Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 24,482
- 34,530
Baada ya kuwekwa hadharani ripoti ya mchanga wa madini na kuonyesha namna Taifa lilivyokuwa linapoteza kiasi kikubwa cha mapato, ni wazi sasa kunahitajika umakini mkubwa kulinda rasilimali za nchi ziweze kuwafaidisha watanzania kwanza kabla ya mengineyo.
Inawezekana kulikuwa na ripoti za uvushaji huu kwa muda mrefu na hazikuwahi hata kuguswa na waliotangulia, lakini pia ninaona kuna unyonge kwenye taasisi yetu ya Usalama wa Taifa ambapo kisheria wanategemea vyombo vingine katika uchukuaji hatua kwenye mambo muhimu ya taifa. Kisheria Usalama wa Taifa wanaishia kukusanya taarifa na kuziwasilisha kwa waziri mwenye dhamana ambaye naye ana utashi wa kuamua ama kutoamua kuzipeleka kwenye maamuzi.
Hivyo inawezekana kabisa Wizara hiyo kushikwa na mtu ambaye hajui dhima na umuhimu wa Usalama wa Taifa hivyo kukawa na mwendelezo wa hovyo hovyo katika maamuzi.
Ni wakati sasa rais akaona umuhimu wa kuiboresha taasisi hii kwa kuipa nguvu hasa kuchukua hatua kwa maslahi ya Taifa pale inapobidi.
Viundwe vitengo vya kufanya tafiti kwa kila maamuzi ya kisera kwa Taifa.
Viundwe vitengo vya kushirikisha raia kusaidia taasisi kufanikisha oparesheni zake bila kuvunja sheria za nchi....
Kwa sasa naweka haya machache, kwani nimeona yana umuhimu sana kuzuia makosa kama haya ya kina Muhongo kushindwa kusimamia Wizara zao yasijirudie

Kwa hali ilivyo sasa, kuna umuhimu wa kuwa na taasisi zaidi ya moja na zenye majukumu tofauti kwenye eneo la ushushu na kila taasisi iruhusiwe kupepesa macho kwa mwenzake na kurupoti mahali husika pale inapo gundua kuna hujuma.
Pia vyombo hivi vipewe mamlaka ya kupepesa macho kwa MTU yoyote hata Rais wa Jamhuri ya muungano na kurippti hatari kwa vyombo husika pale kunapokuwa na jambo lisilo sahihi.
Leo tunalia na mikataba, rushwa, ubafhilifu tc kwa sababu chombo chetu kimetekwa au kimewekewa mipaka ya kutochungulia baadhi ya mambo au kuyapuuza hata kama ni hatarishi kwa taifa...
Pia ujasusi wa nje hasa kwenye eneo la uchumi uongezewe nguvu na nyenzo has a technologia ..