusi ambalo litakuwa na nguvu kubwa ya kiuchunguzi kwa mwenendo wowote wa ukiukwaji wa maadili ya viongozi....

Nimewaza kwa sauti tu
 
nakubaliana na hoja kabisa. Haya mambo ya kurudisha kina lowassa ndani tusahau. Hawa wazee wametupiga sana.
Nathani tubadili katiba na maraisi washtakiwe.
System iwe check and balance ilikuzuia madudu haya ya kishenzi.
Lakni bado naikubali TISS ndio tassisi iliyobakia yenye maana Tanzania sema hawana meno. Hawa wapewe meno.
 
Hasa upande wa serikali kuwa na vitengo vya tafiti kila idara itasaidia sana. Hatuwezi kuendelea bila kuwa na vitengo vya tafiti serikalini...
 
Ajira za TISS zingewekwa wazi watu waombe kwa sifa zilizowekwa kama ilivyo kwa mashirika yaliyobobea kama MOSSAD, CIA. Wao wafanye vetting ya kutosha kwa wale watakaoona wanafaa, na iwe ni kwa field zote zinazomhusu binadamu. Huku nje hatujui huwa wanatumia vigezo gani kuajiri na kwa sifa zipi, ila niliwahi kudokezwa tu kwamba chama kubwa kikisema huyu sawa basi unaajiriwa, hebu kwa mfano wa bashite, kama kweli ni mtu wao, basi unaweza ona jinsi taasisi yetu hiyo ilivyo.
Yaani bashite anapakaza mavi vibaya vibaya.
 
NO! TISS hawafanyi vzr kazi yao..makosa makosa mengi sana, kwny teuzi,uwekezaji, ukusanyaji taarifa nk..ukikuta DSO anayeweza kuandaa hata page 1 ya ripoti bs tungekuwa mbali sana kiuchumi na kijamii..tusingekuwa na maloloso haya!

Tatizo la wachangiaji wengi humu jukwaani hawajui kitu ila wanajifanya wanajua kila kitu na wanaona kila kosa.Hakuna kati yetu anayejua kila kitu.Ukiondoa MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi TISS wamefanya kazi nzuri mno kutufanya tuwe hivi tulivyo.

Chunguzeni jirani zetu wote wanaotuzunguka utaelewa nasema nini.
 
Muda unaenda Bado nyie mnapanga na kushauri utafikiri nchi mpya. Raisi anaomuda kapewa baada ya kunadi ilani ya chama chake, na huu muda mshauri atekeleze ahadi na apunguze Sanaa na maigizo Hali za wananchi zinazidi kuporomoka na lazima akubari wananchi wajiletee maendeleo wenyewe serikali ni wawezeshaji tu.

Baada ya kuwekwa hadharani ripoti ya mchanga wa madini na kuonyesha namna Taifa lilivyokuwa linapoteza kiasi kikubwa cha mapato, ni wazi sasa kunahitajika umakini mkubwa kulinda rasilimali za nchi ziweze kuwafaidisha watanzania kwanza kabla ya mengineyo.

Inawezekana kulikuwa na ripoti za uvushaji huu kwa muda mrefu na hazikuwahi hata kuguswa na waliotangulia, lakini pia ninaona kuna unyonge kwenye taasisi yetu ya Usalama wa Taifa ambapo kisheria wanategemea vyombo vingine katika uchukuaji hatua kwenye mambo muhimu ya taifa. Kisheria Usalama wa Taifa wanaishia kukusanya taarifa na kuziwasilisha kwa waziri mwenye dhamana ambaye naye ana utashi wa kuamua ama kutoamua kuzipeleka kwenye maamuzi.

Hivyo inawezekana kabisa Wizara hiyo kushikwa na mtu ambaye hajui dhima na umuhimu wa Usalama wa Taifa hivyo kukawa na mwendelezo wa hovyo hovyo katika maamuzi.

Ni wakati sasa rais akaona umuhimu wa kuiboresha taasisi hii kwa kuipa nguvu hasa kuchukua hatua kwa maslahi ya Taifa pale inapobidi.

Viundwe vitengo vya kufanya tafiti kwa kila maamuzi ya kisera kwa Taifa.

Viundwe vitengo vya kushirikisha raia kusaidia taasisi kufanikisha oparesheni zake bila kuvunja sheria za nchi....

Kwa sasa naweka haya machache, kwani nimeona yana umuhimu sana kuzuia makosa kama haya ya kina Muhongo kushindwa kusimamia Wizara zao yasijirudie
 
Kwa hali ilivyo sasa, kuna umuhimu wa kuwa na taasisi zaidi ya moja na zenye majukumu tofauti kwenye eneo la ushushu na kila taasisi iruhusiwe kupepesa macho kwa mwenzake na kurupoti mahali husika pale inapo gundua kuna hujuma.

Pia vyombo hivi vipewe mamlaka ya kupepesa macho kwa MTU yoyote hata Rais wa Jamhuri ya muungano na kurippti hatari kwa vyombo husika pale kunapokuwa na jambo lisilo sahihi.

Leo tunalia na mikataba, rushwa, ubafhilifu tc kwa sababu chombo chetu kimetekwa au kimewekewa mipaka ya kutochungulia baadhi ya mambo au kuyapuuza hata kama ni hatarishi kwa taifa...

Pia ujasusi wa nje hasa kwenye eneo la uchumi uongezewe nguvu na nyenzo has a technologia ..
Tuwe kama Marekani wao wana taasisi 17.
 
Tatizo la wachangiaji wengi humu jukwaani hawajui kitu ila wanajifanya wanajua kila kitu na wanaona kila kosa.Hakuna kati yetu anayejua kila kitu.Ukiondoa MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi TISS wamefanya kazi nzuri mno kutufanya tuwe hivi tulivyo.

Chunguzeni jirani zetu wote wanaotuzunguka utaelewa nasema nini.
wewe unajua nini, kujifariji kwa failures za za nchi jirani ndo umeona wanafanya kazi nzr?? nchi jirani kila moja ina historia yake, utamaduni wake, tabia zake nk tofauti na nchi yetu..failures zao zina sababu kulingana na mazingira yao! siku zote mm naomba Rais awatizame TISS na kutathmini utendaji wao km una tija kwa taifa letu kwa mazingira ya sasa, kuna kila dalili za kufanya reform kwa TISS before this Pres. we hv lost in every front as a nation! na km walikuwa wanafanya kazi yao ipasavyo halafu mapendekezo yao yanatelekezwa walikaa hapo kufanya nini..? mtu asipofuata ushauri wako unamwachia kazi yake unaenda zako..! uliona nchi gani nyngn hbr ya afisa wa serikali mhasibu (TAKUKURU) au yule masamaki (TRA) ana-accumulate utajiri wa hivyo bila hata kuulizwa??? hiyo ndio kazi nzr unayoisema wanafanya..
 
Niambie Beriscon alikuwa kiongozi wa nchi gani na nini kilitokea kuhusu ulipaji wake wa kodi na yalitekelezwa baada ya muda gani kupita? umesikia nini kuhusiana na uchaguzi wa Marekani na nini kinachoendelea huku.Shukuru kwa mema boresha mapungufu,tusijifanye kuona udhaifu tu.

Bila umakini wa TISS kuna wahuni wangekuwa jengo jeupe muda huu na usingesikia chochote kuhusiana na uhuni unaousikia sasa ukiumbuliwa.
 
Baada ya kuwekwa hadharani ripoti ya mchanga wa madini na kuonyesha namna Taifa lilivyokuwa linapoteza kiasi kikubwa cha mapato, ni wazi sasa kunahitajika umakini mkubwa kulinda rasilimali za nchi ziweze kuwafaidisha watanzania kwanza kabla ya mengineyo.

Inawezekana kulikuwa na ripoti za uvushaji huu kwa muda mrefu na hazikuwahi hata kuguswa na waliotangulia, lakini pia ninaona kuna unyonge kwenye taasisi yetu ya Usalama wa Taifa ambapo kisheria wanategemea vyombo vingine katika uchukuaji hatua kwenye mambo muhimu ya taifa. Kisheria Usalama wa Taifa wanaishia kukusanya taarifa na kuziwasilisha kwa waziri mwenye dhamana ambaye naye ana utashi wa kuamua ama kutoamua kuzipeleka kwenye maamuzi.

Hivyo inawezekana kabisa Wizara hiyo kushikwa na mtu ambaye hajui dhima na umuhimu wa Usalama wa Taifa hivyo kukawa na mwendelezo wa hovyo hovyo katika maamuzi.

Ni wakati sasa rais akaona umuhimu wa kuiboresha taasisi hii kwa kuipa nguvu hasa kuchukua hatua kwa maslahi ya Taifa pale inapobidi.

Viundwe vitengo vya kufanya tafiti kwa kila maamuzi ya kisera kwa Taifa.

Viundwe vitengo vya kushirikisha raia kusaidia taasisi kufanikisha oparesheni zake bila kuvunja sheria za nchi....

Kwa sasa naweka haya machache, kwani nimeona yana umuhimu sana kuzuia makosa kama haya ya kina Muhongo kushindwa kusimamia Wizara zao yasijirudie
Naunga mkono hoja hii muhimu. Usalama wa Taifa wapewe mamlaka zaidi ya KUCHUKUA HATUA FOR THE PUBLIC INTEREST. Pia, ikibidi waweze kuwashirikisha wananchi ktk utekelezaji wa majukumu yao. Hata hivyo nawapongeza sana hawa TISS.
 
Jukumu la karibia National Security Agencies zote duniani ni Kunusa hatari ambayo itaathiri Maslahi ya Taifa na Wananchi wake kisha wanafuatilia na kupeleka Ripoti yao katika Mamlaka husika ambayo ni ya juu na ya mwisho ambayo Kiutendaji huwa ipo chini ya Marais hivyo kama ni lawama technically ziende kwa Marais waliopita ambao hapa wala hatufichi ni Mzee Mkapa na Mzee Kikwete.

Hakuna ambacho kimesikika ile majuzi pale IKULU wakati wa uwasilishwaji wa ile Ripoti ya Madini ( Makinikia ) Idara husika haikujua isipokuwa walifanya Kazi yao kama Utendaji wao unayowataka na ukizingatia kuwa hawana meno zaidi ya yale ya Kunusa ambapo mwenye meno sasa makali huwa ni Bosi wao Mkuu ambaye ni Rais.

Hata hivyo huu ni mtazamo wangu tu na nipo tayari kukosolewa kwa hoja kwani nimehisi kama vile tuna tatizo la kujua hasa nini Majukumu ya hizi Idara Nyeti za Usalama katika nchi nyingi duniani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom